China na Russia kamwe hawawezi kutumia hiyo chanjo ya mRNA ya kampuni ya Pfizer (Billgate) na BioNTech (Mjerumani): Kwa nini Afrika tulazimishwe?

China na Russia kamwe hawawezi kutumia hiyo chanjo ya mRNA ya kampuni ya Pfizer (Billgate) na BioNTech (Mjerumani): Kwa nini Afrika tulazimishwe?

Dr Akili

JF-Expert Member
Joined
Aug 21, 2011
Posts
5,119
Reaction score
4,569
Hiyo tunayoiita chanjo inayotengenezwa na kampuni ya Pfizer ikishirikiana na kampuni ya BioNTech ya ujerumani si sawa na chanjo zinazojulikana ambazo hutumia virusi vya ugonjwa huo huo vilivyopunguzwa makali (attenuated live viruses). Hawa wanatumia genetically engineered manufactured synthetics za genetitically coded mRNA to instruct our DNA in the genes of our cells (nucleas chromosomes) to produce certain proteins which are thought to be protective or curative of certain diseases including cancer diseases.

Utafiti wa kutumia synthetic mRNA kutibu au kukinga magonjwa ya cancer, rabies, zika etc ni wa siku nyingi. Hata hivyo dawa au chanjo za magonjwa hayo zinazotumia genetic mRNA hazikuweza kupata approval ya kutumika kwa binadamu kutoka FDA. Kwa sababu ya taharuki, hofu na wasiwasi wa janga hili la covid - 19 FDA imezipa emergency approval dawa/ chanjo hizo za mRNA. Hazijapitia hatua zote za kimchakato za usalama kama inavyotakiwa kisayansi. Inaelekea waafrika baada ya kujazwa hofu na pesa kupenyezwa walitumika kama guine pigs katika utafiti wa usalama na uwezo wa dawa hizi. Utafiti huo haukuoneshwa kwani ulikuwa unethical.

Chanjo za covid 19 zinazotengenezwa China na Urusi ndizo chanjo halisi zinazotumia live attenuated sars- cov-2, kirusi kinachosababisha covid-19. Urusi na Uchina kamwe haziwezi kutumia hizo chanjo za mRNA kutoka Pfizer/ BioNTech. Ni kipi cha ajabu Tanzania chini ya rais mwanasayansi wa level ya PhD kuzikataa au kuzitilia mashaka hizo chanjo zao za mRNA. Kama tutaamua kuchanja tutatumia chanjo toka China au Russia kwani hizo hazichezi na DNA zetu. Chanjo zinazotumia live attenuated viruses ni rahisi kuzi verify. Hizo za mRNA huwezi ukatambua code (ujumbe) zilizobebeshwa hizo RNA.

Halafu ukweli ni kuwa Afrika ugonjwa huu si tishio hata kidogo. Takwimu ambazo tumelazimishwa na WHO kwamba hata wale ambao hawana ugonjwa lakini wame test positive kwa baadhi ya antigens za cov-2 tuwahesabu kama ni wagonjwa (covid-19), ni kitu ambacho si sahihi na hakikubaliki kisayansi. Unachokonolewa pua kutafuta kama una hizo antigen wakati antigen hizi ungaliweza kuzipata kwenye kinyesi au kwa kuchokonolewa kwenye mkundu. China sasa hivi wanatumia kipimo cha kinyesi au rectal swab which is easier and more convinient. Halafu WHO inatulazimisha tupimane sana na vipimo hatupewi bure, ni za ghari takribani Tsh laki moja kila kipimo - wanatukopesha.

Takwimu wanazozitaka siyo za prevalence wala incidence ya ugonjwa au wa virusi hao wa cov-2 kiepidemolojia nakisayansi. Ndiyo maana Trump aliiondoa USA kwenye shirika hili la WHO kwa kuvurunda kwake kuhusu suala hili. Kama ni kutaka kujua prevalence ya virusi hivi ni vyema a scientific prevalance survey of an unbiased sample population ikafanyika. Si hizi takwimu za kujumlisha contact tracing, patients and carriers.Virusi hivi vimekuwapo duniani tangia zaidi ya miaka million 50 iliyopita. Binadamu amekuwapo hapa duniani kwa miaka million tano tu. Dunia imekuwapo kwa miaka billion tano (after the Big - Bang)!

Hata kwa hizo takwimu tulizolazimishwa kukusanya bado Afrika corona si tatizo la kutufanya tutaharuki. Kwa mfano Kenya ambayo population yake ni 55 million kwa kipindi cha mwaka mmoja ni watu elfu 90 tu ndiyo wame test kuwa na antigen za corona kwenye pua zao, yaani elfu nane tu kwa mwezi! Na wanaofikiriwa kufa kwa corona (kama primary cause of death) hawazidi elfu moja kwa mwaka. Na wengi wa hawa waliokufa walikuwa na magonjwa yao mengine kama kisukari, pressure, congestive cardiac failure, renal failure, cor pulmonary, bronchoathma (pumu) etc. Wala corona haikuwa the primary cause of death. Kwa sababu ya woga na taharuki iliyojengwa kuhusu corona wagonjwa wote hawa wenye changamoto la upumuaji (dypsnoea and tachpnoea) wamekuwa wakikimbiwa au kuogopwa na wauguzi/ madaktari na kupelekea wasipate huduma sahihi ya magonjwa yao na kusababisha vifo vyao. Tumeshuhudia hadi migomo ya wauuguzi, madaktari na watoa huduma za afya wengine.

Taharuki hii kwa nchi za Afrika ndiyo wazungu wanataka ili wapate watu wa kujaribia dawa au chanjo za ugonjwa huu na pia kupiga pesa. JPM kawagusa penyewe. Ndiyo maana hawakuchelewa kuwawaya - mara oh jiandae kupokea chanjo za msaada (lakini mkopo) za mRNA etc.

Inasikitisha sana Kanisa katoliki kupitia Padre wake machachari wa Baraza la Maaskofu Tanzania, anayeitwa Kitima, bila ushahidi wa kisayansi wala ridhaa ya malaka husika, ghafla kwa taharuki limeamua kuvunja utulivu wa nchi yetu uliokuwapo dhidi ya virusi hivi. Nchi ilikuwa imetulia chini ya ulinzi wa Mungu kwa kutambua kuwa ugonjwa huu hauna tiba wala kinga na kwamba kinachoua kwenye ugonjwa huu hasa ni ile hofu na taharuki na si ukali wa virusi hivi. Hizo barakola, social distancing na lockdown hazisaidii cho chote (useless) na hapa kwetu zina madhara zadi (dangerous) au haviwezekani. Wazungu wamefanya hivyo hazikusaidia chochote. Sweden hawakufanya hivyo kama sisi and are much better! Waafrika waliouawa kwa risasi kwa sababu ya kukiuka masharti ya lockdown ni wengi kuliko waliouawa na corona.

Hata hizo barakola za grade ya juu zinazouzwa Sh elfu kumi kwa moja ambazo zinapaswa kubadilishwa kila baada ya nusu sasa, bado uwezo wake wa kuzuia virusi hivi ni 60% tu. Hivi vya nguo vikibadilishwa kila nusu saa uwezo wake ni 20%. Ukikaa nayo muda murefu (zaidi ya saa)yenyewe ndiyo inakuwa source ya kukuambukiza. Hizo PPEs wanazotakiwa kuvaa watoa huduma wa afya bei yake ni sh laki tano, na zinatakiwa kubadilishwa kila saa moja (disposable).

Na bado udhibiti wake wa virusi hivi ni kama 80% tu! Haya mambo si rahisi scientifically. Isitoshe barakola nyingi zinazoingizwa nchini zinaelekea zilishapandikizwa virusi vya corona. Barakola hizi zinasaidia tu kupunguza hofu kwa wasiojua lakini ni more risk na hatari sana hasa zinapotumika visivyo. Kumuamini Mungu kunatoa hofu hii bila risk yo yote. Na hichi ndicho rais wetu alichokuwa amekifanya kuanzia mwezi April 2020. Vifo vya corona vilitoweka baada ya wananchi kuondokewa na hofu. Walimuamini Mungu, waliamini nyungu na dawa zingine za asili. Sasa kanisa katoliki limeturudisha tulikotoka - kwenye hofu na taharuki. Vyama vya upinzani na mabeberu wame take advantage. Tusikubali.

Social distancing kwa mazingira yetu ni next to impossible na lockdown ndiyo balaa zaidi.

Vita vya dunia ya sasa zinatumia silaha za kibiolojia za mRNA.

 
The Bill gates have been controversial and no one trusts them in medicine for their evil wills. That being the case, it will be unfair to force people into their malicious and fake smiles especially when they do not like. So long as there are many COVID 19 interventions, is good to research from other sources who are not involved with these guys.

Please please acheni kukurupuka na kudharau maonyo yote haya ambayo yamekuwa yakitolewa kuhusu nia ya huyu jamaa na kupunguza binadamu duniani kupitia chanjo. Chanjo ambazo hata familiar yake hawezi kuruhusu wachomwe.



 
Hiki kirusi na ugonjwa wake umejificha na mengi. Naona kila mtu anaugua mafua na mwili, anajiponea na kwenda zake na maisha. Ila chanjo inavyopigiwa chapuo.

Biashara na maisha ya watu. Watu wenye matumbo meupe ni washenzi sana.
 
Mrusi ana chanjo yake
Mchina anayo ya kwake, kwanini watumie za watu wengine?
Iko wapi chanjo made from Tz?
Kwani (kwa Mujibu wa Mleta mada) kuna tatizo Tanzania ikiamua kununua chanjo za Urusi au China!? Zenye teknolojia ambayo tunaweza kui-decode na kujua kilichomo!? Kuliko hizi mpya za Kimarekani!

BTW... Chanjo si ipo!? Unadol
 
Mrusi ana chanjo yake
Mchina anayo ya kwake, kwanini watumie za watu wengine?
Iko wapi chanjo made from Tz?
Sasa kwa nini tusinunue chanjo toka China? Kwanza ni rafiki zetu wa damu na juzi tu Waziri wao wa mambo ya nje alikuwa Chato. Wao kazi yao ni kutupiga ban kwenye nchi zao.

Bidhaa zetu nyingi zinatoka China. Kwa nini hii bidhaa ya mRNA tulazimishwe kuinunua kutoka kwa mabeberu hawa trna kwa bei yao kubwa mara 100 ukilinganisha na ile chanjo ya China? Halafu ya China ni original, haina RNA.
 
Leo mnajilinganisha na China na Russia? Kwa taarifa tu hao "marafiki" zenu huwa hawapokei misaada mpaka ya ARV toka kwa mabeberu, na kama kweli hamtaki bidhaa za mabeberu zile Bombardier mnazoringia zimetoka wapi? Mnachekesha sana kwa huu utoto wenu mnaolazimisha muonekane "mnajiweza"

Bidhaa za mchina kwenye haya mataifa ya dunia ya tatu haziaminiki, nyingi ni feki, wanazitengeneza kwa viwango vya chini kwasababu wanajua wakituletea original hatuwezi ku- afford kununua, original watazipeleka S.A, America na ulaya; nendeni mkalete hizo pipi za mchina mmumunye kwa raha zenu.
 
Ni wakati sahihi kwa serikali yetu kuanzisha kitengo kikubwa cha biological warfare ndani ya JWTZ military intelligence unit.

Ni wakati sahihi wa kusomesha wataalamu wa hali ya juu wa microbiology, biotechnology, synthetic biology na vitu kama hivyo.
Huko tuendako sio kuzuri.

Tunahitaji uwekezaji mkubwa kwenye sayansi kwa ajili ya usalama wetu siku za usoni.

La mgambo hili!
 
Ni wakati sahihi kwa serikali yetu kuanzisha kitengo kikubwa cha biological warfare ndani ya jwtz military intelligence unit.
Ni wakati sahihi wa kusomesha wataalamu wa hali ya juu wa microbiology, biotechnology, synthetic biology na vitu kama hivyo.
Huko tuendako sio kuzuri.
Tunahitaji uwekezaji mkubwa kwenye sayansi kwa ajili ya usalama wetu siku za usoni.
La mgambo hili!
Wazo zuri, kuliko kuendelea kujidanganya hatutaki za wengine wakati sisi hatuna chanjo yetu iliyothibitishwa kisayansi.
 
Sasa kwa nini tusinunue chanjo toka China? Kwanza ni rafiki zetu wa damu na juzi tu Waziri wao wa mambo ya nje alikuwa Chato. Wao kazi yao ni kutupiga ban kwenye nchi zao.

Bidhaa zetu nyingi zinatoka China. Kwa nini hii bidhaa ya mRNA tulazimishwe kuinunua kutoka kwa mabeberu hawa trna kwa bei yao kubwa mara 100 ukilinganisha na ile chanjo ya China? Halafu ya China ni original, haina RNA.
Hao rafiki zenu wa damu wameshindwa kuwapa ARV, condoms, chanjo ya polio, chanjo ya TB (BCG) na hata logistic ya kusambaza chanjo ya COVID ni UNICEF ndiyo wasambazaji.
 
Hakuna ugonjwa mbaya kama hofu watu hivi sasa tumejazwa hofu kubwa, tena tunaambiwa hii covid ya sasa ni hatari kuliko ile ya kwanza, cha ajabu wao bado ligi na michezo inaendelea kule kwao. Hapa ndio utagundua kwa nini walitaka idadi ya wagonjwa iwe inatangazwa kila siku tena iwe inatajwa kila siku badala ya kurecord kimya kimya kama inavyofanyika kwa magonjwa mengine, tena idadi ya wagonjwa iwe inaongezeka badala ya kushuka, na pia utashanga kwa nini mke wa Bilgate alitabiri Africa tutakufa kama kuku na pia utajiuliza ni kwa nini Biligate amekuwa akizungumzia utishio wa covid utadhani yeye ni waziri wa afya.

Mimi napongeza msimamo wa Mh. Rais asikubali kufuata mkumbo, wananchi tunapaswa kuchukua tahadhari na kuendelea na shughuli zetu kama kawaida. Ni ajabu kuona nchi za Africa zimeshindwa kudhibiti vifo vinavyotokana na malaria, njaa, mafuriko, na ajali za barabarani ambavyo ndio vinagharimu maisha ya raia kwa wingi eti leo wanatumia njia za matajiri wa magharibi kudhibiti na kujikinga na covid.

Corona itakuja na mengi, binafsi naiona kama hii issue imekaa kibiashara zaidi, sikatai kwamba hakuna coron, corona ipo ila kwa jinsi inavyopaishwa wengi wanakufa na kwa hofu. Embu tujiulize, mbona mafua yamekuwa tishio kwa wazungu miaka nenda rudi mbona hakuna chanjo yake? Sisi wa Afrika tukiugua mafua ndani ya siku saba yanaisha yenyewe. Kumbe kuna uwezekano wazungu wangeamua kututia hofu kwenye mafua basi na sisi tungeanza kufa kwa hofu ya mafua then tungeambiwa tumekufa kwa mafua.

Ifike mahala viongozi wetu wajitambue, kwa mujibu wa maandiko mamlaka yeyote yametoka kwa Mungu, tuliona awamu ya kwanza Mh. Rais alikataa lockdown dunia ikamshanga lakini baadae karibu dunia nzima ilifuata njia zake lakini sijaona hao WHO wakimpa tuzo. Naamini na kwenye hii awamu ya pili ataibuka kidedea tena.
 
Nyinyi Ni wanasayansi wazuri lakini mna kiburi na uwezo mdogo wa kufanya utafiti. Kama mna jeuri hiyo tengenezeni dawa zenu na mtoe chanjo. Kwa Nini Ni rahisi kuchukua ndege kwenda kutuletea juisi ya majani ya kuua viroboto huku mkijiamini 100% kuwa Ni tiba ya corona halafu mnaponda tafiti za kitalaamu?

It is simple, tukatae hizo dawa halafu tuendelee na ARV na condom zao tuone tulivyo wajanja. Surua, polio, pepopunda na TB hatuulizi na huku zimo kwenye miili yetu. Hadi vyandarua vyenye dawa kujikinga na mbu tusiambukizwe maleria hatuweki mkwara, lakini kuvaa barakoa na kupokea chanjo dhidi ya corona tunaweza kutunisha misuli. Kwa kifupi kila mmoja alinde mwili wake awezavyo. Kwaheri
 
WHO wenyewe wanasemaje? Trump alijitoa WHO ila Biden baada ya kuingia cha kwanza alitangaza kurudiana na WHO,siyo kwamba hizo chanzo za US ndo itaenda kupigiwa chapuo na WHO?

Lakini Russia wao washagundua
 
Nyinyi Ni wanasayansi wazuri lakini mna kiburi na uwezo mdogo wa kufanya utafiti. Kama mna jeuri hiyo tengenezeni dawa zenu na mtoe chanjo. Kwa Nini Ni rahisi kuchukua ndege kwenda kutuletea juisi ya majani ya kuua viroboto huku mkijiamini 100% kuwa Ni tiba ya corona halafu mnaponda tafiti za kitalaamu?...
Umeongea point hakuna watu wajinga Kama waafrika walio wengi akiwemo mtoa mada, anadhani hao warusi na wachina ni watu wazuri sana kumbe ni walele kwanza ni wabaguzi wa wazi wazi ukienda nchi zao

Ukiangalia USAID hela anayochangia kwenye sekta ya afya ni kubwa lakin leo tunawaona ni wabaya
 
ilikuwaje corona ikapungua maambukizi mwaka jana June to July?

Pili,imekuwaje imerudi tena six months later tena kwa spidi?

Haya ni mambo tunapaswa kuyatafakari na kuyafanyia kazi kitaalamu.

Ukiishakuwa na jambo si la kawaida duniani kote,unapaswa kulipigia mstari nyumbani kwako kuhakikisha liko controled kwa mazingira yako.

Ni zipi medical,social na economic impact kwa sasa na baadae?Zitatuathiri vipi na tunachukua mkondo gani kuminimise damages?

Nini kinaendelea huko kwa wenzetu kuhusu ugonjwa huu,umetokeaje,wanapambana nao vipi,wanapanga nini kwa sasa na baadae?Mipango yao inatuathiri vipi na mipango yetu itawaathiri vipi wao?

Nani wa kushirikiana nae kwa ukaribu zaidi katika janga hili?

Mwisho kabisa naomba serikali yetu iwe makini sana na anything concerning "gene modifications" na "DNA alterations".Eneo hili tusipelekeshwe kabisa,tujipe mda wa kutosha kabla ya kukubaliana na chochote kuhusu hili...narudia tena,bora tuendelee kufa kwa kuenenda taratibu kwenye masuala ya tafiti zinazohusu modifications za maumbile ya kiasili mpaka tutakapojiridhisha nazo kuliko kuzikubali tu haraka haraka,please,please,please.
 
Bill gate has been controversial and no one trusts them in medicine for their evil wills. That being the case, it will be unfair to force people into their malicious and fake smiles especially when they do not like. So long as there are many COVID 19 interventions, is good to research from other sources who are not involved with these guys...
Hivi bill gates anahusikaje na Pfizer au biotech kampuni ya ujerumani, mnamuongelea as if yeye ndo mmiliki wa kampuni zote za pharmaceutical, Kama ndo hivyo angekua ni trillionaire
 
Back
Top Bottom