China yaitangulia Marekani kwa kiwango cha kukubaliwa kwa uwezo wa uongozi wa kimataifa

China yaitangulia Marekani kwa kiwango cha kukubaliwa kwa uwezo wa uongozi wa kimataifa

Yoyo Zhou

Senior Member
Joined
Jun 16, 2020
Posts
199
Reaction score
322
4a36acaf2edda3cc3a00cbfc71894510233f92f3.webp
Uchunguzi wa maoni uliofanywa hivi karibuni na Gallup, ambalo ni shirika maarufu la kimataifa la uchunguzi wa maoni, unaonesha kwamba mwaka jana, kiwango cha kukubaliwa kwa uongozi wa kimataifa wa China ni asilimia 36, na kuizidi Marekani kwa asilimia 5.

Uchunguzi wa Gallup umeshirikisha zaidi ya nchi 130, na kuwa na uwakilishi mpana. Matokeo ya uchunguzi huo yanaonesha kwamba mwaka 2025, wastani wa kiwango cha kukubaliwa kwa uongozi wa kimataifa wa Marekani kilishuka hadi asilimia 31, kikipungua kwa asilimia 8 ikilinganishwa na mwaka 2024, huku kiwango cha kutokubaliwa kikipanda hadi asilimia 48. Wakati huo huo, kiwango cha kukubaliwa kwa uongozi wa kimataifa wa China kiliongezeka kwa kasi kutoka asilimia 32 hadi 36. Jambo linalofuatiliwa zaidi ni kwamba katika nchi 23, kiwango hicho cha China kilipata ukuaji wa zaidi ya asilimia 10, ikiwa ni pamoja na washirika wa jadi wa Marekani ikiwemo Uingereza, Uhispania, Italia, na Ireland.

Katika miaka ya hivi karibuni, taswira ya kimataifa ya Marekani imeharibika kutokana na vitendo vyake vya upande mmoja. Kutoka kujiondoa kwake mara kwa mara kwenye mashirika ya kimataifa, hatua za kijeshi dhidi ya nchi huru zikiwemo Iran na Venezuela, hadi sera zake zisizo thabiti za ushuru, vitendo vingi vya Marekani vimekiuka sheria za kimataifa. Hata nchi washirika wake wa muda mrefu zinaanza kutathmini upya uhusiano wao na Marekani. Uchunguzi unaonesha kwamba kiwango cha uongozi wa kimataifa wa Marekani kukubaliwa na Wajerumani kilishuka kwa asilimia 39, wakati huo huo kiwango hicho na Wareno, Wacanada, Waingereza, na Waitalia pia kilishuka kwa kiasi kikubwa.

Kinyume chake, uwezo wa uongozi wa kimataifa wa China unaonesha kiwango cha juu cha uhakika na utulivu. Kwa muda mrefu, China imekuwa kama mjenzi wa amani ya dunia, mchangiaji wa maendeleo ya kimataifa, na mtetezi wa utaratibu wa kimataifa. Kupitia mifumo ya ushirikiano ya pande nyingi ikiwemo pendekezo la “Ukanda Mmoja, Njia Moja” na pendekezo la maendeleo ya kimataifa, China imetoa majukwaa mengi ya ushirikiano wa kimataifa na kikanda katika nyanja mbalimbali ikiwemo miundombinu, biashara, uwekezaji, na kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi, na kukaribishwa na nchi mbalimbali duniani haswa nchi za kusini.

Gallup imechambua ikisema matokeo ya uchunguzi wake yanaonesha kuwa katika miongo miwili iliyopita, dunia inaelekea kuwa na ncha nyingi, na nchi nyingi zikiwemo nchi washirika wa Marekani zinapenda kudumisha uwiano katika mahusiano yao na nchi kubwa duniani. Dunia haipendi kushuhudia migogoro ya nchi kubwa, bali inatumai kuwepo kwa amani, utulivu na maendeleo ya pamoja.
 
Huo uchunguzi hauna maana yoyote ni siasa tu hizo. China ni taifa ambalo kuwa kwake juu hakuwezi kuwa na manufaa yoyote kwa dunia hii hasa mataifa machanga yataumia sana.
 
Back
Top Bottom