China: Fursa za biashara, usafiri na masoko

China: Fursa za biashara, usafiri na masoko

S

Safi sana. Ili tuendelee kama Taifa lazima tupeane info za msingi kwa haraka sana. Kila la heri
Just like Mapopo do! wako sharp katika kupeana infos za maana na nyeti,
Nipo interest na mashine ndogo za kuzalisha bidhaa majumbani,kama childs shoes and so on..!
 
Hili mkuu kama una mtaji mkubwa wa kuchukua kontena basi utapata kwa bei nzuri kiwandani na faida utaiona. Ila kama utachukua pcs chache (LCL) ili uje uchuuze Tanzania, basi ushauri wangu, tafuta supplier mkubwa Tanzania, nunua kwake na chuuza.

Kipilipili
Nikupongeze Sana sana personally na Wachangiaji wengine Software Engineer na socrate jr
Huu uzi ni very usefully 99%
Very Detailed na unatoa mwanga halisi wa Field mambo yalivyo.
Hujawa na uchoyo wa Taarifa mpak Figures nikupongeze sana.
Nimeusoma kuanzia saa 9 usiku Mpaka sasa
Nimejifunza mengi sana.
Concept ya MOQ minimum order quantity nimeielewa Vizuri Sana.(wabongo huwa wanajazana sana upepo hapo).
Uzi umetoa majibu ya maswali yote yanayotakiwa.
Ubarikiwe sana Sana.
Mwenyezi Mungu akubariki sana na wengine wote waliotoa miongozo mbali mbali.
Mbarikiwe Mpaka mshangae
 
Ndugu watanzania naomba niseme hili kwa dhati kabisa
Biashara za kuvuka Border zinalipa sana
Lakini shida kubwa wengi mtaji mdogo
Utanunua Bidhaa huko nje kwa Bei rahisi sawa lakini ukija kujumlisha nauli na malazi na chakula Faida yote unaiacha njiani
Kuna jamaa alijazwa upepo mtaani China [emoji630] mzigo Bei rahisi
Akachukua visenti vyake Mpaka huko ng’ambo
Mzigo kweli alipata kule kwa Bei rahisi
Ukija kujumlisha na nauli na kulala
Mpaka anafika Tanzania [emoji1241] unakuta mzigo unasimamia Bei zaidi ya Bei ya rejareja hapo kariakoo, waweza kudata
Nashauri Mtu apate taarifa za kutosha kabla hujaanza Safari
Wafanyabiashara Wote tujifunze sana somo Linaitwa PRODUCT COSTING
Ukilijua hilo hupati Shida kwenye kununua na kuuza
Ukifeli hapo hakuna muujiza wa wewe utoe faida Dukani
Cc: Kipilipili , socrate jr
 
Ndugu watanzania naomba niseme hili kwa dhati kabisa
Biashara za kuvuka Border zinalipa sana
Lakini shida kubwa wengi mtaji mdogo
Utanunua Bidhaa huko nje kwa Bei rahisi sawa lakini ukija kujumlisha nauli na malazi na chakula Faida yote unaiacha njiani
Kuna jamaa alijazwa upepo mtaani China [emoji630] mzigo Bei rahisi
Akachukua visenti vyake Mpaka huko ng’ambo
Mzigo kweli alipata kule kwa Bei rahisi
Ukija kujumlisha na nauli na kulala
Mpaka anafika Tanzania [emoji1241] unakuta mzigo unasimamia Bei zaidi ya Bei ya rejareja hapo kariakoo, waweza kudata
Nashauri Mtu apate taarifa za kutosha kabla hujaanza Safari
Wafanyabiashara Wote tujifunze sana somo Linaitwa PRODUCT COSTING
Ukilijua hilo hupati Shida kwenye kununua na kuuza
Ukifeli hapo hakuna muujiza wa wewe utoe faida Dukani
Cc: Kipilipili , socrate jr
Unachosema kina ukweli ndani yake. Mwanzoni mwa uzi huu nilitoa kabisa angalizo, anaekuja China anatakiwa aangalie vitu vingi sana na nimevieleza.
Watu wengi mtaani wanaamini China vitu ni rahisi na akija na mtaji wake basi atanunua na akifika Tanzania atauza tu kirahisi. Mambo ya kuzingatia
1. Gharama halisi mpaka mzigo unafika Tanzania itakuwa kiasi gani? Hapa ni muhimu mnunuaji wa bidhaa ajifunze kukadiria CBM za mzigo. Mfano kama unanunua mashine China, basi mbaki na kujua gharama za kununua, basi ujue makadirio ya ufungashwaji (Packing size) na hili ni rahisi, muulize muuzaji akwambie packing size. Au kama ni mashine basi hakikisha umepata vipimo vyake yaani urefu, upana na kimo halafu kadira itakapofungashwa (mfano kwa wooden package) itakuwa kiasi gani, yaani ongeza kidogo vipimo kutoka kwenye SIZE ya mashine kwa sababu ikifungashwa kuna size kidogo inaongezeka. Halafu jua utasafirisha kama mzigo mdogo (LCL) au kama unachukua kontena zima (FCL) basi jua mashine hizo zitaingia ngapi? Kama ni mzigo mdogo ambao utawapa mashirika ya kusafirisha basi jitahidi kujua wanacharge kiasi gani kwa cbm? Halafu fanya makadirio. Hapo utapata gharama halisi. Haya mambo ya kutojua gharama kamili, yaliwahi kuwakuta watu fulani. Walikuta sofa zinauzwa bei rahisi china. Wakazibeba. Bila kujua kua sofa zinachukua CBM nyingi na wao wakasafirisha kwa wasafirishaji wa kawaida kwa vile mzigo wao haukutosha kontena zima.
Gharama za usafiri walizopigiwa baada ya mzigo kufika, ilikuwa ni bora wangenunua Tanzania tu kutoka kwa makampuni makubwa ambayo huleta bidhaa zao kama full container na hivyo bei zao kuwa za nafuu.

Watu wengi wakiangalia bei za mtandaoni china wanaona ni rahisi tu, ama wanakuja kununua au wanaagiza. Mzigo ukifika bandarini unakuta gharama ni zaidi ya bei halisi sokoni Tanzania.

2. Timing: Ni muhimu kukadiria mpaka mzigo unafika Tanzania, hali ya soko ikoje? Kuna watu wanakuja kuchukua nguo, wakitaraji watauza kabla ya sikukuu halafu mzigo unafika baada ya sikukuu .Hapo tayari kariakoo mzigo kama huo ulishafika siku nyingi, ulishauzwa na bei ya soko iko chini. Hapo ni maumivu tu na hasara tupu.

Mara zote nashauri sana watu waanzie sokoni/wateja wao kabla ya kuamua kununua kitu china. hayo ni machache tu
 
Kumekuwa na changamoto kubwa mbili kwa watu wanaogiza vitu kwenye mitandao hii nguli ya Kichina
Bei ya mali kuwa rahis lakini usafiri kuwa bei kubwa.

Wengine njia za kufanya malipo kushindwa hasa pale supplier anapo demand Wechat payment.

Unique aircargo tumekuja kuwasaidia Watanzania wenzetu. Sisi tunasafirisha mizigo kwa njia ya ndege kutoka China Guangzhou mpaka Dar es Salaam na kama uko nje ya Dar tunakutumia mzigo wako.Tunafanya dola 10.5 kwa kilo.

Ukiwa na kilo nying kama 100 na kuendelea bei
itashuka
mzigo unakufikia kabla ya 2 weeka
tupigie 0652472486


Sent from my iPhone using JamiiForums
 
Habari wana jukwaa,

Kumekuwa na ongezeko kubwa la wafanyabishara kutoka Tanzania kwenda China kufanya biashara mbalimbali kama nguo, vipuri vya magari na pikipiki, vifaa vya electronics nk. Najua kuna thread nyingi zimewahi kuzungumzia biashara za China, lakini nimuombe mkuu Invisible aifanye hii iwe sticky thread ili iwe refernce point kwa kila anaehitaji kufanya biashara China.

Nitaeleza KIDOGO Kuhusu biashara za China.

BIASHARA YA NGUO: hii inapendwa sana kufanywa na kina dada japo wanaume pia wapo. Wengi walio wageni na biashara hii wamejikuta wakipata hasara hasa wanapofika tu miji kama Guanzhou na kuanza kununua nguo bila kuangalia hali ya soko Tanzania ikoje.

Hujikuta wakinunua nguo on their perspective and not customers perspective! Kinachowavutia machoni mwao ndicho wanachonunua kwa matarajio watauza tu. Wengine wananunua na wanapofika na mzigo kariakoo wanakuta mzigo kama huo uloshaingia a week/month before hivyo kujikuta wanauza kwa bei ya hasara.

Ushauri: Jaribu kutafuta wateja kabla Tanzania , wakupe order na sample kisha ukifika China nunua kile walichokuagiza.Pia jitahidi ujue ni fashion gani bongo iko sokoni na mpaka mzigo umefika bongo,je bado hiyo fashion ulionunua itakuwa inauza? Mind you kwamba biashara ya nguo hasa za WANAWAKE zinaendeshwa kwa nguvu ya soko na fashion hubadilika mara kwa mara!Biashara ya nguo za watoto au wanaume kidogo fashion zake zinakaa muda mrefu ukilinganisha na za wanawake.

BIASHARA YA VIFAA VYA ELEKTRONIKI kama simu na accessories zake, music system n.k

Miji mizuri ya kununua mzigo kwa biashara hii ni Shenzhen na Honkong ,japo mji wa Guanzhou pia ni maarufu isipokuwa fake products kwa Guanzhou ni kubwa zaidi. Changamoto kubwa ya biashara hii ni FAKE PRODUCTS. Angalia wateja wako ni watu wa namna gani. Most low income earners ambao kwa Tanzania ndio wengi, wanapenda cheap price.

Kwahiyo, ukinunua genuine products huwezi kuuza bongo kwa sababu bei itakuwa iko juu na wao watashindwa. Kwa hiyo jua needs and wants za customers wako kabla hujaamua kununua mzigo. Kwa mtu mwenye mtaji mdogo unaweza kuanza na kununua phone acssesories na simu chache tu za bei ya chini, utakuwa unaongeza idadi ya simu kidogo kidogo kadri mtaji unavyokua. Pia kama una mtaji mkubwa unaweza kuingiza used products kama photocopier machines ila jitahidi uwe na orders kabla hujaleta kwa sababu ukija nazo nyingi bila order zinaweza kukaa muda mrefu ukajikuta unaanza kula mtaji.

Wakati unasafirisha photocopier machines jitahidi ununue vitu vidogo vidogo kama vile memory cards, USB cards, power banks nk na uviweke pamoja ndani ili ukija bongo wakati unasubiri kuuza photocopier machines unauza hivyo vitu vidogo vidogo ili kupata faida kidogo kidogo na kuhakikisha huli mtaji.

Kumbuka hapa utasafirisha kwa meli na huwa wanapima CBM na sio uzito kwa hiyo hivyo vitu vidogo vidogo cost yake ya kusafirisha itakuwa imemezwa na hizo machines.Photocopier machines nimetoa kama mfano wa moja ya bidhaa lakini vipo vimashine vingi tu ambavyo unaweza kusafirisha kama: Mashine za juice ya miwa, hizi zimekuwa na demand kubwa sana kwa sasa Tanzania. Wateja wake wapo , kama utakuwa na mtaji mzuri unaweza kununua hizi na kuleta. Nyingi ni portable na modern. Ni kiasi cha kutafuta orders na kisha kuleta.

Kuangalia bei mbalimbali za bidhaa tembelea:
Find quality Manufacturers, Suppliers, Exporters, Importers, Buyers, Wholesalers, Products and Trade Leads from our award-winning International Trade Site. Import & Export on alibaba.com

Made-in-China.com mobile- Connecting Buyers with China Manufacturers, Suppliers & Products

www.taobao.com (hii ni ya kichina, tumia browser ya google chrome na tumia kitufe cha translation ili ije kwa kingereza)

USAFIRI NA USHAURI: Zipo kampuni nyingi zinazosafirisha mizigo kwa njia ya ndege na meli. Kampuni kama GNM, THE LAND, SILENT OCEAN, CHOICE AIR CARGO, MOKHA AGENCY ni baadhi tu na hizi zina ofisi zao pale pale Guanzhou na bei zake zinatofautiana kutegemeana unasafirisha kwa njia gani yaani ndege au meli. Na unapolipia wao ndio huhusika na clearance na kila kitu, wewe ukifika bongo unachukua tu mzigo wako kwenye Ghala lao.

Pia wapo Watanzania ambao hawana kampuni lakini nao wanasafirisha mizigo hasa hasa kwa ndege. Hapa natoa angalizo, hakikisha mtu unayemtumia kusafirisha awe ANAAMINIKA na tafuta watu ambao wamewahi kuhudumiwa na yeye! Vinginevyo Utapigwa na kuingizwa mjini uje hapa kulalamika. Chukia tahadhari! Sio wote ni waaminifu na pia sio wote wakorofi.

Website ya baadhi ya makampuni ni:
Silent Ocean Limited - Specialized in International Cargo Shipping

Kampuni hizi nilizozitaja hapa zinahusika na usafiri lakini pia kama utakuwa na lolote unalotaka kujua kuhusu biashara ya China watafute na uwaulize.

Usafiri wa meli huchukua kati ya siku 25-60 kutegemeana na kampuni. Usafiri wa ndege siku 10-21 itategemea na unapotumia.

Baadhi ya mashirika makubwa ya usafiri shaji mizigo duniani kwa ndege nayo pia yapo China na yanaleta mizigo Tanzania. Sitayataja hapa kwa sababu isijekuonekana naharibu biashara zao . lakini unaponunua mzigo sishauri sana kuyatumia ikiwa utasafirisha kwa ndege kwani gharama zao ziko juu sana. Mpaka unaupata mzigo wako unakuwa hoi bin taaban! Yatakuchaji nauli, na bado yatakuchaji kodi tena ya hali ya juu mpaka upate mafua ghafla[emoji16].

Unaposafirisha kwa ndege hakikisha bidhaa yako haina battery au kimiminika mana makampuni mengi hayataki bidhaa za namna hiyo. Mfano: Usafirishaji wa simu umekuwa na changamoto sana kusafirisha kwa ndege hasa kama ni mzigo mkubwa kutokana na simu kuwa na battery. Bidhaa kama simu hakikisha unatuma kwa meli ili kuepuka usumbufu.

Unaponunua mzigo kwa supplier hakikisha sana anakutumia picha ya mzigo ulivyo kabla hajautuma kwa wasafirishaji. Pia mwambie nje aandike mzigo wako kwa maker pen au abandike karatasi na aweke jina lako, namba yako ya simu, ataje ndani ni bidhaa gani, na aandike pia idadi .Mfano:
Miss Kipilipili
Mobile:+2557XXXXXXX
Product name: Kipilipili Coconut Oil
(Kama ni mashine aandike MODEL number)
100pcs.
Kisha abandike maelezo hayo juu ya package yako. Hii itasaidia sana wakati wa clearance na pia ikitokea mzigo umepotea au umekuwa misplaced ni rahisi kufanya tracking.

KUFUNGA MZIGO: Kama umeenda China mwenyewe, hakikisha unakuwepo wakati wa kufunga mzigo. Usichague bidhaa, kisha wakakwambia njoo kesho tutakuwa tumeshaufunga au tutakuwa tumeshapeleka kwa shipping agent wako! Hakikisha umeona nini kipo ndani kabla hawajafunga. Na kama mzigo wamepeleka kwa agent wako basi mwambie agent aukague wakati wa kuupokea na hakikisha supplier wako anajua kuwa mzigo ukifika kwa agent utakaguliwa. hii itasaidia usipigwe! Wapo Suppliers sio waaminifu


NAULI: Nauli zinategemea season na pia unataka kusafiri lini. Kipindi cha high season kama, July, August bei zinakuwa juu. Kama kwa mfano unatarajia kusafiri July basi ikifika april kata tiketi mapema . Mara nyingi kunakuwa na offer kwenye mashirika ya ndege kwa hiyo pendelea kutembelea website zao.

Pia nauli inategemea na shirika la ndege unalotaka kusafiria na pia daraja unalotaka kukaa.

Kwa wafanyabiashara wengi hutumia ethiopian airline kwa sababu huwa wanatoa kg nyingi kuliko wengine.

Pita kwa mawakala posta na kariakoo au search google kupata bei mbalimbali za nauli. Unaweza kutenga bajeti ya USD 900-1200 Kwa nauli kwa economy class
Angalia bei za NAULI hapa:
International Flights, Airfares, Tickets - Fly Ethiopian
Qatar Airways
KLM Royal Dutch Airlines – Flights | Vliegtickets | Flüge

MALAZI: Hapa nitazungumzia mji wa Guanzhou ambao ndio wenye wafanyabiashara wengi wa mataifa mbalimbali hasa Afrika. Zipo hoteli za hadhi tofauti, bei kutoka 120 yuan(36,000 Tsh) ikiwa ni bei ya chini labisa na kuendelea kutegemeana na mfuko wako. Maeneo kama "shaobei lu" ni maarufu kwa watu weusi na utakisikia kiswahili kila baada ya hatua kadhaa. Hoteli za pembeni ya mji bei huweza kuwa chini mpaka yuan 100.

Angalia range ya bei za hoteli hapa: GuangZhou hotels: cheap rates in GuangZhou by China Hotels Reservation


CHAKULA: Zipo hoteli nyingi Guanzhou na shenzen zinazomilikiwa na foreigners na wanauza chakula kizuri japo kiko ghali kidogo, ila kama unahitaji chakula cha bei ya chini na ambacho ni HALAL (wengi huhofia kulishwa mbwa,kitimoto,nk) unaweza kula kwenye sehemu nyingi ambazo huuza wachina waislamu wenye asili ya Xinjiang ambao huuza HALAL food kwa bei poa kuanzia Yuan 15(4500 Tsh) na kuendelea kutegemea na aina ya chakula ulichoagiza. Kuwa makini na vyakula mana wale wenzetu huwa wanakula vyakula vingi vya "ajabu ajabu".

LUGHA: Wachina hutumia lugha yao kwa kila kitu. Katika miji ya biashara kama Guangzhou wachina wafanyabiashara huongea kingereza cha mawasiliano(kibovu) ila mnawasiliana na kuelewana. Pia lugha ya ishara inatumika pale panapokuwa na language barrier.

Hata kama hujui kabisa kingereza unaweza kuchagua bidhaa na kisha mkapatana bei. Wenzetu wana utaratibu wa kutumia calculator kukuandikia bei, hivyo na wewe utaandika ya kwako mpaka mtafikia makubaliano. Nashauri download application yoyote ya TRANSLATION kama pleco nk ili ikusaidie kwenye mawasiliano unapokwama andika neno unslohitaji kwa kingereza kisha tafsiri kwa kichina na muoneshe mchina hilo neno, itasaidia kurahisisha mawasiliano

Nimegusa juu juu vitu vichache mno kuchokoza mada ili wengine waongezee uzoefu na iwe msaada kwa kila anaetaka kufanya biashara China.

Karibuni tujadili na kusaidia wengine

NB: Kuanzia sasa USIHANGAIKE kutuma ujumbe PM SITAJIBU KABISA, wala SITOI NAMBA YA SIMU. Kila kitu ULIZA HAPA. Wenye majibu watajibu, si lazima mimi
ok
 
Duh nimetembelea websites ulizozitaja kweli bei rahisi ndo nafikiria kuhusu hizo gharama za usafiri NAFANYAJE natamani kuagiza Kipilipili
 
nakutumia namba PM ya mtu wa dukani DSM
Unaposema mambo yote mfanyie kwenye alibaba hii ina maana gani? Mfano mm nimempata supplier kupitia alibaba na baada ya kuchat pale tukatumia whatsap kwa mawasiliano rahic ,je hii inaweza kuwa mawasiliano nje ya Alibaba?
 
waone unique aircacrgo namba zao za simu ni 0652472486 hawa ni mabigwa wa usafir wa anga kwa sas ofis zao zipo kariakoo mtaa wa pemba na livingstone na china wapo pale lujing road xiaboi siku 13 ushapaata mzigo wako kwa bei ndogo sana
Mkuu unawajua vizuri hawa?
 
Wasalam wakuu,naomba kujuzwa,je, ukiwa million I kumi na tank(Tsh.15,000,000)inatosha kufuata mzigo (nguo za watoto wachanga) Guangzhou?hapo ni nje na nauli! Natanguliza shukrani.
 
Nadhani hujanielewa. Hizo bidhaa ulizotaja ZIPO KWA WINGI kwa hiyo demand si kubwa kama NYAMA YA NG'OMBE
Vigezo vipi unatakiwa uvikamilishe ile uweze kupata vibali vya kuuza nyama ya ng'ombe
 
Back
Top Bottom