Xi Jinping
JF-Expert Member
- Jun 14, 2023
- 3,651
- 11,548
Walmart kampuni ya kimataifa inamilikiwa na Walton family inashikilia rekodi ya kuwa muajiri mkubwa zaidi duniani ikiwa imeajiri watu zaidi ya milioni 2 katika nchi tofauti tofauti, na ina stores zaidi ya 10,000 sehemu mbalimbali duniani.
Biashara yao kubwa ni kuuza bidhaa za aina tofauti tofauti kwa njia ya rejareja (retail) kupitia stores au supermarkets.
Asilimia 60 ya bidhaa zilizo katika stores za Walmart zinaagizwa kutoka kwa suppliers wa China.
Baada ya Trump kuongeza tariffs kwa bidhaa za China zinazoingia Marekani, limekuwa pigo kwa Walmart na raia wa Wamarekani walio wateja wa bidhaa za Walmart.
Inachohofia Walmart ni kupungua kwa mauzo na faida ya biashara zao. Kwa upande wa mnunuzi ni kukutana na ongezeko la bei na kuongeza gharama za maisha.
Walmart imeanza kuwaomba suppliers wake walioko China wawapunguzie bei eti ili mzigo wa tariffs uwaangukie makampuni ya China yanayofanya biashara na Walmart.
Wizara ya Biashara ya China na suppliers wa China wanaoiuzia Walmart bidhaa wamekataa ombi hilo na kusema kuwa anayetakiwa kulipia gharama za tariffs ni Wamarekani wenyewe.
Walmart watalazimika kuongeza bei za bidhaa zao ili kufidia tariffs ziliongezwa na serikali ya Trump. Na Wamarekani watalazimika kununua kwa gharama kubwa.
Trump anawatoza kodi Wamarekani indirect kupitia tariffs. Baadaye atasema kupitia tariffs serikali imekusanya kiasi fulani ila ukweli ni kwamba amechukua mapato kutoka mifuko ya Wamarekani.

Tariff policy beneficiaries are always visible, but its victims are mostly invisible. Politicians love this.