China imeufunga huu mwaka kwa kishindo kikubwa imekuwa nightmare kwa watengeneza silaha wa Marekani na dalali wao Pentagon

Marekani walifanyia wapi hiyo testing?

Maana popote ukienda testing ya China ya 6th Gen ndiyo inajulikana ya kwanza duniani

Hiyo project ya NGAD imesimamishwa maana gharama ni kubwa na design yake mpaka imekuwa outdated
 
Marekani anatumia 3.6% ya bajeti kwenye ulinzi, kumbuka Marekani analinda Dunia nzima😂. Kambi za kijeshi kila kona ya Duniani hadi angani (Us Space Force).
China anatumia 1.6% tu ya GDP yake lakini bado anampa challenge na hata kumu-outcompete Marekani.

Marekani ana kambi nyingi za kijeshi kwa ajili ya kulinda maslahi yake ya kigeopolitics na zinamcost sana kuzigharamia

Sasa ona tofauti ya Mchina na Marekani: Wakati Marekani kawekeza kwenye military bases Mchina amewekeza kwenye ports, Mchina anamiliki kwa sehemu au kwa 100% bandari nyingi duniani kwa ajili ya kibiashara

Unafikiri kati ya Marekani na China nani amezichanga karata zake vizuri na anapata benefit?

Juzi Trump ameshtuka kuwa sehemu ya bandari katika Panama canal iliyojengwa na Marekani miaka ya zamani inamilikiwa na China inawaingiza Wachina billions of dollars

Wivu umemshika mpaka ameanza kuitia mikwara Panama. Ndio ujue hizo military base zake hazina faida kama China anayopata kwenye ports hasa kibiashara
 
Wakuu hivi hizi ndege zenye low RCS hazitunguliki kabisa? Chini ya Zelensky tunaona leo Russia anashambuliwa na Sukhois na Mig alizoziunda mwenyewe, hivi ikitokea mbeleni huko US akatwangana na say Uholanzi ambae yuko armed na F-35, inamaana US pia hana namna ya kuziangusha hizi ndege alizoziunda mwenyewe? Wajuzi naomba elimu kwenye hili.
 
Boeing again 🤣

Hizo drones hazina stealth capabilities kama GJ-11

GJ-11 ni super stealthy combat drone
GJ-11 ni combat drone, Boeing Stingray ni refuering tanker drone. Kama unalinganisha stealth features za combat drone linganisha GJ-11 na X-47B.

Na hata kwenye stealth kwenyewe, F-35 ni stealth zaidi ya J-20 na husemi.

China wana refuering drone gani tena ambayo ni stealth?
 
Usiseme China hana haja kuwa na presence kila bahari, sema hana uwezo.

Kwa mfano angekuwa na haja, angeenda kwa meli zipi? China ana meli ngapi za kufaa kuwa flagships? Ana battle groups ngapi, ana naval air power kiasi gani kumtosheleza kuwa dunia nzima. Sema hawezi usiseme hana haja, sizitaki mbichi hizi.
 
Marekani hawana drone AWACS so it means wamepigwa gap na China katika hilo

Na sio tu wamefanya testing ni successful testing hiyo ni green light kuwa inaingia mzigoni
Marekani hawahitaji drone AWACS bali drone tanker ambayo China hawana.
China hawana carrier based AEW&C ndio maana wanataka kuunda kadrone. Marekani anayo E2-D Advanced Hawkeye ambayo inakazidi hako kadude unakoringia

Carriers za ndege za Marekani ni superior hivyo waliweza tengeneza ndege nzito inayotua kwenye carrier, Wachina hawawezi ndio wamekimbilia kwenye kadrone hako mpaka pale KJ-600 itakapokamilika. Marekani ana carrier based AEW&C tangu 1960s China ndio anajitutumua sasahivi na yamemshinda amejishikiza kwenye kadrone kwanza.

Pia China hawana 6th generation bomber wakati Marekani wana B-21.

China vilevile hawana 5th generation bomber, US wana B-2.

China hawana nuclear powered aircraft carrier hata ya kwenye mchoro, Marekani anazo 11 Nimitz class 10 na Ford class 1.
 
Capability ya China kwenye ship building industry ni mara 230 ya Marekani. Sijui kama unaelewa hiyo hesabu hapo

Yaani kwa kifupi linapokuja suala la kutengeneza na kuunda meli China imeiacha mbali sana Marekani.

Kwa hiyo huo uwezo anao ndio maana China inaweza kutengeneza meli vita kwa haraka kwenye docks hata 10 kwa wakati moja kitu ambacho Marekani hata dock 2 kutengeneza meli kubwa hana

Ndani ya miaka 10 iliyopita China imeunda meli vita nyingi kwa mbali kuliko Marekani na gap linazidi kuongezeka ya fleets

Ndiyo maana Marekani mameli yake mengi yamezeeka yako docks anashindwa kuyakarabati. Ashukuru sana msaada wa Japan na South Korea wanampiga tafu

Na hata Japan na S.K wakiungana bado hawamfikii Mchina achana na Marekani ambayo docks zake zote ni sawa na mbili tu zilizo Shanghai
 
J-35 ni stealth zaidi ya F-35 linganisha F-35 na J-35 ndio nasema sasa
Siwezi linganisha ndege iliyopo active kwenye majeshi na ndege iliyo kiwandani inapakwa rangi na kuchokonolewa hata haijulikani itaanza kuwa kwenye production lini.

Basi sawa F-22 inaizidi J-20, na bado F-35 inaizidi J-20.
 
Marekani ina nuclear powered aicraft carriers 11, China ina sifuri.

Nikienda kwenye namba ya nuclear powered submarines Marekani anazo 66, China anazo 12.
Huo uwezo wa China unautoa wapi?

Wewe unahesabu hivyo vidumu ambavyo China anajenga unahisi Marekani hawezi.
Ni kwamba hataki takataka siziso na kazi. Mwaka 1940 US ilitoa Emergency Shipbuilding Program ikaunda melivita 6,000 ndani ya 5 years. Leo 2024 ikiamua utajificha.
 
Siwezi linganisha ndege iliyopo active kwenye majeshi na ndege iliyo kiwandani inapakwa rangi na kuchokonolewa hata haijulikani itaanza kuwa kwenye production lini.

Basi sawa F-22 inaizidi J-20, na bado F-35 inaizidi J-20.
Wewe ndio umasema haipo active lakini kihalisi J-35 ni mkali wa stealth kwa fighter jet zote sio F-22 wala F-35
 
Hana uwezo upi ?wa kutengeneza au wa kufanya nini ?


By the way marekani na China wana foreign policies tofauti.

Si ajabu kuna siku utataka China aanze ku behave kama marekani kwenye kila vita na mgogoro kwa kusingizio hana uwezo
 
1940 ni wakati wa WW2 uhitaji ulikuwa mkubwa ship building capability kwa sasa marekani huwezi iweka kwenye mezani sawa na China ni jambo ambalo hata wamarekani wenyewe wana lalamika.

Marekani ya 2024 si sawa na marekani ya 1940 wakati wa WW2
 
Wanatangaza biashara, kunapokuwa na hofu ya vita mauzo yanaongezeka. Kinachofuata ni kutengeneza hofu.
 
1940 ni wakati wa WW2 uhitaji ulikuwa mkubwa ship building capability kwa sasa marekani huwezi iweka kwenye mezani sawa na China ni jambo ambalo hata wamarekani wenyewe wana lalamika.

Marekani ya 2024 si sawa na marekani ya 1940 wakati wa WW2
Mwaka 1939 walikuwa hawaundi meli nyingi, mwaka 1940 wakaanza kuziunda kama utitiri mpaka baada ya vita kuisha wakaziuza kama kuzitupa wafanyabishara wakazibadili zibebe mizigo.

Ninachomaanisha tech, shipyard, know how haifi. Kwa sasa Marekani yupo kona zote za maji duniani na ana bases kubwa na ana presence kwenye international waters mwaka mzima hahitajiki kuunda meli kwa rate kubwa. China ukimtaka awe na fleets hata 5 hawezi, China ana bahari kubwa duniani anakaa mwaka hajawahi pitisha melivita, hana bases, hana battle groups.
 
Hana uwezo upi ?wa kutengeneza au wa kufanya nini ?


By the way marekani na China wana foreign policies tofauti.

Si ajabu kuna siku utataka China aanze ku behave kama marekani kwenye kila vita na mgogoro kwa kusingizio hana uwezo
Kuna kuwa na uwezo wa kufanya kitu ila ukajizuia usikifanye, kuna kutokuwa na uwezo wa kufanya kitu kwahiyo hata kujizuia usifanye huwezi kwa sababu tiyari uwezo wa kukifanya huna.

China hana uwezo wa kuwa kila bahari kuu duniani. Akikaa South China sea, North Pacific na Indian ocean basi yeye kamaliza. Huwezi muona Atlantic akiwa na battle group, au Red Sea na Mediterranean. Wala China hafanyi patrols nyingi bahari za mbali yake.
 
Blah blah kibao mchina hajawai kuwa serious na kazi zake.hizo ndege zinaweza kushindwa kutoa matairi zikitaka kutua.
Mchina ni copy na paste hilo lipo wazi kwa kifupi mchina ni mpiga chabo mwizi namba 1 duniani akiona Us na Western Europe wametoa majibu juu ya shida fulani za dunia ndo sasa naye anacopy na anaweka mbwembwe nyiiingi wachina wa JF wanaita innovations🤣😂
Ndo maana mchina alipeleka na anapeleka wachina wengi sana kusoma US mpaka leo ili waweze chukua maarifa yaliyo US na kuyapeleka china.
Yaani mchina ni sawa na wale wanafunzi wanaoibiaga majibu darasani halafu akishaibia anaongeza mbwembwe zake.
 
Umeelezea vizuri
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…