China vs U.S, utengenezaji wa meli za kibiashara: Kwa mwaka, China inaunda meli zaidi ya 1,700 huku Marekani ikiunda meli 5 tu.

China vs U.S, utengenezaji wa meli za kibiashara: Kwa mwaka, China inaunda meli zaidi ya 1,700 huku Marekani ikiunda meli 5 tu.

..swali la kujiuliza ni nini kilipelekea sekta ya ujenzi wa meli kuporomoka nchini Marekani.

..kwanini zamani walikuwa wako juu, lakini sasa hivi wako chini?

..kwanini Wamarekani wanaweza kutengeneza masilaha makubwa-makubwa lakini wanashindwa na nchi kama South Korea kutengeneza magari?
Umezugumzia mambo 2 sekta ya ujenzi wa meli kuporomoka na kutengeneza silaha

Tuanze na ship building, hii iko kwenye manufacturing industry. Marekani iliwahi kuwa industrial powerhouse miaka ya nyuma. Kosa kubwa iliyofanya Marekani ni kuipa kipaumbembele finance capitalism kuliko industrial capitalism

Hilo lilipelekea kushuka kwa industrial output kutia ndani ship building.

Lakini pia Marekani ilikabili ushindani mkubwa sana kutoka Japan miaka ya 1980 na 1990 kwenye ujenzie wa meli.

Tuzungumzie upande wa pili. Kwa nini Marekani inaweza kutengeneza silaha?

U.S MIC (Military Industrial Complex) ni combination ya pande 3; Pentagon, defense contractors (watengenezaji wa silaha pamoja) na serikali ya Marekani.

Pentagon ni kitengo maalumu kinachoiwakilisha serikali ya Marekani kudeal na defense contractors

Ikumbukwe kuwa Marekani ndiye muuzaji mkubwa wa silaha duniani.

Ili kuilinda biashara hiyo ya silaha inayoingizia Marekani billions of dollars serikali ya Marekani kupitia Pentagon wanawawezesha defense contractors kwa hali na mali ikiwezekana hata kwa ruzuku ili waweze kuunda silaha

Na silaha zinapouzwa pande zote mbili wanafaidika serikali na defense contractors
 
Manufacturing duniani kashika mchina , majuzi mbunge mmoja India alikua analalamika kua bidhaa nyingi India ni made in china
Tatizo la India ni moja

Wachina walitamani sana kuinvest India ila Wahindi sio watu.

Ni jamii fulani inajiona imejipata lakini kumbe bado wana safari ndefu ni watu wa kujivuna au kutaka kucompete na China lakini wamepigwa gap la kwenda.

Wamekuwa wakiyapiga fines makampuni mengi ya kigeni yaliyowekeza India kwa sababu za kijinga sana zisizo na mashiko.

Imefikia wakati India imepewa jina la graveyard of foreign investment.

Makampuni yamekuwa yakifunga biashara zao India kwa sababu ya sera zao za kipumbavu za uonevu.

Wataendelea sana kuimport bidhaa na components kutoka China

Elon alikuwa na ukaribu sana na Narendra Modi na ilionekana kuwa Tesla watafungua plant India ila Elon akamkimbia alipoona jinsi serikali ya India inawatreat foreign investors
 
Ship building ni moja ya sekta muhimu sana kwa uchumi wa nchi na usalama wa taifa.
  • Wakati Marekani kwa wastani inazalisha meli 5 kwa mwaka China inazalisha meli 5 kwa siku!​
  • Kwa sasa China inazalisha meli mara 340 hivi zaidi ya Marekani​
  • Shipyards za China kwa ujumla zinazalisha zaidi ya 23 millions tons, wakati za Marekani zinalizalisha chini ya 100,000 tons​
  • 95% ya shipping container unazoziona baharini ni China made​
  • Katika soko la dunia China inashikilia nafasi ya kwanza kwa zaidi ya 50% katika global ship building huku Marekani ikiwa nafasi ya 19 kwa 0.1%​

  • Mwaka 2024, China ilikuwa na oda za meli 1,794 kubwa za kibiashara, Korea Kusini ilikuwa na 734, Japan ilikuwa na 587 uliza Marekani ilikuwa na ngapi? Ilikuwa na 5 tu!​
  • Mwaka 2024 China ilikuwa na zaidi ya meli 5,000 za kibiashara baharini, wakati U.S flagged merchant fleet zilikuwa 177 pekee.​
  • Mwaka 2024 shipyard moja tu ya China iliunda meli nyingi za kibiashara kwa tani kuliko shipyards zote zilizo Marekani zikiunganishwa.​

View attachment 3268498
Kwa sasa China ina uwezo mkubwa zaidi wa kutengeneza meli kuliko taifa lolote duniani, hata kuliko nchi 5 zilizo chini yake zikiunganishwa.
  • Makampuni ya kutengeneza meli, ikiwa ni pamoja na makampuni yaliyo katika nchi nyingi washirika wa Marekani kama Denmark, Ufaransa, Greece, Japan, Singapore na South Korea hununua 75% ya critical components za kutengeneza meli kutoka China.​

Katika shipyards zilizo China serikali ya China imefanya kitu kinachoitwa Military-Civil Fusion (MCF) strategy.
  • Yaani imeunganisha uzalishaji wa kibiashara na kijeshi katika shipyards na kuipa PLA Navy (China Navy) miundombinu ya kutengeneza meli vita. Hii imefanya PLA Navy kuwa ya kisasa na kupunguza gharama.​

Baada ya mambo kuwa magumu kwa Marekani imeanza kujaribu kuingia ubia na South Korea na Japan ili wapate tech transfer kunyanyua US ship building industry.
  • Kwa mfano Hanwa Ocean kampuni ya South Korea imenunua shipyard katika jimbo la Philadelphia kwa USD 100 mln. Na imeingia mkataba na U.S Navy kutumia hiyo shipyard kwa ajili ya maintenance and repair ya meli vita zilizozeeka za Marekani.

    Hata iwe kwa msaada kutoka kwa makampuni ya Asia kama S.K na Japan inaweza kuchukua miaka mingi sana Marekani ili kuziba pengo na China katika ship building industry.​

Inashangaza kuwa Trump anapendekeza kupanua ship building industry ya Marekani eti ishindane na China huku ameongeza tariffs kwa chuma na aluminium inayotumika kutengeneza meli hizo.

Ili kutimiza ndoto yake, labda aifanye South Korea na Japan kuwa majimbo ya 52 na 53 ya Marekani.

China has become global powerhouse in ship building industry.

Rising Dragon fading Eagle.
Na hapo kwa usa kwa asilimia kubwa wakorea ndo wanawasaidia ..
 
China wakijipata hizo kazi zitaenda India na Vietnam huko na tayari washaanza wao watabaki kufanya kazi za kitozi kwa maslahi makubwa kama USA.

Kazi ngumu mpe mjinga. Believe me you boss wako anafanya kazi ndogo kwa maslahi makubwa kuliko wewe.
Mchina hana mentality hiyo ya kivivu ya watu wa Magharibi

Kwanza kabisa ukae ukijua kuwa China ndiye investor mkubwa upande wa manufacturing sector katika nchi za ASEAN kuzidi S.K, Japan na Marekani

Lakini hilo halijamfanya Mchina arelax nyumbani kwake eti kisa tu ameinvest nje. Bado ni kazi kazi hata ndani ya China
 
Tatizo la India ni moja

Wachina walitamani sana kuinvest India ila Wahindi sio watu.

Ni jamii fulani inajiona imejipata lakini kumbe bado wana safari ndefu ni watu wa kujivuna au kutaka kucompete na China lakini wamepigwa gap la kwenda.

Wamekuwa wakiyapiga fines makampuni mengi ya kigeni yaliyowekeza India kwa sababu za kijinga sana zisizo na mashiko.

Imefikia wakati India imepewa jina la graveyard of foreign investment.

Makampuni yamekuwa yakifunga biashara zao India kwa sababu ya sera zao za kipumbavu za uonevu.

Wataendelea sana kuimport bidhaa na components kutoka China

Elon alikuwa na ukaribu sana na Narendra Modi na ilionekana kuwa Tesla watafungua plant India ila Elon akamkimbia alipoona jinsi serikali ya India inawatreat foreign investors
Wahindi amna kitu ni wa chuuzi tu tena wawashukuru wachina
 
Wahindi amna kitu ni wa chuuzi tu tena wawashukuru wachina
Umesema vyema bado wana akili za kitumwa sana kwenye jamii yao hasa kuwanyenyekea Wazungu

Wakipata nafasi ya kufanya kazi Ulaya au Marekani wanajiona wamemaliza. Wazungu wanawanyonya kwa kuwafanya CEOs

Sasa ona tofauti ya Mchina na Mhindi. Mchina anapathamini sana nyumbani kwao na tamaa yake ni kujitegemea kiteknolojia na kiuchumi

India pamoja na kuwa na talents nyingi kwenye IT hawana hata google yao kama China walivyo na BaiDu, au jinsi China ilivyo na BaiDu maps badala ya Google Maps

Hawana brands za ushindani wa kimataifa kwenye sci-tech kama China walivyo na HUAWEI, Lenovo, Xiaomi, BYD, Hisense, DJI, TikTok, DeepSeek n.k
 
Kwa mfano kwenye pharmeceutical industry wanategemea sana China

Zaidi ya 70% ya APIs za kuengeneza dawa India wanaimport kutoka China

Bila China pharamaceutical industry ia India ni bure kabisa
Kuna wale wachumi na watafiti waliokuwa wanasema the "The next China is India."

Sasa hivi wamekiri kuwa "The next China is China."
 
Umesema vyema bado wana akili za kitumwa sana kwenye jamii yao hasa kuwanyenyekea Wazungu

Wakipata nafasi ya kufanya kazi Ulaya au Marekani wanajiona wamemaliza. Wazungu wanawanyonya kwa kuwafanya CEOs

Sasa ona tofauti ya Mchina na Mhindi. Mchina anapathamini sana nyumbani kwao na tamaa yake ni kujitegemea kiteknolojia na kiuchumi

India pamoja na kuwa na talents nyingi kwenye IT hawana hata google yao kama China walivyo na BaiDu, au jinsi China ilivyo na BaiDu maps badala ya Google Maps

Hawana brands za ushindani wa kimataifa kwenye sci-tech kama China walivyo na HUAWEI, Lenovo, Xiaomi, BYD, Hisense, DJI, TikTok, DeepSeek n.k
True wakishaaenda ulaya na usa na wao hujiona tiari wameshaamaliza kila kitu ..
 
Industrial power ya Wachina ni next level,
Hata ammunition wana uwezo wa 1mil kwa siku wakati marekani hiyo ni mwaka mzima.
Marekani wamepitwa hadi na Ukraine kwenye utengenezaji wa Drone, Ukraine drone 2mil kwa mwaka, Marekani Drone 100K
Na hapo usa akitengene mnyororo wa ubeneru ndo unajaa huko mpka product inakuja kutoka kuna hela za wanasiasa kibao huko na product inakuwa ghali karibu mara 20 zaidi
 
Binafsi naona China wapo vizuri kwenye technology na Engineering kuliko taifa lolote hata US. Ukiangalia wao ndo wa kwanza kutengeneza hypersonic bombs, wametengeneza maglev trains ( treni zinazoelea) na pia wametengeneza treni zinazopita katikati ya majengo bila kuisahau Deepseek AI inayoongoza sasa hivi.

Nakubali China wanatengeneza fake items ila kwenye vitu serious kama meli wapo vizuri ndo maana wanapokea order nyingi.
Maglev hii hii technology ya Mjerumani? Au nyingine !? China anajua kutumia technology zilizobuniwa na wengine, ila sio kubuni mpya.
 
Kina ww ndio tuliosema kama hujui kitu usilete habari za kwenye kitchen party mnaboa huna data unapayuka Ukraine hzo meli na former USSR Ukraine hajawahipo tengeneza meli wakt wa mungano viwanda viliwekezwa Ukraine sasa ww mtu yupo space huko anashindwaje kujenga machma hata song or Marine pale kigamboni anaweza usilete mada zankusutana tunataka data/ reliable sources wala hatulinganishi eti Trump mtu ana mwez madarakani against China isiyotawaliwa na mkoloni
China isiyotawaliwa na Mkoloni!? Kwani US anatawaliwa na mkoloni!? By the way ,hao wote US na China wadhawahi kutawaliwa na Waingereza pamoja Japan.
 
Maglev hii hii technology ya Mjerumani? Au nyingine !?.
Upande wa High Speed Railway China ina technology yake mfano treni lenye kasi zaidi duniani ni la China 450km/hr na linatumia teknolojia ya China fuxing

Mchina ametumia Maglev tena ni kakipande kadogo sana km 29 kutoka Pudong Airport Shanghai kwenda city centre

Ila km zote za HSR zilizobaki karibu 50,000 zinatumia teknolojia ya ndani Fuxing na Hexie
 
Maglev hii hii technology ya Mjerumani? Au nyingine !? China anajua kutumia technology zilizobuniwa na wengine, ila sio kubuni mpya.
Maglev za China usizifananishe na takataka zingine zozote zile. Maglev ya China ina speed sawasawa na ndege sasa za Mjerumani au Mjapan zina maajabu yapi?
 
Maglev za China usizifananishe na takataka zingine zozote zile. Maglev ya China ina speed sawasawa na ndege sasa za Mjerumani au Mjapan zina maajabu yapi?
Nimeandika technology ya Mjerumani ,wewe unaleta porojo. Hiyo Msglev ni technology ys Mchina!?
 
Back
Top Bottom