China imeachia bomu jingine kwenye ulimwengu wa AI — Kimi K3

Xi Jinping

JF-Expert Member
Joined
Jun 14, 2023
Posts
9,548
Reaction score
28,817
Mkurugenzi Mtendaji (CEO) wa kampuni changa ya Moonshot AI, Dkt. Yang Zhilin (miaka 34), ambaye ni mhitimu wa Chuo Kikuu cha Tsinghua, amezindua modeli mpya ya akili bandia (AI) iitwayo Kimi K3.

Kimi K3 imekuwa miongoni mwa modeli za AI zilizozungumziwa zaidi mwaka 2026 kutokana na uwezo wake mkubwa katika kufikiri kimantiki, uandishi wa programu (coding), na utekelezaji wa kazi za mawakala wa AI (AI agents)

Baadhi ya tathmini huru zimeonyesha kuwa katika baadhi ya majukumu maalumu inaweza kushindana kwa karibu au hata kuzizidi baadhi ya modeli za juu zinazotengenezwa na kampuni kubwa duniani

Athari za uzinduzi huu zimekuwa kubwa kiasi kwamba mahitaji ya kuitumia Kimi K3 yaliongezeka kwa kasi, na Moonshot AI ililazimika kuchukua hatua za muda kufunga maombi mapya kutokana na changamoto za miundombinu ya kompyuta kushindwa kuhimili idadi kubwa ya watumiaji kwa wakati mmoja

Maendeleo ya Kimi K3 yanaonyesha kasi kubwa ya ukuaji wa sekta ya AI nchini China, sambamba na modeli nyingine kama DeepSeek na Qwen ya Alibaba, jambo linaloifanya China kuwa mmoja wa washindani wakuu katika mbio za kimataifa za maendeleo ya akili bandia

Kwa sababu ya uwezo wake mkubwa na mfumo wake wa open-source/open-weight, Kimi K3 imeanza kuvutia shauku kutoka kwa watengenezaji, watafiti na makampuni mbalimbali duniani wanaotaka kuijaribu na kuchunguza uwezo wake wa kushindana na modeli zinazoongoza kutoka Marekani.

Wenye mamlaka Marekani wameingiwa na woga, mafanikio ya Kimi K3 yamezua taharuki Washington

TAARIFA MPYA: Utawala wa Trump unafikiria uwezekano wa kupiga marufuku modeli za AI za China zenye mfumo wa open-source ndani ya Marekani, kufuatia kuzinduliwa kwa modeli mpya ya AI ya China Kimi K3, kwa mujibu wa ripoti ya Axios 💔😅​
 
20260721_053526.jpg

BIG NEWS: Kimi K3 imepanda hadi nafasi ya #1 kwenye Frontend Code Arena ikiwa na alama 1679, ikiipita Claude Fable 5 ya Marekani​
 
Watakuja wapnge wale waabdu marekani
Walikuwa wakisema China iko nyuma ya Marekani kwa miaka 10 kwenye AI, lakini China imejibu kwa kasi ya ajabu

Kupitia ubunifu, uwekezaji mkubwa na vipaji vya watafiti wake, kampuni kama Moonshot AI, DeepSeek na Alibaba zimeifanya China kuwa nguvu kubwa inayotikisa uongozi wa AI duniani
 
Watakuja wapnge wale waabdu marekani
Hizi Promo ni za kawaida siku zote baada ya kuzinduliwa DeepSeek Ai wale Pro China walianza kutamba kuwa ina uwezo mkubwa zaidi ya Chat GPT, Gemini, Copilot na AI zingine .. muda ni mwamuzi mzuri leo hakuna tena tambo km hizi na Deepseek imeonekana si lolote..jambo la muhimu tuache ushabiki maandazi ktk mambo muhimu katika maendeleo ya mwanadamu..
 
Walikuwa wakisema China iko nyuma ya Marekani kwa miaka 10 kwenye AI, lakini China imejibu kwa kasi ya ajabu

Kupitia ubunifu, uwekezaji mkubwa na vipaji vya watafiti wake, kampuni kama Moonshot AI, DeepSeek na Alibaba zimeifanya China kuwa nguvu kubwa inayotikisa uongozi wa AI duniani
Ni vile tu watu wanakaza mafuvu Yao lakini China Kwa Technology Iko na speed ya Hali ya juu mno
 
Katika Mkutano wa Dunia wa Akili Bandia (World Artificial Intelligence Conference - WAIC) Shanghai 2026, Rais wa China Xi Jinping alisisitiza mambo makuu yafuatayo:
​
  • AI isiwe mali ya taifa moja pekee. Bali itumike kama teknolojia ya manufaa kwa dunia nzima kupitia ushirikiano wa kimataifa.​
​
  • Aliunga mkono open-source AI, akisema uwazi, kushirikiana na kugawana teknolojia vinaweza kuharakisha ubunifu.​
​
  • Alionya dhidi ya kuzuia maendeleo ya AI kwa kutumia hoja za usalama wa taifa ili kunufaisha nchi chache, akisema hilo linaweza kuleta pengo kubwa la kiteknolojia duniani.​
​
  • Alitangaza msukumo wa China kusaidia nchi zinazoendelea kujenga uwezo wa AI kupitia mafunzo na ushirikiano wa kimataifa.​

Kwa ufupi: Xi Jinping alitoa ujumbe kwamba China haitaki kuwa mtumiaji wa AI pekee, bali inataka kuwa mmoja wa waongoza mwelekeo wa AI duniani. ​
 
Hizi Promo ni za kawaida siku zote baada ya kuzinduliwa DeepSeek Ai wale Pro China walianza kutamba kuwa ina uwezo mkubwa zaidi ya Chat GPT, Gemini, Copilot na AI zingine .. muda ni mwamuzi mzuri leo hakuna tena tambo km hizi na Deepseek imeonekana si lolote..jambo la muhimu tuache ushabiki maandazi ktk mambo muhimu katika maendeleo ya mwanadamu..
Kusema DeepSeek si lolote si sahihi na hujui lolote kuhusu AI. DeepSeek haikuthibitisha kuwa imezidi kila AI duniani

Kila modeli ina nguvu na udhaifu wake; ChatGPT, Gemini, Claude na DeepSeek zote zina nafasi kulingana na kazi inayofanyika

Sasa nikupe sifa za DeepSeek:
​
  • DeepSeek V4 Pro iko kwenye kundi la AI za juu (frontier-level) na ni miongoni mwa modeli bora zaidi za China​
​
  • Katika baadhi ya vipimo iko karibu na modeli kama GPT-5 na Claude za juu, lakini bado mara nyingi iko nyuma kidogo ya modeli zinazoongoza kabisa za Marekani kwenye uwezo wa jumla​
​
  • Nguvu yake kubwa ni coding, ufanisi wa gharama, open-weight na uwezo wa kushughulikia muktadha mrefu (hadi takribani tokeni milioni 1)​

Nimekuwa nikitumia DeepSeek na nikilinganisha na modeli nyingine niseme tu yafuatayo:​
 
Nimetumia models zungine na DeepSeek haya ndiyo niliyojifunza:

Unajua ukitumia modeli zingine is like asking a very knowledgeable person with lots of stored information to do a calculus problem for you

Lakini mara zote ninapotumia Deepseek is like asking a Calculus professor to do it for you

DeepSeek mara zote imekuwa bora kwangu kwenye depth data analysis

Kuna watu wengine wamekuwa wakitumia DeepSeek kwenye coding problems hawataki tena kusikia uchafu wa ChatGPT

Kwenye issue za kiacademic hapo ndipo the real strength ya DeepSeek ilipo, nazungumzia the thinking process DeepSeek iko more interactive

Nyinyi majanja hamtaweza kunielewa ila kwa sisi tunaocheza na AI kwenye masuala ya academic huwa mwanetu ni DeepSeek, huyu nyangumi achana naye salute kwake
​
 
Ni vile tu watu wanakaza mafuvu Yao lakini China Kwa Technology Iko na speed ya Hali ya juu mno
Umesema vyema

Kitu kingine wanaoibeza China wapo kwenye kipindi cha coping (kukabiliana au kuzoea hali fulani ngumu, mabadiliko au changamoto)

Sio kwamba watu hawajaona maendeleo ya China, bali wengine wamekataa kukubali ukweli

China imepita hatua ya kuwa mfuatiliaji na sasa imekuwa mshindani mkuu wa teknolojia duniani

Kwa kasi ya AI, 5G, roboti, magari ya umeme na anga za juu, China inaonyesha kuwa haiwezi kupuuzwa tena

Historia ya teknolojia inaandikwa upya, na China iko mezani kama mmoja wa wahandisi wakuu

Rising Dragon, fading Eagle
​
 
Hizi Promo ni za kawaida siku zote baada ya kuzinduliwa DeepSeek Ai wale Pro China walianza kutamba kuwa ina uwezo mkubwa zaidi ya Chat GPT, Gemini, Copilot na AI zingine .. muda ni mwamuzi mzuri leo hakuna tena tambo km hizi na Deepseek imeonekana si lolote..jambo la muhimu tuache ushabiki maandazi ktk mambo muhimu katika maendeleo ya mwanadamu..
na kazia hapa
 
Hizi level huwa zinazofautiana kati ya benchmark moja na nyingine, but currently AI Marekani bado yupo mbele na hizo Claude unazoona apo ni moto wa kuotea mbali, saivi ndio AI bora zaidi duniani overall
 
China hawana mpango wa kutengeneza AI kubwa kuzidi zilizopo,mpango wa China kutengeneza ecosystem ya AI,washaona hawawezi ku catch up tena na marekani...

Na kama wakifanikiwa kutengeneza miundo mbinu hiyo,basi watakua mbali sana ki tech,wanataka tu AI iwasaidie nchi nzima kuanzia mkulima mdogo,dereva wa Tax,mwanafunzi and all..but sio ku compete...
 
Mkurugenzi Mtendaji (CEO) wa kampuni changa ya Moonshot AI, Dkt. Yang Zhilin (miaka 34), ambaye ni mhitimu wa Chuo Kikuu cha Tsinghua, amezindua modeli mpya ya akili bandia (AI) iitwayo Kimi K3.

Kimi K3 imekuwa miongoni mwa modeli za AI zilizozungumziwa zaidi mwaka 2026 kutokana na uwezo wake mkubwa katika kufikiri kimantiki, uandishi wa programu (coding), na utekelezaji wa kazi za mawakala wa AI (AI agents)

Baadhi ya tathmini huru zimeonyesha kuwa katika baadhi ya majukumu maalumu inaweza kushindana kwa karibu au hata kuzizidi baadhi ya modeli za juu zinazotengenezwa na kampuni kubwa duniani

Athari za uzinduzi huu zimekuwa kubwa kiasi kwamba mahitaji ya kuitumia Kimi K3 yaliongezeka kwa kasi, na Moonshot AI ililazimika kuchukua hatua za muda kufunga maombi mapya kutokana na changamoto za miundombinu ya kompyuta kushindwa kuhimili idadi kubwa ya watumiaji kwa wakati mmoja

Maendeleo ya Kimi K3 yanaonyesha kasi kubwa ya ukuaji wa sekta ya AI nchini China, sambamba na modeli nyingine kama DeepSeek na Qwen ya Alibaba, jambo linaloifanya China kuwa mmoja wa washindani wakuu katika mbio za kimataifa za maendeleo ya akili bandia

Kwa sababu ya uwezo wake mkubwa na mfumo wake wa open-source/open-weight, Kimi K3 imeanza kuvutia shauku kutoka kwa watengenezaji, watafiti na makampuni mbalimbali duniani wanaotaka kuijaribu na kuchunguza uwezo wake wa kushindana na modeli zinazoongoza kutoka Marekani.

Wenye mamlaka Marekani wameingiwa na woga, mafanikio ya Kimi K3 yamezua taharuki Washington

TAARIFA MPYA: Utawala wa Trump unafikiria uwezekano wa kupiga marufuku modeli za AI za China zenye mfumo wa open-source ndani ya Marekani, kufuatia kuzinduliwa kwa modeli mpya ya AI ya China Kimi K3, kwa mujibu wa ripoti ya Axios. 💔😅​
Kimi K3 iko close but sio top model, so kusema trump anawaza kupiga ban is a false wish

Najua unaipenda china but at this usishabikie bila kuelewa other AI models
 
Back
Top Bottom