China: Fursa za biashara, usafiri na masoko

Hii thread ni mzuri sanaa!!! Binafsi niko masomoni China. Na kila leo naona fursa mbali mbali kwa kweli!!!
Kwa wanaohitaji bidhaa za jumla kama nguo za watoto, nguo za kike na kiume, underwears kwa BELO viatu, machines, furniture kutoka China please
WhatsApp me +8618857052304
Na pita kwenye Instagram yangu @panda_sourcing @pamda_sourcing
 
wadau, naitaji maelekezo ya wapi ntapata chupi za kike na boxer za kiume zenye ubora nje ya nchi hususani china.

Hello, nipo China kama unahitaji chupi kwa bei ya jumla
WhatsApp me +8618857052305
Visit my Instagram page @panda_sourcing
 
Hii thread ni mzuri sanaa!!! Binafsi niko masomoni China. Na kila leo naona fursa mbali mbali kwa kweli!!!
Kwa wanaohitaji bidhaa za jumla kama nguo za watoto, nguo za kike na kiume, underwears kwa BELO viatu, machines, furniture kutoka China please
WhatsApp me +8618857052304
Na pita kwenye Instagram yangu @panda_sourcing @pamda_sourcing
HATOPIGWA MTU HAPA ?

"ILA MAISHA LAZIMA YAENDELEE."
 
Hapana mkuu, sifahamu, tuombe wengine wanaofahamu watusaidie hili
Nje ya mada kidogo:

Hivi mkuu unaweza kujua kampuni zinazosafirisha mizigo midogo kutoka India na Thailand kwa gharama nafuu ?
 
[Kipilipili]

  • Kipilipili asante kwa kutufungua macho!!..

    Nina mpango wa kuwa na kiwanda cha kidogo -mpaka cha kati. Sasa kuna mashine (food processing) kutoka China maana najua huko ndipo nitapata kwa gharama nafuu.. Please naomba contacts zako ili unipe ushauri zaidi..!!​

The bridge wapo wanausika na uzaji wa mashine mbalimbali

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mkuu kama utojali unaweza kunipatia namba tuyajenge zaidi
Mkuu Kipilipili, mimi nilikuwa Shaghai wakati wa CIP. Nilipitia pale kwenye soko lao la mnada nikachukua Laptop HP nane ambazo nilinunua kwenye 900 UAN kila moja. Nikipiga hesabu kwa madafu haikuzidi laki sita ila nilipokuja Bongo nilipata faida ya almost laki nne kwa kila laptop...Pia nilichukua iphon 7 na Samsung kadhaa ambazo airport vyote vilipita free...Nakuja huko mwezi wa pili nataka nifanye kabisa biashara ila nikiwa tayari na masoko kwa wanafunzi nk. Pia nataka nilete flight camera niziuze kwa wanahabari.

Vipi unaonaje soko la Shanghai kwa hizo bidhaa?
Una ushauri wowote wa bidhaa nyingine nzuri ambazo naweza kuchukua mbali ya hizo?

Ikibidi nikifika tuwasiliane mkuu ila nipe kwanza ushauri!

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Tafadhali naomba ushauri jinsi ya kuexport products zetu kwenda China; ni hatua zipi za kufuata ili na sisi tuwauzie bidhaa zetu.
Ungetaja bidhaa maalum (be specific) ingesaidia sana. Mana pamoja na kuwa na taratibu za jumla, lakini zipo ambazo zinategemea unasafirisga nini.
Changamoto kubwa iliyopo kwa watanzania kuuza bidhaa zao nje ni pamoja na:
1. Ubora (Quality) mf. Wenzetu wakisema wanataka upeleke machungwa UAE kwa mfano, basi fahamu si kwamba utaenda tu Muheza pale Tanga ukafungashe tu uwapelekee! Wenzetu huwa wanaweka vigezo (kulingana na nchi husika) kuanzia mbegu gani, mbolea gani itumike, uvunaji, ufungashaji nk. Sisi tunajijua wenyewe, mtu anaweza kuvuna kwa "kuchucha" machungwa kwa magongo ili aangushe mengi [emoji1][emoji1]. Kwa hiyo kabla hujazalisha bidhaa, cha kwanza ni kutauta soko, kisha angalia hilo soko linataka bidhaa yenye vigezo gani? kisha zalisha kulingana na soko husika. Mfano. Tantrade mara nyingi wanatangaza kwenye tovuti yao kuwa kuna masoko haya na haya na yanataka bidhaa yenye sifa ABCD...Sasa baada ya kujua sifa basi jipange ili uzalishe kulingana na sifa hizo.
Wakulima wa kitanzania, wengi wao wanalima kwanza kwa namna wanavyojua wao wenyewe, halafu ndio sasa wanakwambia wanatafuta soko ulaya! Tutaendelea kuyasikia tu masoko ya nje kwa mwendo huu! Hili ni tatizo hata kwa soko la ndani, mtu analima mpaka amemaliza halafu anakuja kwenye group la whatsApp anaandika "Jamani nna choroko tani 3, hivi soko la choroko liko wapi". Kwa hiyo moja ya jambo muhimu ni kutafuta kwanza ABC ya ubora wa hicho kitu unachotaka kuuza nje. Kama ni ngozi je inatakiwa ya ubora gani? kama ni ni zao la kilimo fatilia details zote na hizi huwa anaenunua ndio anazitoa kulingana na yeye anahitaji nini. Unaweza kuzipata hizi kupitia mawakala wa nje, kupitia tantrade, wizara ya viwanda, na pia kupitia bodi za mazao .
2. Kiwango (Quantity)
Siku zote mnunuaji wa nje anataka awe na supplier wa kuaminika (reliable supplier) ambaye atakidhi hitajio lake muda WOTE. Sio leo ameleta tani 2, kesho hana, miezi inapita tu! Watanzania wengi tunakwama hapa iwe kwenye malighafi, iwe kilimo nk. Kiwango runachozalisha ni kidogo mno! mfano, ukulima wa wengi ni wa kijungu jiko na hata wale wanaolima kisasa basi kiwango ni kidogo na kwa bahati mbaya wengi hawataki kukusanya nguvu pamoja (partnership) ili kulihudumia soko la nje kwa kiwango kinachohitajika. Ukiwa na gunia 100 za mahindi halafu unatafuta soko la nje kwa mfano, ni kiwango kidogo sana, na hiki kwa wakulima wa kawaida yaani hapo ndio amevuna haswaa! Wengi wa wakulima kwa mfano hata ile njia ya kutafuta out growers ili wawasimamie walime kisha wawauzie ili ukidhi kiwango cha soko la nje, bado watanzania wengi hawajafika kabisa katika uwezo huu. Kwa hiyo unapowaza kuuza nje, jiulize je uzalishaji wangu unakidhi kiwango na je utakuwa na mwendelezo au ni wa msimu? kumbuka kama unazalisha kwa msimu basi utapoteza wateja wengi sana na kila siku utajikuta unaanza moja
3. Wengi hawataki kufuata utaratibu (wanapenda shotcut). Hakuna biashara isiyo na urasimu! Watanzania wengi wakishaambiwa tu ili uuze nje kuna 1,2,3....9 basi wataishia katikati..wanaona kila kitu kama kigumu hivi! Mwisho watakuuliza "Hivi hauna mtu pale.......ili anisaidie" Yaani wanaamini lazima kila mahali uwe na "mtu" ndio utatoboa! Mambo mengine ni kufatilia tu na kukomaa! Wengi wakiona changamoto mbili tatu wanaachana na mchakato! Jambo la msingi ukitaka kuuza nje ni kuhakikisha uwe na utayari na uthubutu wa kufanya followup ya mambo na uwe active na positive muda wote!
4. Utafutaji na ufuatiliaji taarifa. Wengi watakwambia tupe taarifa , ohoo tupe mchongo flani, wakati hicho anachokwambia nipe kipo tu akigoogle atakipata ndani ya sekunde tu! lakini wanataka kila kitu waletewe waambiwe hiki hapa.
Mtu huyo anaekwambia nipe mchongo anashinda instagram na hajawahi hata kupitia hata tovuti ya Tantrade tu au hata kufika pale ofisi zao pale sabasaba, tena usishangae mtu mwenyewe anakaa mbagala[emoji1]. Sasa hangaika umtumie hizo taarifa. utatuma file 5 au 7 za taarifa, anaweza hata asidownload au akadownload halafu asizisome. Au mwengine atadownload na yeye atazituma kwenye group la whatsApp ili aonekane nae wamooo![emoji1]. Hivyo ushauri wa bure, hakuna atakaekuja kukupa taarifa, taarifa zinatafutwa na ukizipata zifatilie hatua kwa hatua usione ugumu. Mf. Ukiambiwa ili uuze muhogo China inabidi utambulike na taasisi husika China kwa kupitia wizara yetu ya viwanda na biashara basi fuatilia wizarani na jisajili ili uwe na sifa. Wengi waliotaka kuuza muhogo China waliposikia kuna kujisajili wakaona kama mchakato mrefu au kuna mlolongo lakini kimsingi hakuna, ni kuwa attention to details na kufuata utaratibu uliowekwa.
5. Uhifadhi na ufungashaji. Hapa tujifunze kwa wenzetu wakenya. Wana packaging nzuri sana. Sisi tukiletewa package nzuri, tunaona gharama, tunataka zile za yeboyebo za tsh 100 kariakoo. Usitarajie utauza nje ikiwa packaging yako ni mbovu! Wakenya wanakuja Tanzania kununua chai, kahawa pilipili mwendo kasi zetu halafu wanakwenda kuzipack upya na kuuza. Sisi tupo tu tunaishia lawama nyingi kama ndugu wa mume[emoji1]

Mimi mtu akinambia nipe taarifa, cha kwanza nataka yeye aseme amefanya juhudi gani kuzitafuta hizo taarifa. Taarifa zipo nyingi mtandaoni! nyingiii mnoo! Zipo katika balozi za nchi mbalimbali, kila ubalozi una kitengo hicho na taarifa zipo BURE kwa umma. Tuache uwoga, zile balozi sio vituo vya polisi. Mfano, kuna mtu alitaka kujua kuhusu soko la muhogo china. Nikamwambia nenda pale ubalozi wa china mtaa wa kajificheni! watakupa details zote, wizarani taarifa zote zipo! Nikamwambia pitia tovuti ya ubalozi wa Tanzania uliopo beijing zipo taarifa telee! Nikamwambia, weka oder request Alibaba, na wahitaji watakutafuta wao wenyewe mpaka utawakambia! Baada ya muda nikamuuliza huyu mtu umefikia wapi? Akaishia kujing'ata tu! Nikamtumia taarifa zote na mpaka leo yupo yupo anaishia kulaumu tu kila kitu lakini hakuna hatua hata moja aliyochukua.
Soko la nje kama mtu analitaka, halafu ni mvivu hata wa kugoogle, huyo aachane nalo tu, aendelee kuuza mahindi tule tushibe tu kwa kweli[emoji1]. Mana najua kuna wengine hawataki kuambiwa ukweli, hata tukiweka link za tantrade hapa, za wizara hapa, bado watazipita kama tangazo la ukimwi. Anaetaka utaratibu apitie tovuti za maeneo hayo niliyotaja. zipo aukigoogle hata sekunde haifiki utazipata.
Links:
Mwanzo |Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara Tanzania
Embassy of the United Republic of Tanzania Beijing, China
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
 
Breath in, breath out.....Relax! Mkuu , tunatofautiana watanzania, tuelimishane taratibu! Kuna wengine japo anatumia internet eg. JF lakini ukimwambia habari ya kusearch yaani umeshamvuruga, twende nao mdogo mdogo its a matter of time wataelewa tu.
Asante
Mkuu ni pm no yako plz nilikuwa nahitaji mashine mojawapo kati ya ulizonazo tufanye biashara
 
Hongera, mada nzuri Sana , Ina vitamini za kutosha. Eti unajamaa pale unaemfahamu anisaidie! Hiyo kweli ni matunda ya kutokujiamini.
 
Back
Top Bottom