China: Fursa za biashara, usafiri na masoko


Safi sana, umelenga kama wazo langu, tumuombe #kipilipili kwa uzoefu wake kama anaweza kupata bei ya hizo mashine ulizoorozesha hapo atusaidie, tanzania tunaweza tukianua wenyewe
 
Asante mkuu, vizuri umeorodhosha vitu ambavyo ulikisudia. Ngoja niwaachie wengine watupe uzoefu katika vifaa hivyo

Mkuu hali ya usalama ikoje? Na hawa ndugu zetu Wabongo wanaoabudu utapeli na kuingizana mkenge wameshaweka maskani huko?

Na homeshopping center nina taarifa wao ndio mawakala wakubwa wa kusafirisha mizigo wa wabongo je hawana ubabaishaji?

Kwa biashara ya nguo unashauri mtu aanze na mtaji kiasi gani? Kwq uzoefu wako kuishi China wiki mbili hotel na chakula inaweza kukugharimu kiasi gani?

Na vipi kuhusu polisi wa China ni waadirifu? Nchi nilizowahi kwenda mimi hakuna kitu kubambikiwa kesi na polisi labda kwenye mambo ya siasa tu.
 
Nataka kuagiza kitimoto na Kuku kutoka China.
 

Mkuu,
hali ya usalama kwa ujumla ni nzuri sana, na jamaa wako vizuri katika system. Cha msingi fuata sheria na fuata kilichokupeleka.ukilikoroga utalinywa tena bila zengwe hawana utani .Sijawahi kushuhudia ubambikaji wa kesi!

kuhusu wabongo na utapeli:mkuu kutapeliwa kupo mahala popote, cha msingi ni kuepuka tamaa na jitahidi kuwa makini na kila unachofanya! Usimuamini mtu hasa unapokutana na country mates zako au watu kutoka ukanda mmoja wa east africa. Usimlete mtu chumbani ulikofikia. Mnajuana barabarani na mnaachana huko huko. Kama ni kukutana basi kutaneni sehemu ya chakula kama vile hoteli nk. Wapo wabongo ambao unawalipa kiasi cha pesa na wanakuzungusha masokoni ila ni muhimu uwe umeunganishwa na mtu unae muamini na iwe ni kwa ajili ya escort tu. Asikupige longolongo nyingine, atakuliza!

kuhusu home shopping center binafsi sijawahi kufanya nao kazi, kwa hiyo naomba nisizungumze lolote kuhusu wao ila nakiri kuwa wapo wanaosafirisha kupitia hao jamaa.kama wapo humu watusaidie taarifa tafadhali.

Kuhusu mtaji wa biashara ya nguo;mara nyingi nimekuwa mgumu kusema mtaji mtu aanze na kiasi gani kwa sababu tunatofautiana scale na vision ya biashara zetu. Hivyo hata mtaji unaweza kuwa tofauti unless mtu awe specific katika aina ya nguo anazotaka kuchukua na matarajio yake ya mauzo then unaweza ukakadiria mtaji wake. Ila kukadiria from "unknown ground " huwa inakuwa ngumu mana unaweza ukataja less au zaidi ya pesa halisi

Kuhusu chakula na kukaa hoteli kwa wiki mbili. Nimeeleza tayari estimation za malazi na chakula hapo juu. Kwa hiyo unaweza kurejea na kufanya makadirio kwa idadi ya siku hizo.
 
Nataka kuagiza kitimoto na Kuku kutoka china

Hahaa mkuu rejea nadharia ya demand and supply. Ukiagiza hizo bidhaa na kuingiza nchini UTAPATA HASARA(I promise you). Nakushauri, achana na hilo wazo kwa sababu supply ya hizo bidhaa hapa kwetu ni kubwa pengine kuliko hata demand yake.
 

Naomba namba yako kama hutojali bro #kipilipili nmekuwa interested sana na uelewa wako juu ya ujasiliamali wa watu wenye mitaji midogo
 
uzi safi sana.. leo tu nimetuma usd zangu 3000 pale silent ocean...

huduma nimepata safi.. mdada mrembo recho na totoz za kiarabu zinapiga kazi safiiiiii...

kiukweli dunia sasa kama kijiji... kila unachotaka kinapatikana mikononi.mwako
 
uzi safi sana.. leo tu nimetuma usd zangu 3000 pale silent ocean...

huduma nimepata safi.. mdada mrembo recho na totoz za kiarabu zinapiga kazi safiiiiii...

kiukweli dunia sasa kama kijiji... kila unachotaka kinapatikana mikononi.mwako

Hahaa....mkuu naona umeweka na msisitizo hapo kwenye "TOTOZ", chonde chonde usije ukala mtaji(joking). By the way, karibu and share with us your valuable experience! Karibu sana!
 

Naomba namba yako mkuu tafadhali
 
Kipilipili asante kwa kutufungua macho!!..

Nina mpango wa kuwa na kiwanda cha kidogo -mpaka cha kati. Sasa kuna mashine (food processing) kutoka China maana najua huko ndipo nitapata kwa gharama nafuu.. Please naomba contacts zako ili unipe ushauri zaidi..!!
 
[Kipilipili]



  • Kipilipili asante kwa kutufungua macho!!..

    Nina mpango wa kuwa na kiwanda cha kidogo -mpaka cha kati. Sasa kuna mashine (food processing) kutoka China maana najua huko ndipo nitapata kwa gharama nafuu.. Please naomba contacts zako ili unipe ushauri zaidi..!!​



 
mi labda nichangie kuhusu biashara ya simu ambayo ndo naifanya,mi nilikua nachukulia simu pale guangzhou original ila nyingi zilikua na problem nikabadilisha maskani sasa iv nachukulia hongkong.

kwanza HONGKONG vitu kama simu ni original alafu kama used unapata nzima na zenye quality nzuri sana ila tatizo ni gharama kubwa za kuishi hongkong..

Smartphone ambayo nachukua kule kwa 400 HKD sawa na kama 120000 hivi huku naweza kuuza si chini ya 250000 kwa simu mmoja na huku nakua na ma dealer wangu ambao nawauzia wao pia wanauza...

ubaya wa hii biashara ilikua usafiri wa shida sababu niktuma kwa ndege kama parcel hapo airport wanataka pesa nyingi kwaiyo tulikua tunawapa hawa wabongo wanaokuja huku nampa simu mbili au tatu alafu naampooza na 20000 hivi anachukua kwaiyo akifika huku kuna mtu anazipokea na pale airport hasumbuliwi sababu wanajua ni za kwake tu.
 

Ahsante sana mkuu.
Ni kweli living cost za HK ziko juu mno kuanzia makazi hadi malazi.

Suala la usafiri linaumiza sana kichwa hasa ukizingatia jamaa wa pale "Njia panda ya ulaya"walivyo na "njaa". Pale hata uwe na laptop moja sometimes wanakukomalia hasa wakiiona ina upya kidogo...yani ni shida.

Kutokana na changamoto ya usafiri niliamua kushift na kununua bidhaa ambazo hata nikizitia kwenye meli mwezi zinakuwa bado ziko kwenye soko ,sio kama nguo ambazo ikipita mwezi ujue kariakoo waeza ukaziuza kama mtumba.
 

Umetisha sister.

Bado upo gz au bongo?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…