China: Hatuna nia ya kukamata mradi wowote Afrika kwa sababu ya mkopo

Hoja sio kujengwa au kutojengwa bandari ya Bagamoyo bali vipengele vya mkataba kama vitahakikisha kuwepo kwa win win. Kwa nini ni muhimu:
1. Bandari ya Bagamoyo itakuwa na uwezo wa kupokea meli za kiwango cha 4th generation. Kwa hiyo mizigo mingi ya Tanzania na majirani zake kama DRC, Zambia, Rwanda, Malawi, Burundi na hata Uganda itabebwa na meli hizo. Hivyo bandari ya Dar out , au itapokea mizigo michache sana.
2. Endapo bandari ya Bagamoyo itajengwa na Wachina, watahakikisha shehena inayopokelewa/kutoka Tanzania au nchi jirani inapitia Bagamoyo ili warejeshe mtaji wao kwanza. Charity begins somewhere. Hili liko wazi.
3. Katika mazingira ya sasa ya biashara ya kimataifa upo uwezekano mkubwa mizigo mingi itakuwa ya China -kupokelewa au kupelekwa. Katika usafirishaji wa baharini shipping company ndiyo huamua bandari ya kushusha/kuchukulia mizigo. Ni wazi makampuni ya China yatapendelea Bagamoyo 'yao'.
4. Bandari ya Dar itabaki kupokea mizigo kidogo. Hata bandari za Zanzibar (ikiwemo inayotarajiwa kijengwa kwa ufadhili wa serikali ya Oman) zitaguswa na changamoto ya kupatikana mizigo ya kutosha. Je, hali kama hiyo haitaathiri vibaya mapato yake na mapato ya serikali kwa ujumla. Nani ataziba pengo hilo au serikali itakimbilia IMF/Benki ya Dunia.
5. Kama ufanisi wa bandari ya Dar utasuasua, je, hii haitaathiri mzunguko wa biashara katika jiji. Bagamoyo usije kuwa chazo cha Dar kusinyaa kibiashara.

Vipengele hivyo vinafikirisha lakini hatuna wasiwasi na umakini wa serikali katika suala hili lenye maslahi mapana kwa taifa kiuchumi na kisiasa.
 
Mpuuzi wewe, uchaguzi ulifanyika lini tukachagua hao wabunge wako
Whether uliwachagua or not ndio mbunge wako, so kazi yako ww ni kumbana adai mikataba ipelekwe bungeni. Kama wananchi hamuwezi kuwasimamia wabunge wenu then udhaifu unakua wa wananchi sio bunge.

Kila mtu akikutana na mbunge analia lia hana mtaji, sijui katapeliwa hati n.k ila hakunaga mtu anaehoji mambo ya kibunge kma sheria au regulations.

So shida inaanzia kwenu kabla ya bungeni
 
Faida ni kwenye multiplier effect ya mradi sio direct mapato kwa serikali. Mfano kma mapato yetu bandari Dar ni 1000 kwa mwaka wao wakipitisha mizigo Bagamoyo kwa spidi kubwa unakuta kwa mwaka wataingiza 3000. Ambapo kuna 1000 nzima itaishia kwa TZ sababu kuna mizigo itabebwa na SGR, Malori yetu, Benki za Tz zitapata ukwasi, ajira kwa service firms zote zitazowekeza bagamoyo, ATCL kuongeza wateja, Cross selling kupitia utalii na blue economy, n.k sasa kama hayo yote yatanyonya hyo 1000 kutoka kwa wachina hauoni itaziba pengo la hyo 1000 ambayo tulikuwa tunaipata bandari ya Dar??

Nadhani tukiangalia kwa upana huu utaona mradi una spillover effects nyingi kuliko risk ya kupoteza mapato.
 
Bagamoyo usije kuwa chazo cha Dar kusinyaa kibiashara.
Nadhani ni faida kubwa sana kwa nchi kama mikoa tofauti inageuka business hubs. So kama Dar itakufa kibiashara ila Bagamoyo ambayo ipo Tz ikapanuka kibiashara nadhani ni positive sababu tutakua na inclusive economy and urbanisation kubwa itatokea mkoa wa pwani kuelekea Tanga n.k so maendeleo yanatanuka.

So maadam Bagamoyo ni Tz then ondoa hofu hakuna hasara. Hta makao makuu yalipohamia dodoma tuliambiwa Dar ingekufa, ila that wasn't the case.
 
Deni la China kwa Zambia linatishia uhuru wa nchi hiyo hadi Rais wao mpya Hichilema kaamua ufanyike ukaguzi wa madenu yote upya na makubaliano mapya ya jinsi ya kuyalipa.
 
Ni lini mkataba umewahi kuwekwa mtandaoni, walau ungesema bungeni. Tatizo mnapenda speculation sio facts.
Siyo kweli. Terms na conditions za mikataba kwa mfano ya IMF na World Bank ziko mtandaoni. Hata letter of intent za hiyo mikopo wanaweka mtandaoni.
 
What about Zambia?
 
Uganda si wamedonate shule Chato?
 
Tukiwa tunapigwa tutajuaje? Wanataaluma wangapi wamefanya ufisadi kwenye historia ya nchi hii? Wanataaluma hawaaminiki tena bro. Zero trust.
 
Tukiwa tunapigwa tutajuaje? Wanataaluma wangapi wamefanya ufisadi kwenye historia ya nchi hii? Wanataaluma hawaaminiki tena bro. Zero trust.
Sasa kma wanataaluma ndio mafisadi ina maana mkataba uchambuliwe na laymen wa mtandaoni?

Maana nisichopenda ni watu wasio ma idea na uchumi wanataka kuchambua masuala ya kiuchumi. Mtu anakomaa kwamba kuna mkopo pale, wakati serikali ikijiingiza ni guarantor tu sio mkopeshwaji!!

Then kila mtu anawaza negative, mbona hatuogopi kwamba SGR tutaporwa ama tutaporwa Tazara kisa kuna hela ya mabeberu pale?

Tuwe optimistic
 
Siyo kweli. Terms na conditions za mikataba kwa mfano ya IMF na World Bank ziko mtandaoni. Hata letter of intent za hiyo mikopo wanaweka mtandaoni.
Kwani bandari ya bagamoyo serikali yetu inakopeshwa?? Mbona tunachanganyana mkuu.
Ni kama tu wachimba madini au gesi hawatukopeshi kitu ila wanawekeza hela yao na sie tunafaidika kwa concession agreement model tunayochagua.
 
Kila mtu wa mtandaoni siyo laymen. Ukishaanza na assumption hiyo utamaliza na wrong conclusion. Na wajibu wa hao wanataaluma ni kuwaeleza na kufanunua vitu kwa stakeholders ambao ni wananchi.
 
Kwani bandari ya bagamoyo serikali yetu inakopeshwa?? Mbona tunachanganyana mkuu.
Ni kama tu wachimba madini au gesi hawatukopeshi kitu ila wanawekeza hela yao na sie tunafaidika kwa concession agreement model tunayochagua.
Tuone mkataba kwanza kabla hatujaanza kujadili kipi kipo, kipi hakipo. Kipi kina faida, kipi kina hasara.
 
Tuone mkataba kwanza kabla hatujaanza kujadili kipi kipo, kipi hakipo. Kipi kina faida, kipi kina hasara.
Ni lini mikataba ilikua wazi Tanzania? Kuanzia wa SGR mpaka Ya Gesi ila kuna aliewahi kuhoji? Kipindi Tanzania inajitoa OGI mbona hamkupinga mlikaa kimya ila leo ndio mnahoji mikataba iwekwe wazi kwa sheria ipi? Hamkujua OGI ndio ilibana serikali kuweka wazi mikataba yote public?
 
Kila mtu wa mtandaoni siyo laymen. Ukishaanza na assumption hiyo utamaliza na wrong conclusion. Na wajibu wa hao wanataaluma ni kuwaeleza na kufanunua vitu kwa stakeholders ambao ni wananchi.
Hapo juu ulidai wanataaluma ndio mafisadi na walitufikisha hapa. Sasa kama hatuamini wasomi ndio tutaamini watu wa mtandaoni ndio wana uelewa na uzalendo?
Kidogo ungesema iundwe kamati kma ya prof.Osoro ipitie mikataba na itoe mapendekezo ila sio mkataba uwe mtandaoni wkt 90% ya waTZ hawana elimu na experience na sheria za kodi na mikataba.

Tutafanya subjective interpretation. Mfano economic benefit unakumbuka tulivyopotoshana humu mitandaoni kuwa ni faida (Mapato Ukitoa gharama za undeshaji) 50 kwa 50!!

Ndio mnataka interpretation za hivyo? Au ni bora zipite kwa tume yenye brains za kuweza kuchambua the ripoti yao ndio ije public
 
Hatujachelewa bado. Mikataba yote iwekwe wazi. Kuhusu mikopo nimeshakueleza mikopo ya IMF na WB iko wazi. Mikopo ya Mchina haiko wazi. Iwekwe wazi pia.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…