China kuisaidia Tanzania ujenzi wa SGR na mradi wa umeme Mto Rufiji

China kuisaidia Tanzania ujenzi wa SGR na mradi wa umeme Mto Rufiji

Miss Zomboko

JF-Expert Member
Joined
May 18, 2014
Posts
4,599
Reaction score
9,532
China imesema itaangalia namna ya kushirikiana na Tanzania katika utekelezaji wa miradi mikubwa ya kimkakati ikiwemo reli ya kati kwa kiwango cha kisasa (standard gauge railway) na bwawa la kuzalisha megawati 2,115 za umeme katika mto Rufiji (Bwawa la Mwl. Nyerere).

Hayo yamesemwa na Rais wa China, Xi Jinping alipompigia simu Rais wa Tanzania, Dkt. Magufuli ambapo viongozi hao wamezungumzia kuimarisha zaidi uhusiano na ushirikiano hususani katika masuala ya uchumi.

Katika mazungumzo hayo yaliyodumu kwa muda wa saa moja, Rais Xi Jinping amempongeza Rais Magufuli kwa kuchaguliwa tena na kwamba anaiona Tanzania kuwa nchi itakayoongoza kwa ukuaji wa uchumi barani Afrika.

Kwa upande wake Rais Magufuli amemhakikishia Rais Xi Jinping kuwa Tanzania itaendeleza na kukuza zaidi uhusiano wake na China uliodumu kwa takribani miaka 55 baada ya kuasisiwa na Baba wa Taifa Hayati Mwl. Julius Kambarage Nyerere na Hayati Mwenyekiti Mao Zedong, na kwamba Tanzania itaendelea kuiunga mkono China katika masuala mbalimbali ya kimataifa.

Rais Magufuli ameiomba China kushirikiana na Tanzania katika uwekezaji wa miradi mikubwa kwa kutoa mikopo nafuu na ameitaja baadhi ya miradi hiyo kuwa ni wa kuzalisha megawati 358 za umeme katika mto Ruhudji, Megawati 222 za umeme katika mto Rumakali na ujenzi wa barabara visiwani Zanzibar.

Halikadhalika, Dkt. Magufuli ameiomba China kufungua zaidi masoko ya bidhaa mbalimbali kutoka Tanzania hususani mazao mbalimbali ya kilimo.

Rais Xi Jinping ameahidi kufanyia kazi maombi yaliyotolewa na Rais Magufuli ikiwemo ujenzi wa miradi ya kuzalisha umeme ya Ruhudji na Rumakali, ujenzi wa reli, Bwawa la Nyerere na ununuzi wa mazao ya Tanzania.
 
CHINA siyo mabeberu kwa mujibu wa MATAGA.

Na fedha toka china "NI ZETU ZA NDANI" kwa mujibu wa MATAGA.

Na "china Wanatupa fedha zetu bure" kwa mujibu wa MATAGA.

CHINA ,IN RETURN "HATUWAPI MAKAA YA MAWE, MIGODI WALA MALIASILI " ILI KUNUFAIKA NA MKOPO WENYE MASHARTI MAGUMU WALIOTUPA KUJENGA SGR na STIGLERS.

MAREKANI NA UINGEREZA hawajagoma kutupa fedha za ujenzi huo kwa mujibu wa MATAGA ila tumeamua kuchukua CHINI kwakuwa wao NDIO MARAFIKI WA KWELI.

Haijawa kutokea na haitakaa itokee Tanzania kupata raisi mzalendo kama
 
Hayo ni mambo mazuri na muhimu yaliyojadiliwa na hao viongozi.

Lakini isiwe ndiyo iwe sababu ya kuwanyima wananchi wa nchi hii kuamua mambo yao kwa uhuru na haki.

Wasitutawale kwa mgongo wa CCM, ambayo ndiyo kibaraka wao wanayemtumia.

China wasiingilie uhuru wetu wa kuchagua viongozi, vyama na mifumo yetu ya maendeleo. Wasiwatumie viongozi wanaotumia mabavu kufanya lolote wanalotaka kufanya hata kama kufanya hivyo kutawaumiza wananchi.

Wasikubali kutumiwa na watawala kulazimisha wabaki madarakan kwa hila au kwa nguvu, hata kama watu hawawataki.

Wasiifanye CCM ndiyo iwe kama chama chao cha kikomunisti, ambacho ndiyo kinachoamua kila kitu kinachofanyika China.
 
WACHINA! Wawekezaji? Waulize Wazambia - airport wamechukua wanakusanya mapato wao yaani ni mali yao hadi walipe senti ya mwisho! Waulize Kenya! Mombasa-Nairobi standard gauge railway wamechukua wanakusanya mapato wao. Hadi wauza chai ni Wachina! Mchina hana dini wala demokrasia! Tegemeeni ukoloni mkorofi na wa kishenzi kuliko wazungu!
 
Wachina twende nao kwa umakini mkubwa sidhani kama wana dini hawa!

Bora umetoa hilo angalizo, ifahamike muda mfupi kabla ya Kikwete kumaliza muda wake madarakani, aliingia mikataba 16 ya siri na serikali ya China, walichopatana wanajua wenyewe.

Nikiangalia kiwango cha pesa cha miradi miwili ya SGR & SG, inahitaji si chini ya 10t kukamilika. Sioni ni wapi Magu anapata hela hizo ndani ya 5yrs, kwa vyovyote vile atajilipua kwenye fedha za Wachina, maana anasimimiwa na bunge kibogoyo. Yajayo yatafurahisha.
 
Back
Top Bottom