China: Fursa za biashara, usafiri na masoko

China: Fursa za biashara, usafiri na masoko

Kipilipili

JF-Expert Member
Joined
May 25, 2010
Posts
2,272
Reaction score
1,897
Habari wana jukwaa,

Kumekuwa na ongezeko kubwa la wafanyabishara kutoka Tanzania kwenda China kufanya biashara mbalimbali kama nguo, vipuri vya magari na pikipiki, vifaa vya electronics nk. Najua kuna thread nyingi zimewahi kuzungumzia biashara za China, lakini nimuombe mkuu Invisible aifanye hii iwe sticky thread ili iwe refernce point kwa kila anaehitaji kufanya biashara China.

Nitaeleza KIDOGO Kuhusu biashara za China.

BIASHARA YA NGUO:
hii inapendwa sana kufanywa na kina dada japo wanaume pia wapo. Wengi walio wageni na biashara hii wamejikuta wakipata hasara hasa wanapofika tu miji kama Guanzhou na kuanza kununua nguo bila kuangalia hali ya soko Tanzania ikoje.

Hujikuta wakinunua nguo on their perspective and not customers perspective! Kinachowavutia machoni mwao ndicho wanachonunua kwa matarajio watauza tu. Wengine wananunua na wanapofika na mzigo kariakoo wanakuta mzigo kama huo uloshaingia a week/month before hivyo kujikuta wanauza kwa bei ya hasara.

Ushauri: Jaribu kutafuta wateja kabla Tanzania , wakupe order na sample kisha ukifika China nunua kile walichokuagiza.Pia jitahidi ujue ni fashion gani bongo iko sokoni na mpaka mzigo umefika bongo,je bado hiyo fashion ulionunua itakuwa inauza? Mind you kwamba biashara ya nguo hasa za WANAWAKE zinaendeshwa kwa nguvu ya soko na fashion hubadilika mara kwa mara!Biashara ya nguo za watoto au wanaume kidogo fashion zake zinakaa muda mrefu ukilinganisha na za wanawake.

BIASHARA YA VIFAA VYA ELEKTRONIKI
kama simu na accessories zake, music system n.k

Miji mizuri ya kununua mzigo kwa biashara hii ni Shenzhen na Honkong ,japo mji wa Guanzhou pia ni maarufu isipokuwa fake products kwa Guanzhou ni kubwa zaidi. Changamoto kubwa ya biashara hii ni FAKE PRODUCTS. Angalia wateja wako ni watu wa namna gani. Most low income earners ambao kwa Tanzania ndio wengi, wanapenda cheap price.

Kwahiyo, ukinunua genuine products huwezi kuuza bongo kwa sababu bei itakuwa iko juu na wao watashindwa. Kwa hiyo jua needs and wants za customers wako kabla hujaamua kununua mzigo. Kwa mtu mwenye mtaji mdogo unaweza kuanza na kununua phone acssesories na simu chache tu za bei ya chini, utakuwa unaongeza idadi ya simu kidogo kidogo kadri mtaji unavyokua. Pia kama una mtaji mkubwa unaweza kuingiza used products kama photocopier machines ila jitahidi uwe na orders kabla hujaleta kwa sababu ukija nazo nyingi bila order zinaweza kukaa muda mrefu ukajikuta unaanza kula mtaji.

Wakati unasafirisha photocopier machines jitahidi ununue vitu vidogo vidogo kama vile memory cards, USB cards, power banks nk na uviweke pamoja ndani ili ukija bongo wakati unasubiri kuuza photocopier machines unauza hivyo vitu vidogo vidogo ili kupata faida kidogo kidogo na kuhakikisha huli mtaji.

Kumbuka hapa utasafirisha kwa meli na huwa wanapima CBM na sio uzito kwa hiyo hivyo vitu vidogo vidogo cost yake ya kusafirisha itakuwa imemezwa na hizo machines.Photocopier machines nimetoa kama mfano wa moja ya bidhaa lakini vipo vimashine vingi tu ambavyo unaweza kusafirisha kama: Mashine za juice ya miwa, hizi zimekuwa na demand kubwa sana kwa sasa Tanzania. Wateja wake wapo , kama utakuwa na mtaji mzuri unaweza kununua hizi na kuleta. Nyingi ni portable na modern. Ni kiasi cha kutafuta orders na kisha kuleta.

Kuangalia bei mbalimbali za bidhaa tembelea:
Find quality Manufacturers, Suppliers, Exporters, Importers, Buyers, Wholesalers, Products and Trade Leads from our award-winning International Trade Site. Import & Export on alibaba.com

Made-in-China.com mobile- Connecting Buyers with China Manufacturers, Suppliers & Products

www.taobao.com (hii ni ya kichina, tumia browser ya google chrome na tumia kitufe cha translation ili ije kwa kingereza)

USAFIRI NA USHAURI:
Zipo kampuni nyingi zinazosafirisha mizigo kwa njia ya ndege na meli. Kampuni kama GNM, THE LAND, SILENT OCEAN, CHOICE AIR CARGO, MOKHA AGENCY ni baadhi tu na hizi zina ofisi zao pale pale Guanzhou na bei zake zinatofautiana kutegemeana unasafirisha kwa njia gani yaani ndege au meli. Na unapolipia wao ndio huhusika na clearance na kila kitu, wewe ukifika bongo unachukua tu mzigo wako kwenye Ghala lao.

Pia wapo Watanzania ambao hawana kampuni lakini nao wanasafirisha mizigo hasa hasa kwa ndege. Hapa natoa angalizo, hakikisha mtu unayemtumia kusafirisha awe ANAAMINIKA na tafuta watu ambao wamewahi kuhudumiwa na yeye! Vinginevyo Utapigwa na kuingizwa mjini uje hapa kulalamika. Chukia tahadhari! Sio wote ni waaminifu na pia sio wote wakorofi.

Website ya baadhi ya makampuni ni:
Silent Ocean Limited - Specialized in International Cargo Shipping

Kampuni hizi nilizozitaja hapa zinahusika na usafiri lakini pia kama utakuwa na lolote unalotaka kujua kuhusu biashara ya China watafute na uwaulize.

Usafiri wa meli huchukua kati ya siku 25-60 kutegemeana na kampuni. Usafiri wa ndege siku 10-21 itategemea na unapotumia.

Baadhi ya mashirika makubwa ya usafiri shaji mizigo duniani kwa ndege nayo pia yapo China na yanaleta mizigo Tanzania. Sitayataja hapa kwa sababu isijekuonekana naharibu biashara zao . lakini unaponunua mzigo sishauri sana kuyatumia ikiwa utasafirisha kwa ndege kwani gharama zao ziko juu sana. Mpaka unaupata mzigo wako unakuwa hoi bin taaban! Yatakuchaji nauli, na bado yatakuchaji kodi tena ya hali ya juu mpaka upate mafua ghafla[emoji16].

Unaposafirisha kwa ndege hakikisha bidhaa yako haina battery au kimiminika mana makampuni mengi hayataki bidhaa za namna hiyo. Mfano: Usafirishaji wa simu umekuwa na changamoto sana kusafirisha kwa ndege hasa kama ni mzigo mkubwa kutokana na simu kuwa na battery. Bidhaa kama simu hakikisha unatuma kwa meli ili kuepuka usumbufu.

Unaponunua mzigo kwa supplier hakikisha sana anakutumia picha ya mzigo ulivyo kabla hajautuma kwa wasafirishaji. Pia mwambie nje aandike mzigo wako kwa maker pen au abandike karatasi na aweke jina lako, namba yako ya simu, ataje ndani ni bidhaa gani, na aandike pia idadi .Mfano:
Miss Kipilipili
Mobile:+2557XXXXXXX
Product name: Kipilipili Coconut Oil
(Kama ni mashine aandike MODEL number)
100pcs.
Kisha abandike maelezo hayo juu ya package yako. Hii itasaidia sana wakati wa clearance na pia ikitokea mzigo umepotea au umekuwa misplaced ni rahisi kufanya tracking.

KUFUNGA MZIGO: Kama umeenda China mwenyewe, hakikisha unakuwepo wakati wa kufunga mzigo. Usichague bidhaa, kisha wakakwambia njoo kesho tutakuwa tumeshaufunga au tutakuwa tumeshapeleka kwa shipping agent wako! Hakikisha umeona nini kipo ndani kabla hawajafunga. Na kama mzigo wamepeleka kwa agent wako basi mwambie agent aukague wakati wa kuupokea na hakikisha supplier wako anajua kuwa mzigo ukifika kwa agent utakaguliwa. hii itasaidia usipigwe! Wapo Suppliers sio waaminifu


NAULI: Nauli zinategemea season na pia unataka kusafiri lini. Kipindi cha high season kama, July, August bei zinakuwa juu. Kama kwa mfano unatarajia kusafiri July basi ikifika april kata tiketi mapema . Mara nyingi kunakuwa na offer kwenye mashirika ya ndege kwa hiyo pendelea kutembelea website zao.

Pia nauli inategemea na shirika la ndege unalotaka kusafiria na pia daraja unalotaka kukaa.

Kwa wafanyabiashara wengi hutumia ethiopian airline kwa sababu huwa wanatoa kg nyingi kuliko wengine.

Pita kwa mawakala posta na kariakoo au search google kupata bei mbalimbali za nauli. Unaweza kutenga bajeti ya USD 900-1200 Kwa nauli kwa economy class
Angalia bei za NAULI hapa:
International Flights, Airfares, Tickets - Fly Ethiopian
Qatar Airways
KLM Royal Dutch Airlines – Flights | Vliegtickets | Flüge

MALAZI: Hapa nitazungumzia mji wa Guanzhou ambao ndio wenye wafanyabiashara wengi wa mataifa mbalimbali hasa Afrika. Zipo hoteli za hadhi tofauti, bei kutoka 120 yuan(36,000 Tsh) ikiwa ni bei ya chini labisa na kuendelea kutegemeana na mfuko wako. Maeneo kama "shaobei lu" ni maarufu kwa watu weusi na utakisikia kiswahili kila baada ya hatua kadhaa. Hoteli za pembeni ya mji bei huweza kuwa chini mpaka yuan 100.

Angalia range ya bei za hoteli hapa: GuangZhou hotels: cheap rates in GuangZhou by China Hotels Reservation


CHAKULA: Zipo hoteli nyingi Guanzhou na shenzen zinazomilikiwa na foreigners na wanauza chakula kizuri japo kiko ghali kidogo, ila kama unahitaji chakula cha bei ya chini na ambacho ni HALAL (wengi huhofia kulishwa mbwa,kitimoto,nk) unaweza kula kwenye sehemu nyingi ambazo huuza wachina waislamu wenye asili ya Xinjiang ambao huuza HALAL food kwa bei poa kuanzia Yuan 15(4500 Tsh) na kuendelea kutegemea na aina ya chakula ulichoagiza. Kuwa makini na vyakula mana wale wenzetu huwa wanakula vyakula vingi vya "ajabu ajabu".

LUGHA: Wachina hutumia lugha yao kwa kila kitu. Katika miji ya biashara kama Guangzhou wachina wafanyabiashara huongea kingereza cha mawasiliano(kibovu) ila mnawasiliana na kuelewana. Pia lugha ya ishara inatumika pale panapokuwa na language barrier.

Hata kama hujui kabisa kingereza unaweza kuchagua bidhaa na kisha mkapatana bei. Wenzetu wana utaratibu wa kutumia calculator kukuandikia bei, hivyo na wewe utaandika ya kwako mpaka mtafikia makubaliano. Nashauri download application yoyote ya TRANSLATION kama pleco nk ili ikusaidie kwenye mawasiliano unapokwama andika neno unslohitaji kwa kingereza kisha tafsiri kwa kichina na muoneshe mchina hilo neno, itasaidia kurahisisha mawasiliano

TAHADHARI:
1. Hata siku moja usimwamini supplier wa kichina hata kama umeshawahi kufanya naye biashara. Unapotaka kumlipa, mlipe kwenye njia salama za malipo kama vile NDANI ya Alibaba, Taobao au 168.com ili kama kukitokea shida yoyote uwe na uwezo wa kuomba kurejeshewa hela yako au kufungua kesi.
Katika kipindi hiki cha Covid-19 ambapo China imefunga mipaka, watu wengi wamelizwa hasa kwa kufanya malipo NJE ya Alibaba au Apps nyingine salama za malipo. Usikubali mchina akakupa account umlipe nje ya hizi platforms
2. Wachina huwa hawafanyi kazi mahali pamoja kwa mda mrefu sana kama sisi. Kama uliwahi kudeal na mchina akiwa kampuni fulani, basi jiridhishe kama bado yupo kampuni hiyo. Wengi wamelizwa kwa kuwalipa wachina nje ya utaratibu huku wachina hao wakiwa sio wafanyakazi tena wa kampuni husika. Kuwa makini, utapigwa!
3. Kabla ya kumlipa mchina jiridhishe kama eneo alipo haliko lockdown maana ukilipa tu na kama kiwanda kiko lock down na kama ulimlipa nje ya utaratibu uliotakiwa basi juwa wazi kuwa hela yako haitarudishwa na atakwambia usubirie hadi watakapotoka lockdown. Hapo utasubiri saana na muda ukienda sana mchina anaweza kupotea na usijuwe cha kufanya. Kama ulimlipa kwenye safe platforms basi unaweza kuomba refund na hela ikarudi.

Nimegusa juu juu vitu vichache mno kuchokoza mada ili wengine waongezee uzoefu na iwe msaada kwa kila anaetaka kufanya biashara China.

Karibuni tujadili na kusaidia wengine

NB: Kuanzia sasa USIHANGAIKE kutuma ujumbe PM SITAJIBU KABISA, wala SITOI NAMBA YA SIMU. Kila kitu ULIZA HAPA. Wenye majibu watajibu, si lazima mimi

Mimi ni mmoja ya watu wanatoa info za china hapa JF. Sijawahi bana information kama hizo.

Nimekuuliza kwa sababu majibu yako yangerahisisha upatikanaji wa specific procedures za task unayotaka kufanya.

Anyway, ili uweze ku export zingatia yafuatayo
1. Chagua bidhaa unayotaka ku export
2. Cheki soko kupitia mitandao au wadau walioko china wakusaidie kutafuta mteja wa china
3. Utapokea viwango vya bidhaa toka kwa mteja
4. Utampa sample za bidhaa zako
5. Mteja atatupa offer ya bei yake, na wewe utatoa bei yako kama yake haina maslahi, mara nyingi wanataka CIF
4. Mtakubaliana port ya kushusha huo mzigo, mara nyingi mzigo unashushwa Guangzhou, Ningbo au Qingdao port
5. Mteja atakupa terms na kiwango cha mzigo anachotaka kila mwezi, so inabidi ujipime kama unaweza supply kiwango hicho
6. Mtakubaliana na mteja terms za malipo. Alipeje? kiasi cha mwazo ni asilimia ngapi? When alipe? Kiasi cha mwisho alipeje.
7. Itabidi utafute watu wa quality assurance walioko china au hongkong wakupe details za viwango vya nchi yao. Hii huduma lazima ulipie. Watakuelekeza a to z, cha muhimu uwe mkweli. Ukidanganya itakula kwako mzigo ukifika unaweza kuwa blocked bandarini.

Mambo ya msingi
1. Wachina ni wagumu sana ktk kulipa hela, hivyo basi hakikisha mzigo unapokuwa loaded kuondoka tz wawe wameshalipa asilimia fulani ya mzigo. Mara nyingi wanazingua mzigo wako ukishafika bandarini au warehouse wanazungusha kukamilisha malipo. Zipo kesi zishatokea na hadi mahakamani wameenda. Kibaya zaidi communication ni issue.Chinese Chinese everywhere

2. Export kitu chenye quality nzuri. Fuata makubaliano. Usiforge vitu kibongo kibongo. Akisema nyama iwe grade A basi hakikisha inakuwa grade A not B. Hii itaepusha usumbufu bandarini.

3. Katika hatua zoooote, hatua ya kutoa mzigo bandarini china ndiyo nzito. Hata hivyo vishoka wapo. Cha muhimu kujipanga tuu. Lakini quality ya mzigo ikiwa mbovu vishoka ni useless.

Nadhani inatosha kwa leo.
Bidhaa hotcake
1. Mbao aina ya redwood from brasil, India na Madagascar
2. Samaki, jina limepotea, wapo lake Victoria
3. Kuna raw material fulani ya kutengeneza nyuzi za kushonea watu wapofanyiwa operation
4. Ngozi za ng`ombe
5. Mchele, kwa kiasi kikubwa unatoka Thailand na Malaysia. Wao upo kama kitumbo rice.
6. Korosho
7. Ufuta
8. Alizeti
9. Nyama ya ng`ombe. Kuna wachina wanataka kufungua kiwanda cha kuchinjia ngo'mbe hapo tz kisha wana export mzima mzima. Ni hatari. Watz mmelala.
View attachment 314263 View attachment 314264
Mawasiliano ya jamaa wa silent ocean na The Land. nimeshindwa kuiweka juu ya thread naona kila nikiingia EDIT option ya picha ni kuattach linj tu na sio file. may be labda sijacop na mabadiliko ya jf interface mpya. kama @Invisible au @Moderator mnaweza kutusaidia kuweka ndani ya thread mwanzoni pale kama updates itakuwa vizuri
mkuu inategemea unafanya biashara ya aina gani. kuna biashara ambazo ukija wakati wa summer masoko ni mengi na bidhaa ni nyingi mfano bidhaa kama nguo(tunazovaa nyumbani ambazo nyingi ni nyepesi na kwa huku huvaliwa wakati wa summer) ukija wakati wa winter miez ya november-march hutapata machaguo mengi kwa sababu maduka mengi yatakuwa yanauza nguo za winter. lakini pia kama wewe ni mfanyabiashara wa spare parts kuja kipindi cha baridi inaweza kukupunguzia gharama za nauli mana kipindi hiki mashirika ya ndege huwa na ofa nyingi na pia abiria wanaosafiri ni wachache kwa hiyo bei ya nauli iko chini...kwa hyo inategemea mkuu
 
Last edited by a moderator:
Huko China. Hao wachinese wana demand nini kipo Tz kwa wingi kama electronics zilivyo nyingi kwao.

Mkuu, in most cases hawa jamaa wanahitaji MALI GHAFI kama vile MBAO zenye ubora ili kutengenezea samani mbalimbali. Pia wanahitaji sea products kama samaki wa aina mbalimbali kwa ajili ya kusindika.

Bidhaa nyingine ambazo watanzania tunaweza kuuza kwao ni kahawa, matunda hasa maembe! Juice ya maembe iko ghali sana China na nadhani ni kwa sababu wao hawalimi.

Nyama ya NG'OMBE hasa wanaotoka huku kwetu ni WATAMU ukilinganisha na nyama inayouzwa China ambayo haitoshelezi soko. . Ikumbukwe kuwa kuku na kitimoto ndio nyama rahisi inayoliwa na wachima
 
ushauri kama huu nchi za wenzetu tulitakiwa tuulipie ila hapa tunapewa bureee. Asante Nyerere kutuletea ujamaa, asante JF kutuletea jukwaa na ubarikiwe mleta uzi na kizazi chako

Ni kweli mkuu hii ni consultation na watu wanalipia ila kwa Tanzania acha tuwape watu bure ili tukuze uchumi wetu. Amiiin kwa dua!
 
Kipilipili

Ubarikiwe sana mtoa mada kwa mchango wako!,kwa vile bado sijawahi kufika china nitakuwa na vijiswali kadhaa,kwa kuwa namna pekee ya kujikomboa kiuchumi sio kuacha kabisa biashara za uchuuzi kwani swala hiyo haiwezekani popote pale bali kupunguza japo kidogo,

ss mkuu labda ungemshauri nini mtu ambaye ana mpango wa kuwa na kiwanda cha nyumbani(home industry)anunue mashine za gani kutoka china ambazo mtaji wake usizidi 3500-5000usd?,Natanguliza shukrani
 
Last edited by a moderator:
Ubarikiwe sana mtoa mada kwa mchango wako!,kwa vile bado sijawahi kufika china nitakuwa na vijiswali kadhaa,kwa kuwa namna pekee ya kujikomboa kiuchumi sio kuacha kabisa biashara za uchuuzi kwani swala hiyo haiwezekani popote pale

bali kupunguza japo kidogo,ss mkuu labda ungemshauri nini mtu ambaye ana mpango wa kuwa na kiwanda cha nyumbani(home industry)anunue mashine za gani kutoka china ambazo mtaji wake usizidi 3500-5000usd?,Natanguliza shukrani

Mkuu , huo mtaji wa 5000 USD( 5000X6.2 元= 31,000 &#20803😉huo ni mtaji mkubwa tu na unaweza kufanya biashara kwa baadhi ya vitu ikiwa tu hiyo itakuwa ni nje ya nauli na pesa ya kujikimu.
BACK TO YOUR QN. Sina current price ya baadhi ya machines lakini unaweza kununua machine zifuatazo kwa mtaji wako:
1. Machine ya kutengeza bisi(popcorn )
2. Machine ya kutengeneza ice cream/ barafu
3. mashine ya kutengenezea juice mbalimbali(juicer). kama machungwa(ninayo MPYA ambayo haitumii umeme, ukihitaji tuwasiliane)
4. Mashine ya kukaangia chips(ninayo MPYA,ukihitaji tuwasiliane)
5. Mashine ya kutotolea vifaranga
6. Mashine ya kubania glasi za juice km take away(ninayo MPYA, ntafute kama unahitaji )
Nk. Wengine wataongezea
 
Kipilipili,

Mkuu shukrani kwa kuorodhesha baadhi ya mashine ila mifano ya mashine ulizotoa ni za kawaida sana,Nilitegemea kwa uzoefu wako ungeniambia mashine simple ya kutengenezea mifuko laini, mifuko ya kaki,n mashine ndogo ya kutengenezea vitu kama take-away,mashine ya kutengenezea bic, mashine ndogo za kutengenezea viatu etc,hiyo ni mifano ila nategemea baada ya kusoma uzi huu utanielewa zaidi,Natanguliza shukrani
 
Mkuu shukrani kwa kuorodhesha baadhi ya mashine ila mifano ya mashine ulizotoa ni za kawaida sana,Nilitegemea kwa uzoefu wako ungeniambia mashine simple ya kutengenezea mifuko laini,mifuko ya kaki,mashine ndogo ya kutengenezea vitu kama take-away,mashine ya kutengenezea bic,mashine ndogo za kutengenezea viatu etc,hiyo ni mifano ila nategemea baada ya kusoma uzi huu utanielewa zaidi,Natanguliza shukrani

Asante mkuu, vizuri umeorodhosha vitu ambavyo ulikisudia. Ngoja niwaachie wengine watupe uzoefu katika vifaa hivyo
 
Asante mdau,bado nipo interested sana, labda nihangaike na capital😛anda:
 
Kipilipili

Ubarikiwe sana mtoa mada kwa mchango wako!,kwa vile bado sijawahi kufika china nitakuwa na vijiswali kadhaa,kwa kuwa namna pekee ya kujikomboa kiuchumi sio kuacha kabisa biashara za uchuuzi kwani swala hiyo haiwezekani popote pale bali kupunguza japo kidogo,

ss mkuu labda ungemshauri nini mtu ambaye ana mpango wa kuwa na kiwanda cha nyumbani(home industry)anunue mashine za gani kutoka china ambazo mtaji wake usizidi 3500-5000usd?,Natanguliza shukrani
The most useful thread
 
Nadhani hujanielewa. Hizo bidhaa ulizotaja ZIPO KWA WINGI kwa hiyo demand si kubwa kama NYAMA YA NG'OMBE

Kaka umetufumbua macho wengi sana. Hasa mimi. Naomba nikuulize kitu. Nikiwa na mil.1.5 nitapata mashine gani ya kufanyia biashara kwa maeneo yaliyopo mipakani?
 
Back
Top Bottom