China kuisaidia Tanzania ujenzi wa SGR na mradi wa umeme Mto Rufiji

China kuisaidia Tanzania ujenzi wa SGR na mradi wa umeme Mto Rufiji

Mkuu sasa hivi naamini SGR itakamilika baada ya fedha za ndani kushindwa kufua dafu na mchina kuamua kuingilia kati!
Hahaha ni majibu ya hisia za mtu mshindwa mmoja kutoka Ufipa!

Kwani China alijua saa ngapi kwamba tumeshindwa kujenga huo mradi wa umeme ndipo akampigia simu Rais John Magufuli.
 
Sharti kubwa laweza kuwa ni kuuza nyama ya punda na mbwa.
Hili sharti lina ugumu gani mkuu? Mbona ni kama fursa nzuri sana.
Yajayo yatafurahisha.
Sidhani.
Huenda unamaana ya kinyume chake.

Hawa watu wanajua wanaweza kufanya chochote na wasihojiwe na yeyote yule. Hii ndiyo sababu tutaendelea kukandamizwa na serikali za CCM zitakazofuata, ikiwa ni kulinda maslahi ya hawa watu.

Huyu sasa anamlindia siri zake aliyemtangulia, na kama atatoka, huyo atakayewekwa kazi yake ya kwanza ni kufunika maovu yote waliyofanya watangulizi wake.

Hali hii ni lazima iondolewe kwa kuiondoa CCM.
 
Hahaaa!! Ni majibu ya hisia za mtu mshindwa mmoja kutoka Ufipa!!

Kwani China alijua saa ngapi kwamba tumeshindwa kujenga huo mradi wa umeme ndipo akampigia cm Raisi JPM
Kwani wewe umejua vipi kuwa ile kupigiana simu haikuwa ni official tu?Inawezekana walishasimuliana huko jinsi fedha za ndani zilivyoshindwa kufua dafu na jana wakakubaliana kuwa wapigiane simu officially kuweka mambo hadharani!
 
Kumrudia Mchina tena ili atusaidie kujenga SGR ni kula matapishi yetu. Magufuli alipoingia madarakani alikuta mazungumzo yetu na China yameiva.

China ilikuwa tayari kutoa mkopo wa bei nafuu kujenga SGR kupitia China Exim bank ambao tungeulipa ndani ya miaka 20, yeye akaja akapanguapangua na kuwaleta Waturuki instead, lakini waturuki hawana hela kama Wachina. Matokeo yake 5 years later tumerudi square one, tumemrudia Mchina atusaidie, Sasa sijui safari hii atakuja na terms zipi.
 
Yajayo yatatufurahisha..tushangilie tu kwa Sasa.
 
Back
Top Bottom