China imeufunga huu mwaka kwa kishindo kikubwa imekuwa nightmare kwa watengeneza silaha wa Marekani na dalali wao Pentagon

Umeniwahi aisee!

Nami nilikuwa nawaza hivyo hivyo kama wewe.

Silaha nyingi za China ni untested kwenye uwanja wa vita.

Na ubora na ufanisi wa silaha zake si wa kuridhisha.

Naona watu wanazuzuka tu na maumbo ya hizo ndege na hizo meli.

Kwa kulinganisha tu bajeti za masuala ya ulinzi kati ya Marekani na China, bado Marekani iko juu sana.

Ukiwa na bajeti kubwa, utakuwa na uwezo wa kuboresha hazina yako ya silaha, utakuwa na uwezo mkubwa wa kuzifanyia majaribio, na utakuwa na uwezo mkubwa wa kufanya mambo mengi zaidi.

Bajeti ya China haifiki hata nusu ya Bajeti ya Marekani.
 
Marekani haijawahi kufanya testing hizi ni propaganda
 
Bajeti ya China haifiki hata nusu ya Bajeti ya Marekani.
Ikiwa kwa sasa China inatumia tu 1.6% ya GDP yake kwenye defense budget na infanya hayo yote vipi ikipandisha hadi kufikia 3.6% kama Marekani

Marekani ina bajeti kubwa kwa sababu ya military bases na kuanzisha au kuingia kwenye unnecessary conflicts

Na kingine ni kwa sababu ya upigaji unaofanywa na defense contractors, ndio maana hata project ya 6th Gen imekuwa paused kwa sababu ya cost overruns
 
Ukiwa na bajeti kubwa, utakuwa na uwezo wa kuboresha hazina yako ya silaha, utakuwa na uwezo mkubwa wa kuzifanyia majaribio, na utakuwa na uwezo mkubwa wa kufanya mambo mengi zaidi.
Mbona mara nyingi tu China wanafanya majaribio ya silaha zao na wanatest new type weapons inakuwa live fire drills
 
Nafikiri kila nchi ina oparation procedure zake .
 
China ina programu ya kununua wanasayansi dunia nzima na kuwapa wanachotaka katika mda wote lengo ni kuhakikisha wanakua kila mahali na jambo hili linaiumiza dunia nzima na kuna prof mmoja namjua alipewa Big project ya utafiti wa wanyama flani na presentantion ilifanyika China na hadi sasa he belong to them on every aspect of innovation . Ndo uelewe kwann wanapigwa kwa kila mahali ni sababu wanaiba wataalamu dunia nzima
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…