China kuisaidia Tanzania ujenzi wa SGR na mradi wa umeme Mto Rufiji

China kuisaidia Tanzania ujenzi wa SGR na mradi wa umeme Mto Rufiji

Kumrudia mchina tena ili atusaidie kujenga SGR ni kula matapishi yetu. Magufuli alipoingia madarakani alikuta mazungumzo yetu na China yameiva, China ilikuwa tayari kutoa mkopo wa bei nafuu kujenga SGR kupitia China Exim bank ambao tungeulipa ndani ya miaka 20, yeye akaja akapanguapangua na kuwaleta waturuki instead, lakini waturuki hawana hela kama wachina. Matokeo yake 5 years later tumerudi square one, tumemrudia Mchina atusaidie, Sasa sijui safari hii atakuja na terms zipi!.
Lazima aje na terms NGUMU kuliko za mwanzo. Wale si walitakiwa wasibugudhiwe kwa miaka 100, sasa itaenda kuwa LIFE TIME
 
Hao wachina wamewavuruga wakenya na ile SGR yao sasa wakenya hawana hamu nayo, naona na sisi ndio tunaelekea huko.

Jidanganyeni tu na wimbo wenu wa "rafiki zenu" wachina.
Kenya hii hii mnayosema ina uchumi bora hapa EAC na ina Rais bora kuliko wote hapa EAC?
 
WACHINA!!! wawekezaji? waulize wazambia - airport wamechukua wanakusanya mapato wao yaani ni mali yao hadi walipe senti ya mwisho!! Waulize Kenya! Mombasa-

Nairobi standard gauge railway wamechukua wanakusanya mapato wao. Hadi wauza chai ni wachina!! Mchina hana dini wala demokrasia! Tegemeeni ukoloni mkorofi na wa kishenzi kuliko wazungu!
Wewe unaongelea ya Zambia mbali huko? Uliza gesi ya mtwara inaenda wapi.
 
Wachina twende nao kwa umakini mkubwa sidhani kama wana dini hawa!
Wana dini 😁, dini si lazima ziwe hizi za Wazungu na Waarabu, Wachina wana dini zao nzuri tu.

Ile reli wangeanza nayo Wachina, saa hizi tungeshasahau kusafiri kwa mabasi. Kwa upande wa miundombinu Mchina hapa duniani hana mshindani, labda tukihamia paradiso ndo atapata mshindani.
 
Wale tunaowaita mabeberu wana nafuu kubwa kuliko Mchina. Mchina ni mshenzi zaidi tumewasikia mara nyingi hapa Afrika wanafanya kila aina ya uwekezaji wa kijinga kabisa.

MIRADI hii mikubwa ilitakiwa iende na PPP. Ni mahela mengi sana yanayokwenda huko ndio mana tunatakiwa kuwa makini sana na kauli hizi mara mabeberu mara hivi wakati hawa jamaa wako mbali sana kimaendeleo hatuwakuti hata miaka 300.

Tudeal nao kwa busara na uzalendo.
 
Serikali ya Tanzania iweke mazingira ya wananchi wake kuwa matajiri mambo yatakuwa mepesi sana. Nchi hujengwa na wananchi.
Laiti kama wanakusikia ndugu. Ukishakorofisha wafanyabiashara (kwa kuwaita wapigaji) jua kuna mambo mengi yatakwama. Kwa sasa saruji haishikiki, mafuta ya kula hayashikiki, sukari haishikiki, siku wakivuruga wafanya biashara wa mafuta (petroleum) basi ndio biashara imeishia hapo bro. Sekta binafsi ukishaivuruga, kila kitu kinavurugika. Sekta binafsi ndio mwajiri mkubwa mara kumi zaidi ya serikali.
 
Tafadhali wana ufipa habari hii haiwahusu kabsa. Mnaruhisiwa kuchangia habari za EU huko, hizi za rafiki yetu China, msizikodolee Macho.😁

Akufaaye kwa dhiki ndiye rafiki. Pesa za China ni za ndani. Za nje ni za mabeberu.

Karibu China. Karibu Tanzania
 
Back
Top Bottom