China kajipambanua kama chui wa karatasi: Hapa bongo tunasema ni "nyoka wa kibisa"

mbingunikwetu

JF-Expert Member
Joined
Feb 17, 2015
Posts
13,897
Reaction score
18,477
Mabeberu yameshamgundua china kuwa ni chui wa karatasi! Chui wa karatasi ana sura ile ile ya chui na ametoa meno lakini hawezi kuuma!! Ni sawa na nyoka wa kibisa ambaye hata watoto huwa wanaweza kucheza naye maana alishatolewa meno!

China ilibweka sana kutishia Spika wa bunge la marekani Pelosi asitembelee Taiwan ambayo kimsingi ni sehemu ya china!! Akaandaa mameli na midege ya kijeshi lakini kumbe wenye akili zao walijua anatishia nyau na Pelosi alienda Taiwan na Kurudi bila shida yoyote! baada ya hapo china ikaizingira Taiwan kwa mimeli ya kijeshi pande zote na ikafanya mazoezi ya kijeshi ya kufa mtu lakini mabeberu wakamcheka tu na hujiendea Taiwan na kurudi na china kuishia kubweka hadi aibu!!

Hivi sasa tunavyozungumza kuna ziara nzito ya wabunge wa Canada wakitembelea Taiwan "nchini China" kinyume na matakwa ya China na bila aibu China imebweka tena huku ikijua kuwa imeshagundulika kuwa ni "chui wa karatasi". Ili kuondokana na aibu hii mara mia China iamue kuachana rasmi na Taiwan na kuitangazia uhuru wake kuliko hii aibu ya kubweka kila leo huku dunia nzima inajua ubavu wa kung'ata haina!!

Isijidanganye kuwa miongoni mwa wababe ambao wakisema kitu huwa hawapepesi macho!! Hapo ndipo ninapoziheshimu nchi kama Iran, Korea ya kaskazini, Uturuki na baba lao Urusi!!

Beijing fumes over latest foreign visit to Taiwan​

A trip to Taipei by Canadian lawmakers “grossly interfered” in China’s internal affairs, Beijing said
Beijing fumes over latest foreign visit to Taiwan

© Twitter / MOFA_Taiwan
The Chinese government has condemned a recent visit to Taiwan by Canadian MPs, demanding that Ottawa cease direct diplomatic ties with the island and respect its territorial claims.
In a statement issued to the Globe and Mail on Thursday, China’s embassy in Canada denounced a trip to Taiwan by Liberal lawmaker Judy Sgro and other members of the ‘Canada-Taiwan Parliamentary Friendship Group,’ which began last Sunday.

“China has consistently and firmly opposed any form of official exchanges between the Taiwan region and countries having diplomatic ties with China,” it said, adding that the visit “blatantly violates the one-China principle, grossly interferes in China’s internal affairs and sends a seriously wrong signal to the ‘Taiwan independence’ separatist forces.”
 
Uturuki iliwahi kuiambia Urusi, ulisogeza ndege zako kwenye anga yangu (wakati wa mgogoro wa Syria) naitungua, Urusi akadhani masihra akapitisha ndege yake ya kijeshi uturuki akaitungua na ikajizolea heshima!! Leo hii Urusi na Uturuki wanaheshimiana japo Urusi ana nguvu zaidi!!
Korea ya kaskazini iliiambia marekani na korea ya kaskazini miaka ya nyuma walipokuwa wanafanya mazoezi ya kijeshi kuwa meli yoyote ya kijeshi ikisogea kwenye usawa wa eneo langu la bahari nitaizamisha! Wakajifanya kichwa ngumu wakapeleka manowari yao eti imepotea njia kwa bahati mbaya, haikurudi! ikazamishwa jumla!

Iran iliiambia marekani ni lazima italipiza kisasi kwa kuuliwa jemadari wake na marekani nchini Iraq!! Haikupepesa macho, kambi ya kijeshi ya marekani nchini Iraq ilishambuliwa na wimbi kali la makombora na marekani ikalazimika kupotezea!!
Na baba lao Urusi ilishasema NATO waseme wazi kuwa hawataipokea ukraine kwenye umoja wao na ukraine itamke kuwa neutral vinginevyo huo ni mstari mwekundu!! Wakafikiri Urusi ni kama mchina matokeo yake Urusi imevamia ukraine na imeshahalalisha kuchukua majimbo manne ya ukraine kuwa sehemu ya urusi na habari ndiyo imeishia hapo!! NATO watapiga makelele na kujaribu kuisaidia ukraine lakini kamwe hawatafika popote!!

China ijifunze kwa wababe hao!! Ubabe ni kukubali hasara lakini ukatunza heshima!!
 
1_660_111612013543.jpg

Hawa top elite wa China sio wajinga wala wazembe kama wewe unavyo tanabaisha hapa , maamuzi yote wanayo fanya China yana fanyiwa upembuvi akinifu kuliko wewe unavyo dhani. China imefanya ukombozi na kurudisha maeneo yake mbalimbali mengi sana mfano Tibet, Hong Kong , Macau tena mengine bila kurusha hata risasi hata moja usiwachukulie China kawaida .

Haya mambo tuwa achie wataalamu wenyewe wa CPC na PLA wamalize Vita vyao vya wenyewe kwa wenyewe na hao ROC katika njia wao wanayo ona ni bora zaidi, haya mambo yanahitaji mipango sio mihemko kama unavyo dhani.

Maamuzi yote ya China lazima yapite humu na kuwanyia upembuvi akinifu ndipo yatekelezwe👇
41296e54-129d-43b6-a02d-c2955ff49922.jpeg
53607470_303.jpg
5a0cf54ba31061a720dbd9b1.jpeg
618da386a310cdd3d819d841.jpeg

: Tusubiri maamuzi ya chama kuanzia Oktoba 16 nini kitajadiliwa hapo Great Hall of people Beijing tutajua ni namna gani PRC watalikabili swala la mgogoro wao na ROC.
 
View attachment 2386678
Hawa top elite wa China sio wajinga wala wazembe kama wewe unavyo tanabaisha hapa , maamuzi yote wanayo fanya China yana fanyiwa upembuvi akinifu kuliko wewe unavyo dhani. China imefanya ukombozi na kurudisha maeneo yake mbalimbali mengi sana mfano Tibet, Hong Kong , Macau tena mengine bila kurusha hata risasi hata moja usiwachukulie China kawaida .

Haya mambo tuwa achie wataalamu wenyewe wa CPC na PLA wamalize Vita vyao vya wenyewe kwa wenyewe na hao ROC katika njia wao wanayo ona ni bora zaidi, haya mambo yanahitaji mipango sio mihemko kama unavyo dhani.

Maamuzi yote ya China lazima yapite humu na kuwanyia upembuvi akinifu ndipo yatekelezwe👇
View attachment 2386691View attachment 2386692View attachment 2386693View attachment 2386694

: Tusubiri maamuzi ya chama kuanzia Oktoba 16 nini kitajadiliwa hapo Great Hall of people Beijing tutajua ni namna gani PRC watalikabili swala la mgogoro wao na ROC.
Lazima watanywea maana hawatakuwa tayari kukabiliana na gharama na matokeo ya kutumia nguvu kuichukua Taiwan!! Ni kama wameshachelewa!! Lakini pia China inautegemea sana ulimwengu wa magharibi kwa kuuza bidhaa zake ambazo siyo za lazima kwa maisha ya kila siku!! Anajua akiwekewa vikwazo atafilisika na hayuko tayari kufilisika!
 
Kwanza kabla ya yote nikuulize swali moja: Mkuu mgogoro wa PRC na ROC umeanza kuufatilia toka lini [ mwaka gani ] ?
 
Gharama ya heshima ni kubwa sana!! Ni nchi chache sana zinazoweza kulipa gharama hiyo!! Kwa mfano, inajulikana wazi kuwa China inaiunga mkono Urusi kwenye mgogoro wa ukraine, lakini haiwezi kuthubutu kupiga kura UN kupinga azimio la kuilaani Urusi na itaishia KUTOKUPIGA KURA! Lakini Korea ya kaskazini haipepesi macho bali inapiga kura tena ya wazi kupinga azimio lolote la kuilaani urusi!! China ni rafiki mwoga kwenye ugomvi atakukimbia!!
 
Kwa taarifa yako mimi nakimbilia miaka 70!! Mgogoro huu ninaujua toka vita vyao vya wenyewe kwa wenyewe enzi ya Mao!! Hao walioko Taiwan walishindwa vita wakakimbilia kisiwa cha Taiwan!! Kubali tu kunipa shikamooo!!
 
Kwa taarifa yako mimi nakimbilia miaka 70!!
Kulikuwa hakuna umuhimu wowote wewe kuandika hiki ulichoandika hapa.
Mgogoro huu ninaujua toka vita vyao vya wenyewe kwa wenyewe enzi ya Mao!!
Mwaka gani mgogoro umeanza kuufatilia ? sio hiki ulichoandika sija uliza ulicho jibu.
Hao walioko Taiwan walishindwa vita wakakimbilia kisiwa cha Taiwan!! Kubali tu kunipa shikamooo!!
Mkuu sikuhitaji haya maelezo, ungejibu swali tu.

: Mkuu turudi kwenye swali nililo kuuliza
 
Gharama ya heshima ni kubwa sana!! Ni nchi chache sana zinazoweza kulipa gharama hiyo!! Kwa mfano, inajulikana wazi kuwa China inaiunga mkono Urusi kwenye mgogoro wa ukraine, lakini haiwezi kuthubutu kupiga kura UN kupinga azimio la kuilaani Urusi na itaishia KUTOKUPIGA KURA! Lakini Korea ya kaskazini haipepesi macho bali inapiga kura tena ya wazi kupinga azimio lolote la kuilaani urusi!! China ni rafiki mwoga kwenye ugomvi atakukimbia!!
Una fahamu msimamo wa China kwenye huu mgogoro kati ya Russia na Ukraine ?
 
View attachment 2386678
Hawa top elite wa China sio wajinga wala wazembe kama wewe unavyo tanabaisha hapa , maamuzi yote wanayo fanya China yana fanyiwa upembuvi akinifu kuliko wewe unavyo dhani. China imefanya ukombozi na kurudisha maeneo yake mbalimbali mengi sana mfano Tibet, Hong Kong , Macau tena mengine bila kurusha hata risasi hata moja usiwachukulie China kawaida .

Haya mambo tuwa achie wataalamu wenyewe wa CPC na PLA wamalize Vita vyao vya wenyewe kwa wenyewe na hao ROC katika njia wao wanayo ona ni bora zaidi, haya mambo yanahitaji mipango sio mihemko kama unavyo dhani.

Maamuzi yote ya China lazima yapite humu na kuwanyia upembuvi akinifu ndipo yatekelezwe[emoji116]
View attachment 2386691View attachment 2386692View attachment 2386693View attachment 2386694

: Tusubiri maamuzi ya chama kuanzia Oktoba 16 nini kitajadiliwa hapo Great Hall of people Beijing tutajua ni namna gani PRC watalikabili swala la mgogoro wao na ROC.

kama una uwezo wa kumaliza migogoro yako kwa njia bora kabisa ya kidiplomasia kwanini utumie muda na energy yako kupiga mikwara na makelele ukijua kabisa si njia utakayoitumia!!!!

kwa muda dunia ilipofikia ni ushamba kutishiana tishiana na mikwara isiyo na maana,vita au vurugu sio chaguo sahihi.

tunamheshimu china huyu anayemaliza matatizo mezani kuliko huyo anayebweka bweka bila vitendo.
 
Gharama ya heshima ni kubwa sana!! Ni nchi chache sana zinazoweza kulipa gharama hiyo!! Kwa mfano, inajulikana wazi kuwa China inaiunga mkono Urusi kwenye mgogoro wa ukraine, lakini haiwezi kuthubutu kupiga kura UN kupinga azimio la kuilaani Urusi na itaishia KUTOKUPIGA KURA! Lakini Korea ya kaskazini haipepesi macho bali inapiga kura tena ya wazi kupinga azimio lolote la kuilaani urusi!! China ni rafiki mwoga kwenye ugomvi atakukimbia!!
Mkuu mataifa makubwa mfano China haya endeshwi hivyo unavyodhani wewe, lazima yangalie interest zao kwanza kama taifa ndio kina fuata kitu kingine .

Kuliendesha taifa kubwa kama China lenye watu zaidi ya 1.5bln unahitaji chama imara kilicho jaa watu wenye akili wenye kuchukua maamuzi ya akili kwa manufaa ya taifa na sio mihemko. narudia tena mkuu hawa watu top elite mpaka wamefikia hapo juu kuwa top 7 elite wa CPC na PRC na wanajua wanacho kifanya wanazijua siasa za kimataifa ndani nje kuliko mimi na wewe mkuu.
1_660_111612013543.jpg

00221917e13e120fcb771c.jpg

: Mkuu jambo pekee tunapaswa kufahamu ni kuwa China ni taifa kubwa lazima lifanye maamuzi makubwa kwa faida ya taifa lake na sio maamuzi mabovu yatakayo lididimiza taifa lao.
 
kama una uwezo wa kumaliza migogoro yako kwa njia bora kabisa ya kidiplomasia kwanini utumie muda na energy yako kupiga mikwara na makelele ukijua kabisa si njia utakayoitumia!!!!

kwa muda dunia ilipofikia ni ushamba kutishiana tishiana na mikwara isiyo na maana,vita au vurugu sio chaguo sahihi.

tunamheshimu china huyu anayemaliza matatizo mezani kuliko huyo anayebweka bweka bila vitendo.
Wewe ulitaka China ifanye nini ?
 
Kulikuwa hakuna umuhimu wowote wewe kuandika hiki ulichoandika hapa.

Mwaka gani mgogoro umeanza kuufatilia ? sio hiki ulichoandika sija uliza ulicho jibu.

Mkuu sikuhitaji haya maelezo, ungejibu swali tu.

: Mkuu turudi kwenye swali nililo kuuliza
Jibu umelipata nimefuatilia mgogoro huu tangia chimbuko lake!! Ulianzia kwenye vita vya wenyewe kwa wenyewe mara tu baada ya vita kuu ya pili!! Naweza kutoa mhadhara kuhusu mgogoro huu! Nimeufuatilia tangu nikiwa shule ya msingi kupitia redio (dudu proof National 277), na magazeti! Enzi hizo hakuna simu za mkononi, internet wala mitandao ya kijamii!!
 
Jibu umelipata nimefuatilia mgogoro huu tangia chimbuko lake!! Ulianzia kwenye vita vya wenyewe kwa wenyewe mara tu baada ya vita kuu ya pili!! Naweza kutoa mhadhara kuhusu mgogoro huu!
Kwanza kosa lako la kwanza mkuu ni wewe kushindwa kunitajia huo mwaka ambao umeanza kuufatilia huu mgogoro baina ya PRC na ROC .

Kosa la pili ni kusema kuwa mgogoro huu chimbuko lake ni ulianza baada ya vita vya pili vya dunia kitu ambacho sicho.

: Kuwa tu mkweli mkuu huu mgogoro umeanza kuufatilia mwaka gani ? ukweli humuweka mtu huru
 
Pole!! Just read between the lines if you are so interested!! Usijiaibishe!! Vita vya wenyewe kwa wenyewe huko china kati ya majeshi ya wakomunist chini ya Mao na Nationalists wa china vilikuwa toka 1945 hadi 1949 na hao Nationalists waliokuwa wanajiita PRC (Peoples republic of China) walishindwa vita wakakimbilia kisiwani Taiwan na hadi leo wanajiita rasmi kama PRC!! Watoto iweni na adabu!!
 
Ikubali yaishe kuitangazia Taiwan uhuru wake mambo yaishe au iamue kutekeleza vitisho vyake vya kuirudisha Taiwan kwa nguvu!! Ichague moja kuliko kujidhalilisha kwa kubweka huku dunia nzima imegundua meno hamna!
1. Mkuu unafahamu PRC imependekeza njia zipi na zipi kuhusu huu mgogoro wake na ROC ?
2. Kwani katiba ya ROC inasema nini kuhusu China ?

3. Unafahamu swala la One Country two systems ?

4. Unafahamu makubaliano ya UN ya 1971 ?

: Mkuu kuongoza taifa kubwa kama China inahitajika akili nyingi zaidi na sio mihemko.
 
Huko kote si sehemu ya mada au uzi huu!! Ukitaka hayo yote anzisha uzi mwingine tutakuja kuchangia!! Huu uzi unabainisha tu kuwa china kajibainisha kama "paper tiger" na kila leo nchi za mabeberu wanamchezea na kumwaibisha!! Ametishia nyau mara lukuki na mabeberu yamevuka mstari wake mwekundu na hafanyi kitu!! Mara mia akatunza heshima yake kwa kukubali moja analoona ni jepesi kwake!!
 
Kulikuwa hakuna umuhimu wowote wewe kuandika hiki ulichoandika hapa.

Mwaka gani mgogoro umeanza kuufatilia ? sio hiki ulichoandika sija uliza ulicho jibu.

Mkuu sikuhitaji haya maelezo, ungejibu swali tu.

: Mkuu turudi kwenye swali nililo kuuliza
sorry ww ni mbishi ebu mpe heshima yake halaf ndo uweke nondo zako ili tuamin huyo chifu hapo kuna madini hajapata bahat kuyafaham
 
Back
Top Bottom