China imeanza ujenzi wa mfumo mpya wa rada utakaokuwa na uwezo wa kufuatilia kwa kina masuala ya anga za juu kwa lengo la kulinda vizuri Dunia.
Mfumo huo mpya pia utaongeza uwezo wa ulinzi wa nchi hiyo dhidi ya sayari ndogo zilizo karibu na Dunia, na uwezo wake wa kutathmini mfumo wa Dunia na mwezi.
Kituo hicho kinachojengwa katika Manispaa ya Chongqing, kusini magharibi mwa China kimepewa jina la China Fuyan, ikimaanisha mdudu mwenye macho mengi. Kwa mujibu wa rais wa Taasisi ya Teknolojia ya Beijing, Long Teng, timu ya watafiti wametoa jina hilo kutokana na mfumo wa rada kuhusisha antenna nyingi, sawa na mdudu mwenye macho mengi.