China kuisaidia Tanzania ujenzi wa SGR na mradi wa umeme Mto Rufiji

China kuisaidia Tanzania ujenzi wa SGR na mradi wa umeme Mto Rufiji

Kabisa ! Yaani ikibidi ni mwendo wa hela za bandia kwa cheni feki ! Hilo JPM yuko makini sana !!!! Wachina wajipange, hakuna cha kuvishana mikenge hapa !!
Njaa haina baunsa wewe unataka msaada halafu uje na masharti? Masharti ni ya mchina maana hela za ndani zimeisha.
 
China imesema itaangalia namna ya kushirikiana na Tanzania katika utekelezaji wa miradi mikubwa ya kimkakati ikiwemo reli ya kati kwa kiwango cha kisasa (standard gauge railway) na bwawa la kuzalisha megawati 2,115 za umeme katika mto Rufiji (Bwawa la Mwl. Nyerere).

Hayo yamesemwa na Rais wa China, Xi Jinping alipompigia simu Rais wa Tanzania, Dkt. Magufuli ambapo viongozi hao wamezungumzia kuimarisha zaidi uhusiano na ushirikiano hususani katika masuala ya uchumi.

Katika mazungumzo hayo yaliyodumu kwa muda wa saa moja, Rais Xi Jinping amempongeza Rais Magufuli kwa kuchaguliwa tena na kwamba anaiona Tanzania kuwa nchi itakayoongoza kwa ukuaji wa uchumi barani Afrika.

Kwa upande wake Rais Magufuli amemhakikishia Rais Xi Jinping kuwa Tanzania itaendeleza na kukuza zaidi uhusiano wake na China uliodumu kwa takribani miaka 55 baada ya kuasisiwa na Baba wa Taifa Hayati Mwl. Julius Kambarage Nyerere na Hayati Mwenyekiti Mao Zedong, na kwamba Tanzania itaendelea kuiunga mkono China katika masuala mbalimbali ya kimataifa.

Rais Magufuli ameiomba China kushirikiana na Tanzania katika uwekezaji wa miradi mikubwa kwa kutoa mikopo nafuu na ameitaja baadhi ya miradi hiyo kuwa ni wa kuzalisha megawati 358 za umeme katika mto Ruhudji, Megawati 222 za umeme katika mto Rumakali na ujenzi wa barabara visiwani Zanzibar.

Halikadhalika, Dkt. Magufuli ameiomba China kufungua zaidi masoko ya bidhaa mbalimbali kutoka Tanzania hususani mazao mbalimbali ya kilimo.

Rais Xi Jinping ameahidi kufanyia kazi maombi yaliyotolewa na Rais Magufuli ikiwemo ujenzi wa miradi ya kuzalisha umeme ya Ruhudji na Rumakali, ujenzi wa reli, Bwawa la Nyerere na ununuzi wa mazao ya Tanzania.
pesa zimebana😂 “ tutatumia pesa ya ndani”. Magufuli atauza bandari yetu kwa miaka 100😂
 
Wachina twende nao kwa umakini mkubwa sidhani kama wana dini hawa!

Mkuu nimekupa [emoji106]
Twende nao kwa umakini sana ila kiukweli hatuwafikii jwa kufikiri....
Wachina wanataka Bandari ya Bagamoyo kwa udi na Uvumba?
Wanataka wapi watapata watapiga rasilimali.....
Hata hiyo Miradi wanaweza kukupa Mikopo au mikataba ili wao waendeshe halafu baada ya muda fulani wakisharudisha chao ndo wakupe Miradi yao....
Wachina ni wajanja sana tena kuliko hata Wazungu aisee!
Mzungu yuko Straight forward mchina janja janja nyingi anaweza kukuingiza kingi!
Ukashangaa anaondoka na Rasilimali au unaingia mkataba wa muda mrefu na faida kwake na sio 50/50!
 
The Chinese now know we’re desperate. They will surely make us play on their terms. This is getting interesting!
 
WACHINA!!! Wawekezaji? Waulize wazambia - airport wamechukua wanakusanya mapato wao yaani ni mali yao hadi walipe senti ya mwisho!! Waulize Kenya! Mombasa-

Nairobi standard gauge railway wamechukua wanakusanya mapato wao. Hadi wauza chai ni wachina!! Mchina hana dini wala demokrasia! Tegemeeni ukoloni mkorofi na wa kishenzi kuliko wazungu!

Yaani hapo wana port ya Mombasa. Unganisha na SGR ya Bongo. Wanakua wamemaliza kazi.
 
China imesema itaangalia namna ya kushirikiana na Tanzania katika utekelezaji wa miradi mikubwa ya kimkakati ikiwemo reli ya kati kwa kiwango cha kisasa (standard gauge railway) na bwawa la kuzalisha megawati 2,115 za umeme katika mto Rufiji (Bwawa la Mwl. Nyerere).

Hayo yamesemwa na Rais wa China, Xi Jinping alipompigia simu Rais wa Tanzania, Dkt. Magufuli ambapo viongozi hao wamezungumzia kuimarisha zaidi uhusiano na ushirikiano hususani katika masuala ya uchumi.

Katika mazungumzo hayo yaliyodumu kwa muda wa saa moja, Rais Xi Jinping amempongeza Rais Magufuli kwa kuchaguliwa tena na kwamba anaiona Tanzania kuwa nchi itakayoongoza kwa ukuaji wa uchumi barani Afrika.

Kwa upande wake Rais Magufuli amemhakikishia Rais Xi Jinping kuwa Tanzania itaendeleza na kukuza zaidi uhusiano wake na China uliodumu kwa takribani miaka 55 baada ya kuasisiwa na Baba wa Taifa Hayati Mwl. Julius Kambarage Nyerere na Hayati Mwenyekiti Mao Zedong, na kwamba Tanzania itaendelea kuiunga mkono China katika masuala mbalimbali ya kimataifa.

Rais Magufuli ameiomba China kushirikiana na Tanzania katika uwekezaji wa miradi mikubwa kwa kutoa mikopo nafuu na ameitaja baadhi ya miradi hiyo kuwa ni wa kuzalisha megawati 358 za umeme katika mto Ruhudji, Megawati 222 za umeme katika mto Rumakali na ujenzi wa barabara visiwani Zanzibar.

Halikadhalika, Dkt. Magufuli ameiomba China kufungua zaidi masoko ya bidhaa mbalimbali kutoka Tanzania hususani mazao mbalimbali ya kilimo.

Rais Xi Jinping ameahidi kufanyia kazi maombi yaliyotolewa na Rais Magufuli ikiwemo ujenzi wa miradi ya kuzalisha umeme ya Ruhudji na Rumakali, ujenzi wa reli, Bwawa la Nyerere na ununuzi wa mazao ya Tanzania.
THITHI NI MATAJIRIII , DONA KANTREEE!! TUNAJENGA KWA FEZWA ZWETU WENYEWE!!
 
Wachina twende nao kwa umakini mkubwa sidhani kama wana dini hawa!

Wewe unaongelea ya zambia mbali huko?uliza gesi ya mtwara inaenda wapi!!

Mkuu fafanua acha kutulisha Matango pori wakati kila siku kwenye TV TBC tunaona umeme unaozalishwa na Gesi ya Mtwara kutoka Mtwara na bomba hadi Dar es salaam Kinyerezi!
Au Kuna Bomba Linaenda China?
Au Inasindikwa na Meli kwenda china?
Na tunaambiwa Umeme zaidi ya 50%ni wa Gesi
Na tunaona wewe hebu tupe data hapa si hadithi za Alinacha @Cap Tamar
 
Wachina twende nao kwa umakini mkubwa sidhani kama wana dini hawa!

Mkuu ni Kweli kumbuka wanatamani Sana Bandari ya bagamoyo hawa watu!
Ni janja janja mnooo... Mchina ni mjanja kuliko hata Mzungu aisee... Anaweza kukuingiza mkataba ukajikuta anaendesha hiyo miradi yeye mpaka apate faida ndo akupe na mateso kwa watu wako juu unaweza laaniwa ujue. Huyu anaitwa Mchina...[emoji3][emoji3]
 
Hivi dunia hii ya leo, nchi ngapi zimesaidiwa na China? Jirani yake Korea Kaskazini kashindwa kumsaidia, Venezuela ilisaini mikataba mingi na China lakini mpaka leo hali ngumu kule, Cuba, Sudan, Zimbabwe, na nchi zingine za Afrika hali ni ile ile. Linganisha na nchi zilizosaidiwa kiuchumi na Marekani kama Ujerumani, Austria, UK, Japan, Korea Kusini, Phillipines, na nchi zingine za Ulaya magharibi ambazo ziko mbali kiuchumi.
 
Back
Top Bottom