China kuendesha TAZARA kwa miaka 27, Uwekezaji wa dola bilioni 1.4 kuanza

Sioni jipya hata kidogo, si taarifa zinasema hiyo reli yenyewe ilijengwa na hao hao Wachina?

Kwahiyo wamekuja kuchukua reli yao bila shaka

Hakuna kitu Watanzania tunaweza kukifanya kiufasaha zaidi ya uchawa na majungu tu 🙌
 
Naskia WACHINA(CCeCc) walipojaribu kuchunguza reli ya Tazara na kukuta Haina viwango na ni chakavu yamkini Bado inatumika waliliaa sanaa hadi macho yakazidi kutumbukia ndani.

Nadhani wapewe tu ili wafufue TAZARA.
View attachment 3277446
Mkuu unakumbuka ya TRL na wahindi?

Hawa umewapima kuwa na uadilifu gani hadi kuwafurahia namna hiyo?

Tukianza kusema nchi hii imeuzwa, tunaonekana ni watu tunaopinga kila kitu.

Kiuhalisia kama tumeshindwa kuiendesha wenyewe, hao siyo wajomba zetu kusema watatuletea taafifu yoyote zaidi ya kujinufaisha wenyewe.
 
Mtu mweusi anachoweza kufanya sana ni mbinu na ghilba za kushinda uchaguzi, hakuna zaidi. Samia sasa hivi anahaha kweli kweli kufanya kila njia ili aweze kubakia kwenye madaraka baada ya 2025. Wangekuwa na juhudi za namna hii kwa mambo mengine Afrika ingefika mbali.
 
CHADEMA tukitwaa Madaraka tutapitia upya mikataba yote hii ikiwamo ya Bandari nk. Tukibaini kuna RUSHWA na UPIGAJI wale wote waliohusika wanakwenda Jela.

NO HATE NO FEAR ✌️
 
Kweli kabisa angalia hata daraja la Nyerere la kwenda kigamboni kipindi tunakabidhiwa lilikua usiku linawaka taa mbalimbali za urembo safi kabisa. Leo taa zimeungua tumeshindwa kurudishia sijui tunaweza nini.
Kipaumbele kwa sasa ni kumsifia Mama hayo mengine kama kubadilisha taa zilizoungua kuziongelea tu utaambiwa una chuki au utaambiwa ni Mdini.
 
Mkuu Tazara haikua hivi, tuliachiwa ikiwa ni kibuyu Cha asali ila tumeshindwa kuendesha na baadhi ya Mali za taraza zime binafsishwa kwa manufaa ya vingunge, ajira nyingi na biashara nyingi zmepotea zilizotegemea Tazara, Hii inadhihirisha hata iweje hatuwezi kuifufua Bora waje tu hao wachina.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…