China yaongoza duniani katika utengenezaji na uuzaji wa mabasi ya abiria

China yaongoza duniani katika utengenezaji na uuzaji wa mabasi ya abiria

Kwa miaka 9 mfululizo kampuni ya Yutong ya China imekuwa kinara kwa kuuza mabasi mengi zaidi duniani.

Utengenezaji na uuzaji wa mabasi ya abiria imekuwa biashara kubwa yenye ushindani hasa mabasi ya umeme. Mabasi yamekuwa yakitengenezwa kwa kazi na makusudi tofauti tofauti.

Kinachoangaliwa katika ushindani wa biashara hii ni idadi (units) za mabasi ambazo makampuni katika nchi husika yameuza.

Ifuatayo ni 10 bora ya majina ya makampuni yaliyouza mabasi mengi zaidi duniani mwaka 2022 na idadi ya mabasi yaliyouzwa;

(1)YUTONG (China) – 58,688
View attachment 2679250


(2)DIAMLER (Ujerumani) – 32,612

View attachment 2679307

(3)KING LONG (China) – 26,450
View attachment 2679303

(4)GOLDEN DRAGON (China) – 19,392
View attachment 2679306

(5)MARCOPOLO S.A (Brazil) – 15,831
View attachment 2679298

(6)ZHONGTONG (China) – 15,054
View attachment 2679295

(7)MAN (Ujerumani) – 13,972
View attachment 2679308

(8)HIGER (China) – 11,412
View attachment 2679302

(9)VOLVO (Sweden) – 9,731
View attachment 2679309

(10)SCANIA (Sweden) – 7,777
View attachment 2679310

Katika tatu (3) bora duniani, makampuni matano ya China yameongoza kwa pamoja yaliuza mabasi 130,996, ikifuatiwa na makampuni mawili ya Ujerumani yaliuza jumla ya mabasi 46,584 na Sweden mabasi 17,148

REKODI YA CHINA KATIKA BIASHARA YA MABASI
●Kwa miaka 9 mfululizo kampuni ya Yutong ya China imekuwa kinara kwa kuuza mabasi mengi zaidi duniani.

●China ndilo taifa linalouza karibu asilimia 50 ya mabasi katika soko la dunia.

●China inaongoza kwa kutengeneza mabasi yasiyotumia mafuta (new energy vehicle) Asilimia 90 ya mabasi ya umeme duniani ni yaliyotengenezwa na makampuni ya China.

●Youngman ndilo basi kubwa zaidi lililovunja rekodi duniani lenye urefu wa mita 25 lenye uwezo wa kupakia abiria 300. Lilipewa jina la utani triple bus. Lilitengenezwa na kampuni ya China Youngman Automobile Group Co., Ltd.

View attachment 2679287

●China ndilo taifa pekee duniani lenye viwanda 16 vikubwa vya kutengeneza mabasi; Yutong, Higer, Zhongtong, Kinglong, JMC, Foton, BYD, Golden Dragon, Asia Star, Ankai, Changan, Dongfeng, Nanjing Iveco, Briliance Renault, Sunwin na Sunlong.
Hizo namba ni uuzaji nje ya nchi husika au ni pamoja na mauzo ndani ya nchi inayotengezeza mabasi hayo. Unaweza kukuta Yutong inajumuisha mabasi yote yaliyouzwa ndani ya China ambayo yatakuwa mengi sana kuliko yaliyouzwa nje lakini siyo reflection ya competitiveness. Wachina wanapenda kununua vitu vya China na serikali inatoa ruzuku kubwa kwenye bei za bidhaa zilizotengenezwa China
 
Tunasema mchina ana copy sana kwa sababu zifuatazo:





Naweza kutoa mifano mingi tu. Nenda kariakoo uone copycats kibao za wachina.
 
Nimeona katarama polo g7 aiseee hio gari ni balaaa kwa michina inayokuja Africa sijaona wa kukaa mbele

Mchina lazima akimbize sababu kuu ni magari yake yanakaa mda kidogo yanachoka

Sema kuvuta IRIZAR I8 route za dar mwanza ni matumizi mabaya ya akili
Watu wanaongea tu, ukizungumzia durability mzungu kitu kingine.
 
Mabasi ya kichina ni kwa kuwa wafanyabiashara wanayaleta maana bei chee na hivyo wanapata faida mapema but quality wise hayawezi shindana na western hata kidogo. Kwa kifupi mchina kuuza sana wala si ajabu maana bei za bidhaa zake zipo chini sababu ya cheap labour na kutumia raw material za ubora wa kawaida au chini. Ndiyo maana hata company nyingi za europe na US wanaviwanda china sababu ya cheap labour. Iko wazi kabisa hata kariakoo tecno na nduguze utakuta wanauzika sana kuliko I phone au samsung sasa check ubora wa tecno na samsung au i phone ardhi na mbingu[emoji1787][emoji23] simu ya kichina warranty miezi 12+1 wakati brand zinazoeleweka warranty 2 years! Kwa kifupi kinachombeba mchina ni bei chee.
Nilisema hapo juu, product za ulaya unaweza kukaa nazo mpaka 10 years, ikitokea shida ni repairs za kawaida tu. Hamna mchina anayeweza kaa miaka hata 3 bila kumuweka chini. Atakusumbua saaana, kwa simu mimi hapa nna samsung s3 ipo kabatini ni nzima kabisa, simu ya miaka mingi saana, kuna tecno kadhaa za 2019, 2020 zipo kwa fundi.
 
Hizo namba ni uuzaji nje ya nchi husika au ni pamoja na mauzo ndani ya nchi inayotengezeza mabasi hayo. Unaweza kukuta Yutong inajumuisha mabasi yote yaliyouzwa ndani ya China ambayo yatakuwa mengi sana kuliko yaliyouzwa nje lakini siyo reflection ya competitiveness. Wachina wanapenda kununua vitu vya China na serikali inatoa ruzuku kubwa kwenye bei za bidhaa zilizotengenezwa China
Units exported mkuu China inaongoza
 
hilo lipo wazi sana mkuu western ni wavumbuzi then mchina kwa kuwa ana cheap labour plus kutumia raw material za ubora wa chini au kawaida automatically anaonekana ameuza sana sokoni! Au makampuni ya western yanapotaka kupunguza gharama za uzalishaji ndipo yanaenda china. Ndiyo maana kila kinachogunduliwa na western baadae unakuta mchina huyu hapa anauza kwa wingi. Hayo mabasi, malori, na vingine vingine ni copy paste ya western tech, ndiyo maana unakuta imeanza insta china kakopy ana tiktok[emoji1787] sijui western wapo na watsapp china ana wechat[emoji1787], western ana ebay na amazon china ana alibaba[emoji1787] . R&D za universities za western au makampuni ya US ni balaaaaa. R&D za kampuni za kichina mainly hulenga kupunguza gharama, na kuangalia alternative raw materials ili gharama ishuke then wapate kushindana na bidhaa za western[emoji1787][emoji1787][emoji1787]
Wazungu wana iphone wao wakaleta oppo, yaani wakalenga mulemule kwa wenzao, zikaja tec za kadhaa nyingi za simu, jamaa wakawa wanapita mule mule. Wachina wana youtube yao pia.

Ni ngumu sana na kutowatendea haki Ulaya kuwapambanisha na China. Leo tupo hapa JF, tunatumia net, computer n.k sababu ya Tec za ulaya
 
Wazungu wana iphone wao wakaleta oppo, yaani wakalenga mulemule kwa wenzao, zikaja tec za kadhaa nyingi za simu, jamaa wakawa wanapita mule mule. Wachina wana youtube yao pia.

Ni ngumu sana na kutowatendea haki Ulaya kuwapambanisha na China. Leo tupo hapa JF, tunatumia net, computer n.k sababu ya Tec za ulaya
Kwa hiyo wewe Mtanzania umezubaa kusubiria tech za Ulaya

Wenzetu huko Japan, South Korea, China, India, Hong Kong, Taiwan, Singapore wanafanya innovation

Leo wazungu wakienda China wanabaki kushangaa jinsi ambavyo Mchina yuko na advanced technology na cross cutting technology kuzidi hata nchi za Ulaya na Marekani katika baadhi ya fields of sci & tech
 
Polo ni balaa kubwa ila ndio hivyo mchina anachange dizaini kila leo

Wabongo wengi ni washamba hawajui vitu quality

Ruti ya mwanza-dar nilikua napenda kupanda ally's juzi hapa nimepanda katarama aiseee msweedeni ni umeme
Mkuu achana na mzungu, product zao ni jiwe haswa. Hii hata madereva wenyewe wanalijua, abiria anafurahi tu yale mazingira ya mule ndani lakini nje ya hapo kwa anayejua gar, Bus za ulaya ni mziki mnene.
 
Kwamba ni suala mda unamaanisha nini? Mimi nimekwambia kitu nilichoshuhudia mwenyewe hauwezi ukaweka michina na polo g7[emoji3][emoji3] kwa kila kitu

Hio katarama sijui ina mda gani barabarani ila ukikaa kwenye siti yake utanielewa ni nini namaanisha
Hizi ni gar mbili tofauti, comfortability ya Scania na mchina aina yoyote ile ni tofauti.
 
Back
Top Bottom