China vs U.S Trade War: Walmart kampuni ya Marekani yaanza kuonja joto la jiwe la tariffs za Trump kwa bidhaa za China

Xi Jinping

JF-Expert Member
Joined
Jun 14, 2023
Posts
3,651
Reaction score
11,548
Walmart kampuni ya kimataifa inamilikiwa na Walton family inashikilia rekodi ya kuwa muajiri mkubwa zaidi duniani ikiwa imeajiri watu zaidi ya milioni 2 katika nchi tofauti tofauti, na ina stores zaidi ya 10,000 sehemu mbalimbali duniani.

Biashara yao kubwa ni kuuza bidhaa za aina tofauti tofauti kwa njia ya rejareja (retail) kupitia stores au supermarkets.

Asilimia 60 ya bidhaa zilizo katika stores za Walmart zinaagizwa kutoka kwa suppliers wa China.

Baada ya Trump kuongeza tariffs kwa bidhaa za China zinazoingia Marekani, limekuwa pigo kwa Walmart na raia wa Wamarekani walio wateja wa bidhaa za Walmart.

Inachohofia Walmart ni kupungua kwa mauzo na faida ya biashara zao. Kwa upande wa mnunuzi ni kukutana na ongezeko la bei na kuongeza gharama za maisha.

Walmart imeanza kuwaomba suppliers wake walioko China wawapunguzie bei eti ili mzigo wa tariffs uwaangukie makampuni ya China yanayofanya biashara na Walmart.

Wizara ya Biashara ya China na suppliers wa China wanaoiuzia Walmart bidhaa wamekataa ombi hilo na kusema kuwa anayetakiwa kulipia gharama za tariffs ni Wamarekani wenyewe.

Walmart watalazimika kuongeza bei za bidhaa zao ili kufidia tariffs ziliongezwa na serikali ya Trump. Na Wamarekani watalazimika kununua kwa gharama kubwa.

Trump anawatoza kodi Wamarekani indirect kupitia tariffs. Baadaye atasema kupitia tariffs serikali imekusanya kiasi fulani ila ukweli ni kwamba amechukua mapato kutoka mifuko ya Wamarekani.

Tariff policy beneficiaries are always visible, but its victims are mostly invisible. Politicians love this.
 
Walmart kampuni ya kimataifa inayomilikiwa na Walton family inayoshikilia rekodi ya kuwa muajiri mkubwa zaidi duniani ikiwa imeajiri watu zaidi ya milioni 2 katika nchi tofauti tofauti, na ina stores zaidi ya 10,000 sehemu mbalimbali duniani.

Biashara yao kubwa ni kuuza bidhaa za aina tofauti tofauti kwa njia ya rejareja (retail) kupitia stores au supermarkets.

Asilimia 60 ya bidhaa zilizo katika stores za Walmart zinaagizwa kutoka kwa suppliers wa China.

Baada ya Trump kuongeza tariffs kwa bidhaa za China zinazoingia Marekani, limekuwa pigo kwa Walmart na raia wa Wamarekani walio wateja wa bidhaa za Walmart.

Inachohofia Walmart ni kupungua kwa mauzo na faida ya biashara zao. Kwa upande wa mnunuzi ni kukutana na ongezeko la bei na kuongeza gharama za maisha.

Walmart imeanza kuwaomba suppliers wake walioko China wawapunguzie bei eti ili mzigo wa tariffs uwaangukie makampuni ya China yanayofanya biashara na Walmart.

Wizara ya Biashara ya China na suppliers wa China wanaoiuzia Walmart bidhaa wamekataa ombi hilo na kusema kuwa anayetakiwa kulipia gharama za tariffs ni Wamarekani wenyewe.

Walmart watalazimika kuongeza bei za bidhaa zao ili kufidia tariffs ziliongezwa na serikali ya Trump. Na Wamarekani watalazimika kununua kwa gharama kubwa.

Trump anawatoza kodi Wamarekani indirect kupitia tariffs. Baadaye atasema kupitia tariffs serikali imekusanya kiasi fulani ila ukweli ni kwamba amechukua mapato kutoka mifuko ya Wamarekani.

Tariff policy beneficiaries are always visible, but its victims are mostly invisible. Politicians love this.
Marekani stocks zinaanguka wakati china thamani ya stocks inapanda.
Bado tarriffs hazijamaliza kumuua marekani. China wako kwenye majaribio ya mwisho ya kutengeneza machine za kufyatua chips kwa kutumia mwanga zile ambazo zinatengenezwa na kampuni moja tu duniani.
Kwa maelezo yao wanasema wanategemea zianze kuingia sokoni 2026.
 
Wakati Trump anaangalia miles ahead wacha-mbuzi uchwara mnaangalia usawa wa pua zenu!

Kwanini Marekani (Walmart) iagize China 60% ya products zake? Kwanza hiyo ni national security issue. Plan ya Trump ni wazalishaji wazalishie Marekani badala ya Marekani kugeuka Kariakoo.

He is doing great job; matokeo yake yataonekana very soon.
 
Trump alianza na hii sera MAGA (Make America Great Again) tangu 2018

Mpaka sasa amefanikiwa kuanzisha viwanda vingapi kama import substitution industries kwa products wanazoimport kutoka China?
 
Kwahiyo na zile tariffs zilizopangwa kuongezwa na China kwa bidhaa zinazotoka Marekani nazo zitawaathiri wachina wenyewe.
 
Plan ya Trump ni wazalishaji wazalishie Marekani badala ya Marekani kugeuka Kariakoo.

He is doing great job; matokeo yake yataonekana very soon.
But at what cost?

Unafikiri miaka 4 inatosha kwa Marekani kurevive manufacturing industry? Jibu ni HAPANA

Wanasiasa wa Marekani kisiasa wanasema kuhusu kununua bidhaa kutoka mataifa mengine kama Vietnam, Indonesia n.k ambapo napo manufacturers wengi wa nchi ni wawekezaji wa China
 
Uliwahi kuona wapi tariff inamuathiri exporter?
Nimekwambia kwa bidhaa zinatoka Marekani kwenda China.

Issue ilikuwa US ikiongeza tariffs kwa 10% kwenye bidhaa zinazotoka China, naye China anaongeza tariffs kwa 10% kwenye bidhaa zinazotoka US.

Kwahiyo kama raia wa US wanateseka kwa gharama kubwa kwenye bidhaa zinazotoka China, pia raia wa China wanateseka na gharama kubwa kwa bidhaa zinazotoka US
 
Ili kulinda soko la ndani, hivo ndio inavotakiwa kua; kuna bidhaa gani inatengenezwa China Marekani HAWANA? Ili kufanya makampuni mengi yake kuwekeza kwako, njia ya Trump ndio njia sahihi. Weka kodi kubwa kwa bidhaa zitokazo nje while nyie pia mnazo and punguza kodi kwa bidhaa ambazo huzalishi nchini mwako, that will enable investors to invest into your country cause soko lipo. Sio unaweka kodi kubwa kwenye magari na mafuta wakati huna uwezo wa kuzalisha, halafu unapunguza kodi kwenye juice kutoka Misri while Azam na wengine wanatengeneza bidhaa zenye quality hiyo hiyo. Unahitaji kua na wananchi wenye uzalendo sana ku opt kutumia local made than exported products, uzalendo huo kwa nchi za Kiafrica nadhani hata ulaya hakuna, mataifa mengi ya Asia yanao
 
Nimekwambia kwa bidhaa zinatoka Marekani kwenda China.

Issue ilikuwa US ikiongeza tarrifs kwa 10% kwenye bidhaa zinazotoka China, naye China anaongeza tarrifs kwa 10% kwenye bidhaa zinazotoka US.

Kwahiyo kama raia wa US wanateseka kwa gharama kubwa kwenye bidhaa zinazotoka China, pia raia wa China wanateseka na gharama kubwa kwa bidhaa zinazotoka US
Sehemu kubwa ya bidhaa ambazo China inaigiza kutoka Marekani ni agricultural products.

Na China tayari ina suppliers wengi mbadala kama Brazil, Argentina, Australia, Russia, Ukraine na mataifa mengine

Na tena kwa bei nafuu kuliko Marekani kwa hiyo huwezi kukuta Mchina anaathirika na bidhaa za Marekani zilizopigwa tariffs kuingia China

Na sio kwamba China haikuona mataifa mengine kama Brazil ni vile iliheshimu mikataba ya kibiashara kati ya mataifa hayo 2 kwa lengo la kuimarisha diplomatic relationship kati yao

Ila kwa kuwa Trump kaamua kumwaga mboga haina budi China nao wamwage ugali
 
Nimekwambia kwa bidhaa zinatoka Marekani kwenda China.

Issue ilikuwa US ikiongeza tariffs kwa 10% kwenye bidhaa zinazotoka China, naye China anaongeza tariffs kwa 10% kwenye bidhaa zinazotoka US.

Kwahiyo kama raia wa US wanateseka kwa gharama kubwa kwenye bidhaa zinazotoka China, pia raia wa China wanateseka na gharama kubwa kwa bidhaa zinazotoka US
Siipendi Marekani na natamani ianguke kwa sababu ya mabaya anayofanya duniani ila mtoa mada kaandika kishabiki sana.Umemuuliza kama kuongeza kodi kwa bidhaa zinazotoka China wanaoumia ni Wamarekani vipi na kodi iliyoongezwa na China kwa bidhaa kutoka Marekani kuwa watakaoumia ni Wachina wenyewe anakataa haitakuwa hivyo.
 
Soma message #12
 
Wakati Trump anaangalia miles ahead wacha-mbuzi uchwara mnaangalia usawa wa pua zenu!

Kwanini Marekani (Walmart) iagize China 60% ya products zake? Kwanza hiyo ni national security issue. Plan ya Trump ni wazalishaji wazalishie Marekani badala ya Marekani kugeuka Kariakoo.

He is doing great job; matokeo yake yataonekana very soon.
Shida soko sio marekani tu, kuna international market ambapo kutokana na labour cost hawataweza ku compete na china, labda kama viwanda vitatudi kutengeneza kwa U.S market peke yake
 
Wakati Trump anaangalia miles ahead wacha-mbuzi uchwara mnaangalia usawa wa pua zenu!

Kwanini Marekani (Walmart) iagize China 60% ya products zake? Kwanza hiyo ni national security issue. Plan ya Trump ni wazalishaji wazalishie Marekani badala ya Marekani kugeuka Kariakoo.

He is doing great job; matokeo yake yataonekana very soon.
Miaka minne michache sana
 
Back
Top Bottom