Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Mkuu jaribu kucheck Guangzhou na Shenzenbiashara ya auto spare parts used ni mji gan huko china
pole mkuu, nimekujibu tayariKipilipili uko safarini? Mbona hunijibu?
pole mkuu, nimekujibu tayari
Mkuu hujanipa namba
Asante sana na ubarikiwe......Hizi ndio mada za kuleta hapa kwa nchi kama yetu mapenz tuwaachie wazungu sisi tutauwana bure
Ahsante kwa maelezo ya moyo mkuu na kujitoa, unajua sio kuwa hapa JF hakuna wengine wanaojua hivi vitu ila ndio ile "ajue na yeye aende atusue"
Ahsante kwa Moyo wako huu, mimi nna maswali kadhaa huwa yananipa wasiwasi, toa ushauri kwangu na wenye wasiwasi huu
1.Ukipitisha kwenye Meli ushuru inakuwaje kwa hawa TRA na hakuna kuumizana kwenye kodi? Hasa ukiwa mgeni
Nnapotoka hapa nakwenda guanzhoo, au Hong Kong au mji mwingine, nitashukia wapi au ticket yangu nnapokata ndipo nitashushiwa? Au unashukia mji mmoja unautafuta mwingine uutakao kwa basi, tren au vinginevyo, Maana tumezoea hapa kwetu bongo utashuka dar tu kwingine ukomae na basi. Tupe idea
3. Ushauri wako ni upi ni vema mtu mwanzoni akaenda na mwenyeji au hata mwenyewe waeza kwenda ukafanikiwa.
Mwisho mtu akiomba msaada uende nae, Upo tayari
Ahsante kwa kuchukua muda wako kunijibu
1. Ushuru TRA
mkuu ushuru UPO mkuu, na kama unapitisha kwa meli basi nashauri tafuta clearing agent akusaidie kuclere mapema ili mzigi ukifika tu utoke mapema iwezekanavyo. Kumbuka kadri unavyokaa muda mrefu bandarini baada ya kufika ndio gharama zinaongezeka. Ukikosa agents ,nijulishe ntakuunganisha kwa kampuni mbili ninazozifahamu.
Au njia nyingine, wape makampuni kule kule china na yalipe hela ya usafiri, wao watahusika na kila kitu ikiwemo clearing. Wewe utafuata tu mzigo kwenye ghala zao.
Gharama za kodi kiasi gani TRA zinategemea unaingiza bidhaa gani na ipo kwenye hali gani, yaani mpya au mtumba. Kumbuka kama ni mtumba kuna dumping fee itakulazimu kulipa.
2.Kuhusu pa kushukia, mara nyingi kama unatoka bongo kwenda Hongkong zipo ndege za moja kwa moja. Mfano, kama utatmia ethiopian airline, utatoka hapa bongo hadi ethiopia pale Bole int. Airport, kisha hapo utabadilisha ndege utapewa ndege nyingine hadi Hongkong, hivyo hivyo kama unataka kwenda guanzhou au beijing.
Ila kuna miji mengine itabidi ukate nauli ya kutoka bongo hadi guanzhou, kisha local flight/train kwenda mji mwengine. Kwa local flight unakatia huku huku bongo yaani mfano unataka kwenda mji wa WUHAN china, then utakata tiket ya moja kwa moja hadi Wuhan ila utapita ethiopia utabadili ndege, utaenda hadi guanzhou utabadili tena ndege itakayokupeleka hadi wuhan.
Ama kuna miji iko karibu ambayo unaweza kwenda kwa train mf. Shenzen. Ukifika guanzhou utapanda tu train hadi zhenzhen.
3. (A)Kuhusu kwenda na mtu.
Hili lina faida na hasira zake. Faida ni kwamba utakuwa umepata mentor na atakushika mkono katika mambo mengi. Japokuwa uzoefu unaonesha wengi wanapokuwa na mtu kama hivi huwa hawawi makini kujishughulisha kwa sababu hana wasiwasi wa kupotea na kila sehemu anapelekwa tofauti na yule ambae amekwenda mwenyewe ambaye anajishughulisha kujua maeneo nk. Huyu alienda na mtu mara nyingi siku akiachwa peke yake anakuwa wakati mwingine ni kama vile hajawahi kwenda mana kila kitu hajui kwa vile wakati ule kila kitu alikuwa anafanyiwa. Kingine, kwenda na mtu ni gharama, kwa sababu inabidi umugharamie kila kitu.
Otherwise jaribu kutafuta mtu ambae na yeye ni mfanyabiashara, yaani akipanga safari yake na wewe upange same date ili upate kampani na sio kwamba utamlipia kila kitu.
(B) ukinigharamia KILA KITU, nipo tayari kukupeleka
Nahisi nimejibu pia hilo mkuu.Ahsante kwa maelezo kwa faida ya wengine na mimi pia naomba uchukue muda wako kujibu na swali no 3
Nahisi nimejibu pia hilo mkuu.
Thanks nimeona nazani sikuwa nimefika chini. Nimependa jibu namba 3 😀 anyway thanks
hahahahah..haya mkuu.
Ahsante Mkuu kwa msaada Wako usio na tamaa, choyo na ghilba.
Naomba nikuulize, mimi nahitaji used construction equipments je Una taarifa kamili?
mkuu, bahati mbaya sina uzoefu wa bidhaa hizo na pia sina taarifa zake kamili, nashauri "search" katika moja ya websites nilizoweka hapo juu utapata taarifa za kutosha
Mkuu ahsante sana nimepata clue.