Huwezi kutoa hizo details mpaka nijibu hayo maswali? Mbona mtoa mada ametupa details bila kuuliza tunataka kununua nini China. Naomba details za kuexport kama mtoa mada alivyotoa details za kuimport . Ndo mana dola inashuka kwa sababu za kukatishana tamaa; tusaidiane mawazo ya kuexport bidhaa zetu ili nasi tuone jinsi gani dola tutaipandisha. Mleta mada ametoa mfano wa bidhaa ambazo tunaweza kuwauzia waChina. Mimi nina shida ya details za kuexport kama mleta mada alivyotuelimisha kuhusu kuimport bidhaa za China. Anatefahamu tafadhali tuelimishe; hakuna kisichowezekana ukiweka nia.
Mimi ni mmoja ya watu wanatoa info za china hapa JF. Sijawahi bana information kama hizo.
Nimekuuliza kwa sababu majibu yako yangerahisisha upatikanaji wa specific procedures za task unayotaka kufanya.
Anyway, ili uweze ku export zingatia yafuatayo
1. Chagua bidhaa unayotaka ku export
2. Cheki soko kupitia mitandao au wadau walioko china wakusaidie kutafuta mteja wa china
3. Utapokea viwango vya bidhaa toka kwa mteja
4. Utampa sample za bidhaa zako
5. Mteja atatupa offer ya bei yake, na wewe utatoa bei yako kama yake haina maslahi, mara nyingi wanataka CIF
4. Mtakubaliana port ya kushusha huo mzigo, mara nyingi mzigo unashushwa Guangzhou, Ningbo au Qingdao port
5. Mteja atakupa terms na kiwango cha mzigo anachotaka kila mwezi, so inabidi ujipime kama unaweza supply kiwango hicho
6. Mtakubaliana na mteja terms za malipo. Alipeje? kiasi cha mwazo ni asilimia ngapi? When alipe? Kiasi cha mwisho alipeje.
7. Itabidi utafute watu wa quality assurance walioko china au hongkong wakupe details za viwango vya nchi yao. Hii huduma lazima ulipie. Watakuelekeza a to z, cha muhimu uwe mkweli. Ukidanganya itakula kwako mzigo ukifika unaweza kuwa blocked bandarini.
Mambo ya msingi
1. Wachina ni wagumu sana ktk kulipa hela, hivyo basi hakikisha mzigo unapokuwa loaded kuondoka tz wawe wameshalipa asilimia fulani ya mzigo. Mara nyingi wanazingua mzigo wako ukishafika bandarini au warehouse wanazungusha kukamilisha malipo. Zipo kesi zishatokea na hadi mahakamani wameenda. Kibaya zaidi communication ni issue.Chinese Chinese everywhere
2. Export kitu chenye quality nzuri. Fuata makubaliano. Usiforge vitu kibongo kibongo. Akisema nyama iwe grade A basi hakikisha inakuwa grade A not B. Hii itaepusha usumbufu bandarini.
3. Katika hatua zoooote, hatua ya kutoa mzigo bandarini china ndiyo nzito. Hata hivyo vishoka wapo. Cha muhimu kujipanga tuu. Lakini quality ya mzigo ikiwa mbovu vishoka ni useless.
Nadhani inatosha kwa leo.