China: Fursa za biashara, usafiri na masoko

Naomba kujua uliagiza kwa njia gani, nahitaji kuanza hiyo biashara
 
Na mimi nahitaji kuanza biashara ya nguo na urembo kama kuna uwezekano naomba uniunganishe na supplier wanaohusika na hizo bidhaa mkuu
 
Naomba kujua uliagiza kwa njia gani, nahitaji kuanza hiyo biashara

Ingia Playstore AU AppStore inategemea watumia simu gani download Alibaba then jisajili utakutana na bidhaa nyingi tafuta kile unachohitaji kwa umakini hata zaidi ya masiku jiridhishe kwenye page zao utakutana nao au mfate inbox muombe whatsapp namba then mtaanza wasiliana na utamueleza unachohitaji toka kwenye kampuni yake, mkiafikiana bei bas mnaanza fanya bishara
 
Cha kusisitiza hapa ni kwamba mkishakubaliana whatsApp kila kitu basi rudini Alibaba mmalizie mchakato. Mwambie atume quotation kupitia Alibaba kisha michakato mengine yote ifanyike ndani ya Alibaba ili akizingua uwe na uwezo wa kuomba refund. Mkimalizana nje ya Alibaba na akakupa account namba ya bank tofauti na ile anayojulikana alibaba, hapo ukilipia ujue hautakuwa na uwezo wa kurudishiwa hela yako.
Mara nyingi hudumiwa na GOLD SUPPLIER
 
Na mimi nahitaji kuanza biashara ya nguo na urembo kama kuna uwezekano naomba uniunganishe na supplier wanaohusika na hizo bidhaa mkuu
Hello!

Nguo na urembo inabidi uende China kwenye masoko ili uweze kuchagua mwenyewe

Masoko yapo katika miji ya
1. Guangzhou - hapa unaweza kupata kila kitu unachohitaji, lakini kwa kiasi kikubwa nguo zao ni low quality
2. Yiwu -
3. Shanghai -
4. Shenzhen - Nguo, handbags na viatu vizuri. Quality zao ni nzuri pia. Urembo sina hakika
 
 
ukienda unijulishe nami nianze safari za uko
 
Biashara ya nguo ina LAWAMA mno hasa ukinunua online. Biashara hii inabebwa sana MATERIAL. Yaani supplier anaweza kukutumia picha ya nguo ukaipenda mwonekano wake, lakini ukijakuiona kwa macho utatamani uitumbukize chooni! Hata kama supplier ametoa maelezo kuwa material ni aina fulani, lakini bado kuiona "physically" ni muhimu sana. Hii pia kwa handabags! Vinginevyo unaweza kulia aisee! Kama kuna namna ya kwenda China mwenyewe basi nenda au mpe sample anaekwenda akuletee!
 
Habari, naomba namba yako kama hutojali Kuna vitu nahitaji unielekeze
 
wakuu samahanin san <br />naomba mtu au watu amabo wanauzoefu na biashara ya vifaa vya simu(phone accessories) kutoka kenya au Zanzibar kwa bei ya jumla vifaa hvyo ni km vile mics,system chargers, screen touches, glass protectors, earphones, phone covers,chargers,USB cables,carbons, speakers, motherboard,memory cards, flash, battery, nk. nahitaji kujua bei ya jumla kwa hayo maeneo mawili(kenya na zanzibar) na wapi ni nafuu zaid na maeneo ambayo ni dominant kwa kuuza hvyo vifaa kwa bei ya jumla msaada plzzz wakuu<br /> cont: +255769939879<br />whatsapp na voice call online 24/7
 
Mkuu mm nna shida na hiyo mashine ya kubana glass za juice kutoka kwako tunawasilianeje
 
Shukrani sana kwa mwazilishi wa uzi huu mkuu Kipilipili . Shukrani pia ziwafikie Software Engineer na socrate jr pamoja nawatu wote mlioshiriki toka mwanzo katika mjadala huu kwa kuchangia na wengine kuuliza maswali. Laiti watanzani wengi angekuwa na moyo huu wa kupeana taarifa kwa mambo mbalimbali basi tungewasaidia wengi.

Nashauri watu waupitie uzi huu toka mwanzo kuna mengi ya kujifunza yenye kuelimisha katika ugo wa biashara kati ya Tanzania na China.

Ngoja nijipange, kisha nitakutafuta mkuu Kipilipili ili nichukue hatua sasa kwenye eneo nililokuwa nafikiria kufanya lakini sikuwa nimepata ABC zake. Kwa maelezo yako nadhani unaweza nipa mwanga zaidi.

Kweli information is power
 
Asante sana kwa uzi huu Mkuu Kipilipili!
In Sha Allah Mungu akuzidishie wewe na wenzako mnaotupa taarifa hizi muhimu bure kabisa!
Nimependa hizi mashine nitawasiliana nawe!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…