China yasema ipo tayari kuharibu uhuru wa Taiwan kwa njia yoyote

Hawa china na wao waache domo badala yake waishike taiwan mara moja kijeshi. Makubaliano na marekani kwamba hawatatumia nguvu wakati wao mamarekani wanaendelea kuwatia kichwa mabwanyenye na mabepari wa taiwan hayana maana.
Tofaiti na uvamizi wa urusi ukraine dunia nzima na umoja wa mataifa wanatambua taiwan kama sehemu ya china.
 
Suluhisho ni China kutumia demokrasia sio nguvu, hata mimi siwezi kubali kufungiwa. Either wakae hivihivi au waungane kwa amani sio vita otherwise ikitokea matokeo ni baadae
 
Kumbe mnafahamu matatizo yenu ambayo ndio kikwazo kwenu.

Jengeni bara lenu na nchi zenu hayo mataifa ya magharibi yatakuja tu huko.

Masuala ya China hauna ufahamu nayo licha ya kuwa una lazimisha uone unafahamu.
Si Bora sisi tuna AMANI uhuru na UWEZO wa kuichalenji SERIKALI nyinyi kwenu hamna uhuru hata wa kumiliki Ardhi.
Wachina wengi sana wanamalalamiko kwenye local government zao. Uchumi wenu ni bosheni, kilichotajirika ni chama na sio wachina wenyewe.

Takwimu zenu zinaonesha more than 600milions Chinese wanalipwa $150 kwa mwezi na kwa sasa hii hela haipo kabisa kutokana na wimbi la unemployment.

Utajiri ambao hauna manufaa yoyote kwa raia Bali unakitajirisha chama hauna manufaa yoyote
 
Suluhisho ni China kutumia demokrasia sio nguvu, hata mimi siwezi kubali kufungiwa. Either wakae hivihivi au waungane kwa amani sio vita otherwise ikitokea matokeo ni baadae
Peaceful unification ipo proposed toka 1970s

Deng akaleta suala la One country two systems.

General secretary Jiang, Hu, Xi mpaka sasa msimamo ni peaceful unification kwa makubaliano ya pande zote PRC haina muda wa kutaka kuitawala ROC kimabavu kama inavyo zungumzwa huko nje.

Matumizi ya nguvu ni matokeo ya mwisho pale itakapo onekana kuna kila juhudi za kutaka kuiweka mbali zaidi Taiwan kutoka China I mean kuitenga Taiwan na China na kuanzisha taifa lao.

Pande zote mbili PRC na ROC kwa wakati mbalimbali wamekuwa wakiimarisha ushirikiano katika masuala mbalimbali toka miaka ya 1990s ili kudhibiti hali ya kutokea vita baina yao.

Jambo lililo baki ndani ya ROC yenyewe misimamo baina ya KMT na DPP kuhusu uhusiano na mainland na position ya ROC kimataifa.
 
Uhuru na amani mnayo. Je maendeleo bora mnayo au kwenu sio vitu vya msingi ?
 
Uhuru na amani mnayo. Je maendeleo bora mnayo au kwenu sio vitu vya msingi ?
Maendeleo tunayo tena maendeleo yenye AMANI, maendeleo yenu hayana AMANI,

Sasahivi tunavyoongea China vijijini wakulima wanalazimishwa Kukata mazao yao na kubadilisha mazao yao na maeneo yao kupanda mpunga

Malalamiko yamekuwa mengi imefikia mpaaka wanakijiji wanaua wafanyakazi wa selikari.

Maendeleo gani sasa hayo?
 
Kumbe mnafahamu matatizo yenu ambayo ndio kikwazo kwenu.

Jengeni bara lenu na nchi zenu hayo mataifa ya magharibi yatakuja tu huko.

Masuala ya China hauna ufahamu nayo licha ya kuwa una lazimisha uone unafahamu.
Ngoja nikuachie wewe huo ufahamu. Maana mimi sioni sifa, sifukuzane na aliyekwapua taulo langu.
 
Kama urussi aliyebaba wa nishati duniani kachemka sembuse mchina
?
China ina industrial supplies, Hana natural resources muhimu Kwa Dunia atakalishwa faster.

Hana gesi, hana mafuta....atakalushwa mapema kwa vikwazo
Urusi kachemka kivipi kashajichukulia maeneo ya kutosha
 
Nonsense hicho kisiwa china anawez kukizunguka pande zote bila shida
 
China anaongea tu lakini hawezi nusa hapo Taiwan. Watu watarusha vyuma mpaka hapo China.
Najua vita haiwezi kutokea

Ila kinadharia ni kwamba hayo mataifa yataishia tu kuipa msaada wa kijeshi na silaha Taiwan na labda kuunga mkono vikwazo vya kiuchumi kwa China

Ila suala la kusema wataishambulia au kuivamia China hilo haliwezi kutokea
 
Urusi kinatokea nini? Ameshashika zaidi ya 25% ya ardhi ya Ukraine. Uchumi wake umekua toka alipoivamia Ukraine... mauzo ya mafuta ndio yamepamba moto, ulaya wanalazimika kununua kupitia mtu kati kwa bei juu.. hivi hua mnafanya utafuti hata kdg?
 
Sikatai lakini wachina wanageuza nchi za watu jalala nenda karikoo uone takataka zao sijui hata wakaguzi wanakuwa wapi kuruhusu baadhi ya vitu
Ndio hizo takataka za wachina mnazoweka store halafu wahuni wa TRA wanawataka mzilipie kodi.
 
Tunaona selikari ya China inavyohaha kuimarisha mahusiano na USA kwa kuiomba mazungumzo hivi majuzi coz wanajua bila soko la Marekani na Europe hakuna China anymore wanalijua hilo
Labda watawauzia Urusi, Iran
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…