China kuisaidia Tanzania ujenzi wa SGR na mradi wa umeme Mto Rufiji

China kuisaidia Tanzania ujenzi wa SGR na mradi wa umeme Mto Rufiji

Ila mbona miaka ya nyuma walikuwa washirika wazuri tu, mfano kwenye Reli ya Tazara (tunaweza tukaanzia kwa uzoefu huo wa TAZARA kuleta SGR) na pia kiwanda cha Urafiki na vitu vingine. Wakati mwingine hata sie huwa ni watu wa ovyo pia kwa kusainin mikataba bila kuangalia maslahi ya nchi kwa kuwa kama kuna vipengele haviendani vinatakiwa vijadiliwe. Sie tunajua ku-bargain ina apply kwenye fedha tu kwa kuomba punguzo kumbe hata kwenye contract pia kuondoa baadhi ya masharti)
Hapa umekonga moyo wangu. Ila dunia au mfumo wa dunia wa sasa umekaa kimasalahi zaidi. China ya 1960 sio hii, inayovutana na Marekani.
 
Jibu swali - umewahi kukutana au kufanya kazi na Wachina katika mazingira gani - labda tuanzie hapo - wewe unajua Mataifa ya Ulaya na Amerika uwachukulia vipi Wafrika, je, imani/maoni yao kutuhusu sisi yana ukweli gani? Narudia kuwakumbusheni kwamba Wachina wachache wenye akili fyatu kisiwe kisingizio cha kuwachukulia kwamba Wachina wote wako hivyo, mimi ndio maoni yangu, sioni kama nimeku-offend popote kutokana na maoni yangu, kama nimekukwaza samahani.
Mkuu upo sawa, huenda mie ndio nimekosea sehemu. Upo sahihi. Ila kumbuka mfumo wa dunia 1960 sio sawa na sasa. Mie nimefanya kazi kama partners na hao watu. Kwa sehemu nawajua sio wachina wote wabaya, ila agenda zao kama mtu hatokuwa makini ameisha. Sie kama taifa tuwe macho hapo. Kama tutakuwa makini itakuwa 50/50
 
Back
Top Bottom