China imeufunga huu mwaka kwa kishindo kikubwa imekuwa nightmare kwa watengeneza silaha wa Marekani na dalali wao Pentagon

China imeufunga huu mwaka kwa kishindo kikubwa imekuwa nightmare kwa watengeneza silaha wa Marekani na dalali wao Pentagon

Tunataka kuziona kwenye mapambano front line, ampe hata Iran azijaribu pale Israeli ambapo USA ameweka zake.

Ampe Russia azitest pale Ukraine tuone uwezo wake, au alianzishe Pale Taiwan tuone uwezo wake.

Mwenzie USA silaha zake anazijua efficiency yake kwenye uhalisia Kwa maana uwanja wa vita maana ameshapigana vita nyingi na kufadhili vita nyingi, hii imempa nafasi ya kupima ufanisi wa silaha zake.

Japs aka Japan baaada yakuaccumulate silaha nyingi na kuvamia na kuziteka baadhi ya nchi akaona amemaliza na uwezo wake ni mkubwa, kilichomkuta hataki vita tena.
Umeniwahi aisee!

Nami nilikuwa nawaza hivyo hivyo kama wewe.

Silaha nyingi za China ni untested kwenye uwanja wa vita.

Na ubora na ufanisi wa silaha zake si wa kuridhisha.

Naona watu wanazuzuka tu na maumbo ya hizo ndege na hizo meli.

Kwa kulinganisha tu bajeti za masuala ya ulinzi kati ya Marekani na China, bado Marekani iko juu sana.

Ukiwa na bajeti kubwa, utakuwa na uwezo wa kuboresha hazina yako ya silaha, utakuwa na uwezo mkubwa wa kuzifanyia majaribio, na utakuwa na uwezo mkubwa wa kufanya mambo mengi zaidi.

Bajeti ya China haifiki hata nusu ya Bajeti ya Marekani.
 
Wakati SR-71 Blackbird inakuwa launched kulikuwa na ushahidi hata wa jina tu la ndege, achana na picha?

Siku F-117 Nighthawk inakuwa launched jeshini, kabla ya hapo kulikuwepo ushahidi wa picha? Hadi jina waliipa F- wakati ilitakiwa iwe B-.

U-2 Dragonlady ilianza kuruka 1955, hata raia wa Wamarekani wenyewe walikuja kujua kuna ndege kama hiyo mwaka 1960 ambapo Warusi walijua.

Marekani ina testing ground, jangwani uko. Hakuna photographer wala ndege zao hawazipitishi kwenye makazi ya watu wakiwa wanafanya testing. Ndege zote za Marekani huwa zinaonekana kwenye matukio maalum yaliyopangwa. Sio kama Wachina watu wapo wanakunywa supu, wanaona ndege angani wanapiga picha.
Marekani haijawahi kufanya testing hizi ni propaganda
 
Bajeti ya China haifiki hata nusu ya Bajeti ya Marekani.
Ikiwa kwa sasa China inatumia tu 1.6% ya GDP yake kwenye defense budget na infanya hayo yote vipi ikipandisha hadi kufikia 3.6% kama Marekani

Marekani ina bajeti kubwa kwa sababu ya military bases na kuanzisha au kuingia kwenye unnecessary conflicts

Na kingine ni kwa sababu ya upigaji unaofanywa na defense contractors, ndio maana hata project ya 6th Gen imekuwa paused kwa sababu ya cost overruns
 
Ukiwa na bajeti kubwa, utakuwa na uwezo wa kuboresha hazina yako ya silaha, utakuwa na uwezo mkubwa wa kuzifanyia majaribio, na utakuwa na uwezo mkubwa wa kufanya mambo mengi zaidi.
Mbona mara nyingi tu China wanafanya majaribio ya silaha zao na wanatest new type weapons inakuwa live fire drills
 
Wakati SR-71 Blackbird inakuwa launched kulikuwa na ushahidi hata wa jina tu la ndege, achana na picha?

Siku F-117 Nighthawk inakuwa launched jeshini, kabla ya hapo kulikuwepo ushahidi wa picha? Hadi jina waliipa F- wakati ilitakiwa iwe B-.

U-2 Dragonlady ilianza kuruka 1955, hata raia wa Wamarekani wenyewe walikuja kujua kuna ndege kama hiyo mwaka 1960 ambapo Warusi walijua.

Marekani ina testing ground, jangwani uko. Hakuna photographer wala ndege zao hawazipitishi kwenye makazi ya watu wakiwa wanafanya testing. Ndege zote za Marekani huwa zinaonekana kwenye matukio maalum yaliyopangwa. Sio kama Wachina watu wapo wanakunywa supu, wanaona ndege angani wanapiga picha.
Nafikiri kila nchi ina oparation procedure zake .
 
China huwa hafanyi research, ukiona katoa kitu ujue ameshaona mchoro mahala. Yeye matoleo yake ukiyafuatilia utagundua kwa Euro na US ni ngazi ya research, tena hata hawajafika hatua ya kuomba vibali vya majaribio.
Anapenda kuwa wa kwanza ku release halafu sokoni havidumu hata wiki mbili.
Silaha zake nyingi hata hezibollah waliona hazifai, wakaona ni bora hata ya kombeeo na manati
China ina programu ya kununua wanasayansi dunia nzima na kuwapa wanachotaka katika mda wote lengo ni kuhakikisha wanakua kila mahali na jambo hili linaiumiza dunia nzima na kuna prof mmoja namjua alipewa Big project ya utafiti wa wanyama flani na presentantion ilifanyika China na hadi sasa he belong to them on every aspect of innovation . Ndo uelewe kwann wanapigwa kwa kila mahali ni sababu wanaiba wataalamu dunia nzima
 
FB_IMG_1735623539897.jpg
 
Back
Top Bottom