CHINA: Marekani iwajibike kwa kueneza UKIMWI Duniani na seasonal flue mwaka 2009 maana chimbuko la H1N1 na UKIMWI ni Marekani

CHINA: Marekani iwajibike kwa kueneza UKIMWI Duniani na seasonal flue mwaka 2009 maana chimbuko la H1N1 na UKIMWI ni Marekani

Haya boss. Miaka 70 hivi iliyopita mlikuwa mnawindwa kama nyani huko porini mkalime mashamba ya mzungu. Mwafrika msahaulifu sana.

😂😂😂 Mkuu inaonekana Historia ya Advance Uliifaulu Sana hasa . Yaani Una points ambazo ni Very Primitive.

Kwani mkuu mbona nyie wenyewe mlikuwa mnachukuana watumwa kabla hata Hao wazungu Kuja. Ule ni muendelezo tu.
 
Vijembe na maneno ya vigodoro, watuletee barakoa sisi za bure kama walivyotuleteaga ndomuz na ARV, na Feed the Future..

Tunaumia kiuchumi, nchi zetu hazina stimulus packages...mafahali wawili hawa wanaumiza nyasi...

Everyday is Saturday.................... 😎
 
Hawa wapuuzi wanatuona tunavyotaabika kwenye jambo alituhusu
 
Wanapo elekea watapatana... Kutetea maslahi yao, Ila tutakao umia ni sisi wananchi wa 3rd world country.

Ukimwi ulitengenezwa pia...! That's why kirusi cha Corona pia kimefanana na cha H.I.V kwa kiasi kikubwa na ikitokea imeundwa chanjo ya Corona itakuwa na Uhusiano wa karibu sana na ile ya Ukimwi ambayo kwa sasa haipo!

Swali ni kwamba Je, watakubali kuruhusu iundwe?... Tukijua ukweli kuwa H.I.V kunanchi inaingiza pesa nyingi kupitia hiyo... Directly and indirectly!

Je, Marekani imelipa hasara kutokana na majanga ya H1N1, UKIMWI na msukosuko wa fedha duniani?

Msemaji wa wizara ya mambo ya nje ya China Geng Shuang amesema, Marekani inapaswa kufahamu kuwa adui wao ni virusi, sio China, kwani kama nchi nyingine, China pia ni mwathirika wa maambukizi ya virusi vya Corona.

Geng amesema hayo baada ya Rais Donald Trump wa Marekani jana kusema China inapaswa kuwajibika kwa ueneaji wa virusi hivyo.

Geng amesema virusi ni adui wa binadamu wote, na vinaweza kutokea wakati wowote na mahali popote, na China ni mwaathirika wa virusi hivyo. Ameongeza kuwa, hakuna aliyeiwajibisha Marekani kwa majanga yaliyoanzia nchini humo kama mafua ya H1N1 yaliyotokea nchini Marekani mwaka 2009 na kuenea katika nchi 214 duniani, na kusababisha vifo vya watu laki mbili, na pia mgogoro wa kifedha uliotokea mwaka 2008 nchini Marekani na kusababisha hasara kubwa ya kiuchumi duniani, aidha ugonjwa wa UKIMWI pia ulitokea kwanza nchini Marekani.

Geng amesisitiza tena kuwa, kwa mshikamano na ushirikiano tu, ndio jumuiya ya kimataifa itashinda virusi vya Corona, ameitaka Marekani kuacha kuipaka matope China, na kujishughulisha vizuri zaidi na juhudi za kukabiliana na virusi hivyo.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mkuu Hivi hizi program za UKIMWI anazozifund US Hao wachina hawazioni? Naskia Arvs Ni Bure. Nani anafund? Ni US. Atleast they are trying to correct their mistake not to run away from it.

China has to pay and she has to pay dearly. Kwa kupika takwimu na kuchelewa kutoa tahadhari kwa nchi nyingine kuhusu Corona. Yaani walipe for every life that has been lost na wakikataa hakuna kuwalipa loans zao walizokopesha Mataifa mengine na ikibidi they should be isolated by the international community.

Those communists will try to do a cover up lakini naamini joint investigation itawaumbua.Yaaani wafanyiwe kama alichofanyiwa Germany baada ya Kulost World War 1. Racists China.

Yes Keyboard Warrior.
Us wanajifanya wanafund lakini unajua kwa faida gani?... Ili iwe rahisi kukuwekea vikwazo ukishindwa kuendana na Sera zao.

Lakini wangeamua kutengeneza chanjo miaka ishapita 40 now, wangekuwa washapata kama kweli walikuwa na nia ya kutusaidia.

Dozi ya A.R.V ni gharama sana kiasi kwamba wakisema waache kudhamini ni wengi watakufa... Ndo maana nasema kirusi walitengeneza wao kwa faida yao!

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Watasema mengi lakini maumivu ya Leo yanafanana na vita baridi vikuu 1,duniani

Sijui rtusubiri wengine wapate nguvu
 
Inakuwaje miaka kumi nyuma tetesi la janga la China kupigwa na Mafua lilijulikana?

Inakuwaje Mtumishi wa Umma wa Marekani, Dr Faucci, anafadhili 'uimarishaji' wa virusi vya 'corona' kwa fedha za umma na hali serikali yake ishaondoa baraka za utafiti wa mwelekeo huo?

Faucci huyo huyo ahusikaye na kashfa za nyingine za mtindo huo katika virusi vya 'Ebola'...

Faucci huyo huyo kutoka siku za zamani, mwanzoni mwa miaka ya 80 alipigia chepuo uhusiano kati ya HIV na AIDS kwa mashauri yanayogubikwa na utata wa Kisayansi na utaalam akishirikiana na watafiti waliojaa hila--akina Gallo?

Sasa hivi, akipigia chepuo mkondo wa 'Chanjo' kuliko tiba na matibabu ambayo wataalam wengi duniani aidha kwa hofu ya kunyang'anywa leseni, kunyooshewa vidole ama kutengwa--wanakaa kimya ama kunung'unika chini kwa chini jinsi balaa hili la COVID19 Litavyopelekeshwa kimataifa--hali wakitambua dosari kadha wa kadha juu ya namna ya kushughulikia adha za matatizo ya kupumua katika hali ya dharula na ukweli kuhusu 'virusi' na 'tiba lishe' na 'matumizi ya vitamini c' kwa wingi ili kutibu maradhi haya na yale yote mengine ya sura hii?

Adjustments.JPG
 
Kabla wamarekani hawajamchagua Trump, aliekua Raisi wa Zimbabwe comrade Mugabe alionya kua Kama wamarekani watakua wendawazimu na kumchagua Trump kua Raisi basi angeleta vita ya tatu ya Dunia.

RIP comrade Mugabe
 
Je, Marekani imelipa hasara kutokana na majanga ya H1N1, UKIMWI na msukosuko wa fedha duniani?

Msemaji wa wizara ya mambo ya nje ya China Geng Shuang amesema, Marekani inapaswa kufahamu kuwa adui wao ni virusi, sio China, kwani kama nchi nyingine, China pia ni mwathirika wa maambukizi ya virusi vya Corona.

Geng amesema hayo baada ya Rais Donald Trump wa Marekani jana kusema China inapaswa kuwajibika kwa ueneaji wa virusi hivyo.

Geng amesema virusi ni adui wa binadamu wote, na vinaweza kutokea wakati wowote na mahali popote, na China ni mwaathirika wa virusi hivyo. Ameongeza kuwa, hakuna aliyeiwajibisha Marekani kwa majanga yaliyoanzia nchini humo kama mafua ya H1N1 yaliyotokea nchini Marekani mwaka 2009 na kuenea katika nchi 214 duniani, na kusababisha vifo vya watu laki mbili, na pia mgogoro wa kifedha uliotokea mwaka 2008 nchini Marekani na kusababisha hasara kubwa ya kiuchumi duniani, aidha ugonjwa wa UKIMWI pia ulitokea kwanza nchini Marekani.

Geng amesisitiza tena kuwa, kwa mshikamano na ushirikiano tu, ndio jumuiya ya kimataifa itashinda virusi vya Corona, ameitaka Marekani kuacha kuipaka matope China, na kujishughulisha vizuri zaidi na juhudi za kukabiliana na virusi hivyo.
So China wanamaanisha ni kweli wanahusika na kusambza corona virus na ndiyo sababu wamekuwa wakwanza kutoa misaada kwa nchi za Africa,siyo?
 
Back
Top Bottom