Ship building ni moja ya sekta muhimu sana kwa uchumi wa nchi na usalama wa taifa.
Wakati Marekani kwa wastani inazalisha meli 5 kwa mwaka China inazalisha meli 5 kwa siku!
Kwa sasa China inazalisha meli mara 340 hivi zaidi ya Marekani
Shipyards za China kwa ujumla zinazalisha zaidi ya 23 millions tons, wakati za Marekani zinalizalisha chini ya 100,000 tons
95% ya shipping container unazoziona baharini ni China made
Katika soko la dunia China inashikilia nafasi ya kwanza kwa zaidi ya 50% katika global ship building huku Marekani ikiwa nafasi ya 19 kwa 0.1%
Mwaka 2024, China ilikuwa na oda za meli 1,794 kubwa za kibiashara, Korea Kusini ilikuwa na 734, Japan ilikuwa na 587 uliza Marekani ilikuwa na ngapi? Ilikuwa na 5 tu!
Mwaka 2024 China ilikuwa na zaidi ya meli 5,000 za kibiashara baharini, wakati U.S flagged merchant fleet zilikuwa 177 pekee.
Mwaka 2024 shipyard moja tu ya China iliunda meli nyingi za kibiashara kwa tani kuliko shipyards zote zilizo Marekani zikiunganishwa.
View attachment 3268498
Kwa sasa China ina uwezo mkubwa zaidi wa kutengeneza meli kuliko taifa lolote duniani, hata kuliko nchi 5 zilizo chini yake zikiunganishwa.
Makampuni ya kutengeneza meli, ikiwa ni pamoja na makampuni yaliyo katika nchi nyingi washirika wa Marekani kama Denmark, Ufaransa, Greece, Japan, Singapore na South Korea hununua 75% ya critical components za kutengeneza meli kutoka China.
Katika shipyards zilizo China serikali ya China imefanya kitu kinachoitwa Military-Civil Fusion (MCF) strategy.
Yaani imeunganisha uzalishaji wa kibiashara na kijeshi katika shipyards na kuipa PLA Navy (China Navy) miundombinu ya kutengeneza meli vita. Hii imefanya PLA Navy kuwa ya kisasa na kupunguza gharama.
Baada ya mambo kuwa magumu kwa Marekani imeanza kujaribu kuingia ubia na South Korea na Japan ili wapate tech transfer kunyanyua US ship building industry.
Kwa mfano Hanwa Ocean kampuni ya South Korea imenunua shipyard katika jimbo la Philadelphia kwa USD 100 mln. Na imeingia mkataba na U.S Navy kutumia hiyo shipyard kwa ajili ya maintenance and repair ya meli vita zilizozeeka za Marekani.
Hata iwe kwa msaada kutoka kwa makampuni ya Asia kama S.K na Japan inaweza kuchukua miaka mingi sana Marekani ili kuziba pengo na China katika ship building industry.
Inashangaza kuwa Trump anapendekeza kupanua ship building industry ya Marekani eti ishindane na China huku ameongeza tariffs kwa chuma na aluminium inayotumika kutengeneza meli hizo.
Ili kutimiza ndoto yake, labda aifanye South Korea na Japan kuwa majimbo ya 52 na 53 ya Marekani.
China has become global powerhouse in ship building industry.
Rising dragon fading Eagle.