China kuisaidia Tanzania ujenzi wa SGR na mradi wa umeme Mto Rufiji

China kuisaidia Tanzania ujenzi wa SGR na mradi wa umeme Mto Rufiji

Laiti kama wanakusikia ndugu ukishakorofisha wafanyabiashara (kwa kuwaita wapigaji) jua kuna mambo mengi yatakwama. Kwa sasa saruji haishikiki, mafuta ya kula hayashikiki, sukari haishikiki, siku wakivuruga wafanya biashara wa mafuta (petroleum) basi ndio biashara imeishia hapo bro.
Fedha mtaani zikiwa vizuri serikali itafaidi sana. Serikali iangalie namna ya kuwafanya wananchi wake wawe matajiri. JPM hatojuta akifanya hili.
 
😀 😀 😀 😀 ama hujamwelewa mwenye nchi yake. Dona kantri isiyoweza kuongeza mishahara ya watumishi wake.
Isiyoweza Kutoa ajira, inayowafanya wananchi wake waishi kama mashetani. [emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
 
Kwa kilio kikuu hapo baadae... Mchina ana roho mbaya haijawahi tokea.... Wanaofanya kazi na Wachina wanajua haya
Ila China wanaweza kutuvusha toka uchumi wa kati hadi dona katre
 
Weee hilo mzee hataki, anataka tulimie meno ili tuishi kama mashetani.
Tukilimia meno hatutakuwa na uwezo wa kupanda ndege wala SGR haitakuwa na kazi na hilo analielewa maana Rais si mjinga. Tuombe Mungu hii miaka mitano alifanye hili. Tupunguze kumkashifu na kumponda pia.
 
China imesema itaangalia namna ya kushirikiana na Tanzania katika utekelezaji wa miradi mikubwa ya kimkakati ikiwemo reli ya kati kwa kiwango cha kisasa (standard gauge railway) na bwawa la kuzalisha megawati 2,115 za umeme katika mto Rufiji (Bwawa la Mwl. Nyerere).

Hayo yamesemwa na Rais wa China, Xi Jinping alipompigia simu Rais wa Tanzania, Dkt. Magufuli ambapo viongozi hao wamezungumzia kuimarisha zaidi uhusiano na ushirikiano hususani katika masuala ya uchumi.

Katika mazungumzo hayo yaliyodumu kwa muda wa saa moja, Rais Xi Jinping amempongeza Rais Magufuli kwa kuchaguliwa tena na kwamba anaiona Tanzania kuwa nchi itakayoongoza kwa ukuaji wa uchumi barani Afrika.

Kwa upande wake Rais Magufuli amemhakikishia Rais Xi Jinping kuwa Tanzania itaendeleza na kukuza zaidi uhusiano wake na China uliodumu kwa takribani miaka 55 baada ya kuasisiwa na Baba wa Taifa Hayati Mwl. Julius Kambarage Nyerere na Hayati Mwenyekiti Mao Zedong, na kwamba Tanzania itaendelea kuiunga mkono China katika masuala mbalimbali ya kimataifa.

Rais Magufuli ameiomba China kushirikiana na Tanzania katika uwekezaji wa miradi mikubwa kwa kutoa mikopo nafuu na ameitaja baadhi ya miradi hiyo kuwa ni wa kuzalisha megawati 358 za umeme katika mto Ruhudji, Megawati 222 za umeme katika mto Rumakali na ujenzi wa barabara visiwani Zanzibar.

Halikadhalika, Dkt. Magufuli ameiomba China kufungua zaidi masoko ya bidhaa mbalimbali kutoka Tanzania hususani mazao mbalimbali ya kilimo.

Rais Xi Jinping ameahidi kufanyia kazi maombi yaliyotolewa na Rais Magufuli ikiwemo ujenzi wa miradi ya kuzalisha umeme ya Ruhudji na Rumakali, ujenzi wa reli, Bwawa la Nyerere na ununuzi wa mazao ya Tanzania.
Natamani Tanzania tungekuwa tunarekodi na kuachia tapes za Marais wetu pale wanapostaafu kama wanavyofanya Marekani. Ningependa sana kusikiliza mazungumzo ya Nyerere, Magu na Mwinyi (Baba) na viongozi wa nchi nyingine.
 
Kwa kilio kikuu hapo baadae... Mchina ana roho mbaya haijawahi tokea... Wanaofanya kazi na wachina wajua haya

Huko Zambia sijui wamefanyaje! 😀 Yaani, ni kama mtu upo huna msaada halafu ndugu wanakugombania wakusaidie ila kumbe kila mmoja ana malengo na maslahi yake. Mwingine anataka uwe kibarua wake, mwingine ukae na wanaye, mara umlindie nyumba n.k.
 
Hii ni dalili kuwa hakuna hela ya kukamilisha hiyo miradi na sasa tunalazimika kutafuta fedha kutoka chanzo vingine wakiwemo wachina, watu ambao sio wema kabisa.Hiyo SGR itakuwa ni mali ya wachina pale tutaposhindwa kulipa deni na hiki ndio wachina wanachokitafuta.
 
Wachina twende nao kwa umakini mkubwa sidhani kama wana dini hawa!
China pia atafaidika na reli ya mpya ya SGR kwa kuwa inaunganisha China na vyanzo mbali mbali vya malighafi kutoka Congo, Rwanda, Burundi na Tanzania yenyewe na pia itatoa fursa kwa bidhaa nyingi za China kufika kwenye masoko kwa urahisi na kwa gharama nafuu. Mradi wa SGSR ni muhimu pia kwa uchumi wa China. Kikwete alishasema ukitaka KULIWA kubali na wewe ULIWE.
 
China imesema itaangalia namna ya kushirikiana na Tanzania katika utekelezaji wa miradi mikubwa ya kimkakati ikiwemo reli ya kati kwa kiwango cha kisasa (standard gauge railway) na bwawa la kuzalisha megawati 2,115 za umeme katika mto Rufiji (Bwawa la Mwl. Nyerere).

Hayo yamesemwa na Rais wa China, Xi Jinping alipompigia simu Rais wa Tanzania, Dkt. Magufuli ambapo viongozi hao wamezungumzia kuimarisha zaidi uhusiano na ushirikiano hususani katika masuala ya uchumi.

Katika mazungumzo hayo yaliyodumu kwa muda wa saa moja, Rais Xi Jinping amempongeza Rais Magufuli kwa kuchaguliwa tena na kwamba anaiona Tanzania kuwa nchi itakayoongoza kwa ukuaji wa uchumi barani Afrika.

Kwa upande wake Rais Magufuli amemhakikishia Rais Xi Jinping kuwa Tanzania itaendeleza na kukuza zaidi uhusiano wake na China uliodumu kwa takribani miaka 55 baada ya kuasisiwa na Baba wa Taifa Hayati Mwl. Julius Kambarage Nyerere na Hayati Mwenyekiti Mao Zedong, na kwamba Tanzania itaendelea kuiunga mkono China katika masuala mbalimbali ya kimataifa.

Rais Magufuli ameiomba China kushirikiana na Tanzania katika uwekezaji wa miradi mikubwa kwa kutoa mikopo nafuu na ameitaja baadhi ya miradi hiyo kuwa ni wa kuzalisha megawati 358 za umeme katika mto Ruhudji, Megawati 222 za umeme katika mto Rumakali na ujenzi wa barabara visiwani Zanzibar.

Halikadhalika, Dkt. Magufuli ameiomba China kufungua zaidi masoko ya bidhaa mbalimbali kutoka Tanzania hususani mazao mbalimbali ya kilimo.

Rais Xi Jinping ameahidi kufanyia kazi maombi yaliyotolewa na Rais Magufuli ikiwemo ujenzi wa miradi ya kuzalisha umeme ya Ruhudji na Rumakali, ujenzi wa reli, Bwawa la Nyerere na ununuzi wa mazao ya Tanzania.
Chagua who is the best Beberu Mzungu Vs Mchina and discuss.
 
Tanzania nchi ya ajabu sana china kuna soko la makaa ya mawe lakini hapo kwenye simu sidhani kama waliongelea 🙄
 
China Imecheza na "gape".

Biashara/siasa duniani ni sawa na biashara ya daladala...ukisusia root fulani wenzio wanaichangamkia.
Afrika ni sawa na mrembo fulani wa uhakika, jamaa mmoja akijifanya ana hasira halafu akasusa, muda huo huo wengine haraka sana wanaziba pengo.
 
Wachina twende nao kwa umakini mkubwa sidhani kama wana dini hawa!
Wenye dini ndio waliotuuza utumwani, walitukata mikono walifanya mauaji ya halaiki na waanzilishi wa vita zote kubwa duniani.
 
Back
Top Bottom