Mkurugenzi Mtendaji (CEO) wa kampuni changa ya Moonshot AI, Dkt. Yang Zhilin (miaka 34), ambaye ni mhitimu wa Chuo Kikuu cha Tsinghua, amezindua modeli mpya ya akili bandia (AI) iitwayo Kimi K3.
Kimi K3 imekuwa miongoni mwa modeli za AI zilizozungumziwa zaidi mwaka 2026 kutokana na uwezo wake mkubwa katika kufikiri kimantiki, uandishi wa programu (coding), na utekelezaji wa kazi za mawakala wa AI (AI agents)
Baadhi ya tathmini huru zimeonyesha kuwa katika baadhi ya majukumu maalumu inaweza kushindana kwa karibu au hata kuzizidi baadhi ya modeli za juu zinazotengenezwa na kampuni kubwa duniani
Athari za uzinduzi huu zimekuwa kubwa kiasi kwamba mahitaji ya kuitumia Kimi K3 yaliongezeka kwa kasi, na Moonshot AI ililazimika kuchukua hatua za muda kufunga maombi mapya kutokana na changamoto za miundombinu ya kompyuta kushindwa kuhimili idadi kubwa ya watumiaji kwa wakati mmoja
Maendeleo ya Kimi K3 yanaonyesha kasi kubwa ya ukuaji wa sekta ya AI nchini China, sambamba na modeli nyingine kama DeepSeek na Qwen ya Alibaba, jambo linaloifanya China kuwa mmoja wa washindani wakuu katika mbio za kimataifa za maendeleo ya akili bandia
Kwa sababu ya uwezo wake mkubwa na mfumo wake wa open-source/open-weight, Kimi K3 imeanza kuvutia shauku kutoka kwa watengenezaji, watafiti na makampuni mbalimbali duniani wanaotaka kuijaribu na kuchunguza uwezo wake wa kushindana na modeli zinazoongoza kutoka Marekani.
Wenye mamlaka Marekani wameingiwa na woga, mafanikio ya Kimi K3 yamezua taharuki Washington
TAARIFA MPYA: Utawala wa Trump unafikiria uwezekano wa kupiga marufuku modeli za AI za China zenye mfumo wa open-source ndani ya Marekani, kufuatia kuzinduliwa kwa modeli mpya ya AI ya China Kimi K3, kwa mujibu wa ripoti ya Axios. 💔😅