China yaongoza duniani katika utengenezaji na uuzaji wa mabasi ya abiria

China yaongoza duniani katika utengenezaji na uuzaji wa mabasi ya abiria

Family ya ndege unamaanisha nini chifu?
Sasa wewe na ki C919 utashindana na mizigo hii?


Halafu ki C919 kinategemea Western technology!

d0334860-6c37-4af7-b20e-4b91e328f3f0_91ff9b87.jpg
 
Kwa miaka 9 mfululizo kampuni ya Yutong ya China imekuwa kinara kwa kuuza mabasi mengi zaidi duniani.

Utengenezaji na uuzaji wa mabasi ya abiria imekuwa biashara kubwa yenye ushindani hasa mabasi ya umeme. Mabasi yamekuwa yakitengenezwa kwa kazi na makusudi tofauti tofauti.

Kinachoangaliwa katika ushindani wa biashara hii ni idadi (units) za mabasi ambazo makampuni katika nchi husika yameuza.

Ifuatayo ni 10 bora ya majina ya makampuni yaliyouza mabasi mengi zaidi duniani mwaka 2022 na idadi ya mabasi yaliyouzwa;

(1)YUTONG (China) – 58,688
View attachment 2679250


(2)DIAMLER (Ujerumani) – 32,612

View attachment 2679307

(3)KING LONG (China) – 26,450
View attachment 2679303

(4)GOLDEN DRAGON (China) – 19,392
View attachment 2679306

(5)MARCOPOLO S.A (Brazil) – 15,831
View attachment 2679298

(6)ZHONGTONG (China) – 15,054
View attachment 2679295

(7)MAN (Ujerumani) – 13,972
View attachment 2679308

(8)HIGER (China) – 11,412
View attachment 2679302

(9)VOLVO (Sweden) – 9,731
View attachment 2679309

(10)SCANIA (Sweden) – 7,777
View attachment 2679310

Katika tatu (3) bora duniani, makampuni matano ya China yameongoza kwa pamoja yaliuza mabasi 130,996, ikifuatiwa na makampuni mawili ya Ujerumani yaliuza jumla ya mabasi 46,584 na Sweden mabasi 17,148

REKODI YA CHINA KATIKA BIASHARA YA MABASI
●Kwa miaka 9 mfululizo kampuni ya Yutong ya China imekuwa kinara kwa kuuza mabasi mengi zaidi duniani.

●China ndilo taifa linalouza karibu asilimia 50 ya mabasi katika soko la dunia.

●China inaongoza kwa kutengeneza mabasi yasiyotumia mafuta (new energy vehicle) Asilimia 90 ya mabasi ya umeme duniani ni yaliyotengenezwa na makampuni ya China.

●Youngman ndilo basi kubwa zaidi lililovunja rekodi duniani lenye urefu wa mita 25 lenye uwezo wa kupakia abiria 300. Lilipewa jina la utani triple bus. Lilitengenezwa na kampuni ya China Youngman Automobile Group Co., Ltd.

View attachment 2679287

●China ndilo taifa pekee duniani lenye viwanda 16 vikubwa vya kutengeneza mabasi; Yutong, Higer, Zhongtong, Kinglong, JMC, Foton, BYD, Golden Dragon, Asia Star, Ankai, Changan, Dongfeng, Nanjing Iveco, Briliance Renault, Sunwin na Sunlong.

Hivi tofauti ya bei ya hayo mabasi ni hipi eg, hayo ya kichina, kisweden, kijerumani na kibrazil?
 
Kwa hiyo wewe Mtanzania umezubaa kusubiria tech za Ulaya

Wenzetu huko Japan, South Korea, China, India, Hong Kong, Taiwan, Singapore wanafanya innovation

Leo wazungu wakienda China wanabaki kushangaa jinsi ambavyo Mchina yuko na advanced technology na cross cutting technology kuzidi hata nchi za Ulaya na Marekani katika baadhi ya fields of sci & tech
Sasa wewe tangu uzaliwe unakula ugali na maharage halafu unategemea kufanya innovation, mzee upo serious kweli ?
 
Sasa wewe tangu uzaliwe unakula ugali na maharage halafu unategemea kufanya innovation, mzee upo serious kweli ?
Wenzetu hawajalala wanaumiza vichwa wajitegemee kiteknolojia

Badala ya kuwaponda ni bora tuone tunajifunza nini kutoka kwao wamefikaje hapo ni strategies na policies gani walitumia

Japan, South Korea na China ni nchi nazikubali sana kwa innovation tuna ya kujifunza kutoka kwao
 
Iyo Diamler moja ya Ujerumani unanunua youtong ngapi?

Ukute aliyepiga pesa ndefu ni iyo kampuni ya Diamler ya Germany japo kwa idadi yupo nyuma ya Youtong.
Vijana mjifunze masuala ya biashara

Ukielewa profit inavyopatikana hautakurupuka na kusema Diamler kapiga hela zaidi ya Yutong kwa sababu chuma zake zina bei kuzidi Yutong

Hizo ni hesabu za mtu asiyejua biashara
 
Katika utengenezaji wa ndege hili ni jambo la kawaida hakuna kampuni inayotengeneza parts zote za ndege

Hata Airbus na Boeing hununua kutoka makampuni mengine parts
Najua ila kiasi kikubwa cha crucial parts wananunua. Na point muhimu ni kuwa kidege kimoja hakiwezi ku challenge Boeing au Airbus domination. West wakitia ngumu hakiruki.
 
Najua ila kiasi kikubwa cha crucial parts wananunua. Na point muhimu ni kuwa kidege kimoja hakiwezi ku challenge Boeing au Airbus domination
Boeing alikuwa mbele ya Airbus kwenye mauzo ya ndege ila sasa hivi kapitwa na Airbus so kwenye biashara inawezekana
 
Wenzetu hawajalala wanaumiza vichwa wajitegemee kiteknolojia

Badala ya kuwaponda ni bora tuone tunajifunza nini kutoka kwao wamefikaje hapo ni strategies na policies gani walitumia

Japan, South Korea na China ni nchi nazikubali sana kwa innovation tuna ya kujifunza kutoka kwao
Mnatakiwa ku improve lishe za watoto wenu wa kiafrika, la sivyo innovation mtaishia kuzisikia kwa wenzenu Ulaya na Asia.
 
Back
Top Bottom