China kajipambanua kama chui wa karatasi: Hapa bongo tunasema ni "nyoka wa kibisa"

Nilichopinga ni kutuletea baraza la maamuzi la China kana kwamba urusi putin ndo aliamua kuvamia
Kwani mkuu huu mgogoro tunao uzungumzia hapa tuna ufananisha na wa Russia na Ukraine ?

: Mimi nime zungumzia pulitburo ya PRC na wala sijai husisha na Russia na pia sijasema kuwa maamuzi ya Russia juu ya Ukraine yamefanywa na Putin peke yake.
 
Ukitaka kujua ukatili wa china waulize India kule mipakani au Pakistan.

Mchina kama mbongo tu hapendi vita kabisa ila akiamu vita ni hatari

USSR
 
Tuliwahi kusema humu toka vita ya Ukraine na Russia inaanza, tukasema China atakaa mbali kabisa na Russia sababu hawezi kugombana na watu ambao wamemfanya awe tajiri namna hii.

Hilo la kwanza, la pili. Ubabe usiokuwa na maana kama wa Russia umeshapitwa na wakati, China amestaarabika mno.
 
Kwa taarifa yako mimi nakimbilia miaka 70!! Mgogoro huu ninaujua toka vita vyao vya wenyewe kwa wenyewe enzi ya Mao!! Hao walioko Taiwan walishindwa vita wakakimbilia kisiwa cha Taiwan!! Kubali tu kunipa shikamooo!!
Hiyo hata wa shule wanajua ipo kwenye vitabu dogo wewe

USSR
 
Ndio china hana Sera ya vita yupo kimkakati wa biashara zaidi,anajua anapotoka

USSR
 
Ndio china hana Sera ya vita yupo kimkakati wa biashara zaidi,anajua anapotoka

USSR
Kama hivyo ndivyo, anapiga makelele ya nini? analalamika nini? ukishajua wewe ni nyumba ya udongo hauhimili vishindo inabidi uwe mpole!!
Yeye angekubali tu kuiachia uhuru Taiwan aendeleze biashara zake na mabeberu! Tatizo mabeberu wakikugundua wewe mwoga wanakunyanyasa sana! Ila hana jinsi!
La pili China anategemea bidhaa za viwandani ambazo si za lazima kwa maisha ya kila sikuna zina mbadala tena ulio bora zaidi!! Biashara zake zikipigwa ban hapo hana ujanja! Tofauti na urusi ambayo ni tajiri wa mali asili ambazo ni za lazima kwa maisha ya kila siku na hazina mbadala! Mabeberu wanalazimika kutumia gesi na mafuta kila siku! Usipoyanunua moja kwa moja kwa mrusi, utayanunua kutoka kwa mtu wa tatu aliyeyanunua toka urusi, tena kwa bei juu zaidi!! Ndivyo ilivyotokea kwa ulaya magharibi!! Huwezi kuyatoa mafuta ya urusi kwenye soko la dunia na dunia ikabaki salama kwa sasa! Walitaka kufanya hivyo kwa kuitaka saudi arabia iongeze uzalishaji kufidia yale ya urusi, jibu likatoka kinyume chake! Saudia na OPEC+ wameamua kupunguza uzalishaji!! Marekani wakanuna lakini wakaambiwa nuna sana!!
 
Naungana na mleta mada katika hili

Huyo mtetezi wa china anaesema China inaangalia faida zake kuliko hasara kuna jambo ana sahau

Kwanini sasa China alipiga mkwara wa kila rangi kama huo uwezo wa kurusha ngumi hana

Maana Pelosi aliambiwa maneno ya kila rangi na China hadi jeshi likawa linakaa tayari

Lakini mwisho wa siku akaishia kutulia tuli
Kama huwez ugomvi usitoe maneno ya shombo.
 
Binafsi China nilimdharau sana. Mikwara kibao vitendo hakuna. Angeongea tu mara moja alaf asubilie bibi atue amalize mchezo.

Kuna mtu aliwahi kusema jujwaani hapa kua nchi huru duniani ni Russia, N. Korea, Iran, Turkey, na China lkn China sio huru kama tulivyodhani. Inaendeshwa na US.
 
Anatoana jasho na wahindi huko mipakani...
 
Mchina anakwambia Kwa msemo wao local kwamba " all the great battles are won without fighting "
Kuna probability ndio Maana wanakuwa wakitembea nao huo usemi
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…