Mnada wa Mhunze
Senior Member
- Mar 1, 2023
- 168
- 819
Mwanadiplomasia mkuu wa China amesema chanzo kikuu cha msuguano katika uhusiano kati ya China na Marekani ni "mtazamo mbaya" wa Marekani kuhusu nchi yake.
Wang Yi alimwambia Blinken "hakuna nafasi ya majadiliano" juu ya Taiwan, kulingana na taarifa ya wizara ya mambo ya nje ya China baada ya mkutano huo.
Pia aliitaka Marekani kuondoa vikwazo vya upande mmoja dhidi ya China, "ikomeshe ukandamizaji" wa maendeleo ya sayansi na teknolojia ya China, na kutoingilia mambo ya ndani ya China.
"Lazima kuwe na chaguo kati ya majadiliano au makabiliano, ushirikiano au migogoro," amesema
BBC.