Unamaanisha nini mkuu - juzi hapa si amerusha wana anga watatu kwenda kwenye space station yake watakaa huko kwa miezi mitatu, China ndio Taifa pekee Duniani ambalo limefanikiwa kutuma chombo mwezini kikatua upande wa pili wa mwezi ambao hauonekani Duniani - kinacho washangaza wana sayansi wa NASA na Warusi ni kule kufanikiwa kwa Wachina ku-maintain mawasiliano ya radio frequency 24X7 baina ya chombo na base stations za hapa Duniani kikatuma picha pamoja na video seamlessly!! Si Amerika wala Urusi walio wahi kufankisha kitu kama hicho, vyombo vyao vya anga vilipokuwa vinazubguja upande wa pili wa mwezi basi mawasiliano baina ya chombo na aridhi yanakatika mpaka chombo kinapo rudi upande wa pili unao onekana ukiwa aridhini/Duniani - cha kujiuliza hapa Wachina wakitumia mbinu gani kuwapiku wenzao?
Hilo la kwanza, la pili - mwishoni mwa mwaka jana chombo cha anga cha Wachina kiliganikiwa ku-land kwenye sayari ya MARS ambayo umbali wake kutoka aridhini ni makumi ya mamillion Kilometer kilituwa kwenye aridhi ya MARS, kikashusha mobile rover yenye magurudumu ikafanya tour sehemu mbali mbali,ikapima: composition za udogo,hali ya hewa,kupiga high resolution picha na video na kuzituma Duniani - kama unafikiri hilo in jambo dogo kisayansi na kitekinilojia you better think again.
La tatu lina husu jeshi la Uchina kumiliki makombora type ya hypersonic ambayo hata Merikani imekuwa mkweli kwa kusema hawana kinga yoyote ya kulinda Taifa lao dhidi ya makombora/missiles hizo hatarishi, ni mataifa mawili tu Duniani yenye kumiliki hypersonic missiles, nayo ni: ni Uchina na Urusi basi, Amerika inajitahidi kuunda za kwao lakini mpaka sasa hawaja fanikiwa, majaribio yao yote yame-fail, who knows may be watafanikiwa eventually.
Haya sasa tuje kwenye teknilojia ya mawasiliano na hapo Uchina imeyapiku mataifa ya magharibi kwenye nyanja za 5G technology, Wachina ndio wamefanikiwa kuunda a truly 5G stuff unlike mataifa mengine yanayo tinker around na 4G technology halafu wanazuga watu kwamba na hiyo 5G
technology lakini uki-check bit rate throughput unagunduwa kumbe ni dead slow compared na Chinese Huawei stuff, ndio maana Pompeo alilikuwa ana endesha kampeini ya ulaghai tu kwa kusingizia Huawei kwamba katika vifaa vyao vya mawasiliano wame-embed software za kudukuwa watumiaji, anatisha tisha Mataifa kwamba wasinunue equipment za mawasiliano zinazo undwa na Huawei - lengo likiwa kuihujumu China kiuchumi.
Kwa kumalizia - je,una habari kwamba Uchina ndilo Taifa linao ongoza Duniani kwa kuunda fastest super computer wametumia hardware zinazo zalishwa huko huko Uchina kuanzia: Microprocessor, Memories nk. Wachina wameunda Quantum Computers, Quantum radar zenye uwezo wa ku-identify Stealth bombers na fighters, hapo hatujagusia kuhusu maendeleo makubwa kwenye masuala ya teknilojia ya Artificial Intelligence (AI) hivi asa China imeipiku US na mataifa ya Ulaya kwenye teknilojia ya AI.Bottom line is: Hivi ni sekta hipi ambayo Wachina hawana uwezo wa kutoa ushindani. Wachina kitu ambacho hawafanyi ni kutambia mataifa mengine, kuvamia au kupiga mabomu Mataifa ambayo hawayapendi, kuchochea vurugu na ku-assassinate viongozi bila sababu zozote za msingi - Wachina hawana tabia hizo za kishenzi.