Jeshi la China limeripoti kama kitendo Cha uchokozi dhidi ya China, baada ya destroyer Raph Johnson (meli ya kivita) ya Marekani kupita katika lango la bahari linalotenganisha China na Taiwan.(Taiwan strait).
Jeshi la China limelaani/kulaumu KITENDO hicho Cha Marekani Huku likiongeza kuwa,
kitendo hicho Ni Cha hatari na kinatuma alama mbaya kwa (PRO Taiwan Independence forces) vikosi ambavyo vipo kwaniaba ya Uhuru wa Taiwan alisema msemaji wa jeshi la China.
Taiwan ni suala nyeti na muhimu kabisa katika mahusiano ya China na Marekani (Sino-US relationship) hii inakuja siku moja baada ya mazungumzo ya wakuu wa nchi hizo mbili kupitia video call.
Ripoti zinasema China pia ilipeleka meli zake za kivita eneo Hilo nyeti la Lango la Taiwan kufuatilia nyenendo za Meli hiyo.
Baadae Mara ya pili China ilipeleka meli yake mpya Shadong ambayo ni (aircraft carrier).
Suala hili la Taiwan liliongelewa na Raisi wa China XI na mwenzake wa Marekani Biden,
Akisisitiza suala la Taiwan linatakiwa liendeshwe kwa usahihi.
CHINA inaendelea kuihesabu Taiwan Kama eneo lake na siku Hadi siku imeendelea kuimarisha shughuli zake za kijeshi karibu na kisiwa hicho cha Taiwan.
Hali hii imeendelea kuwasha alamu Taipei katikati ya suala la UKRAINE na Urusi kwamba CHINA inaweza ikafuata nyayo za Urusi na kutumia ndugu zake za kijeshi.
View attachment 2158390View attachment 2158392View attachment 2158393View attachment 2158395