China yasema ipo tayari kuharibu uhuru wa Taiwan kwa njia yoyote

Iweje anashindwa penyeza watu wake pale?
 
Kuna vitu vinachekesha na kutafakarisha sana hapa duniani

Taiwan kudai aachwe huru asiwe upande wa China anaonekana yupo sawa na Marekani plus Europe wanaungana kumtetea

Ila yale majimbo ya Ukraine ambayo raia wake wengine wameungana na Urusi kupambania uhuru wao wanaonekana wanakosea sana

Hapa naona mchina anatafutwa ili apunguzwe nguvu za kiushawishi na kiuchumi duniani.
 
Iweje anashindwa penyeza watu wake pale?
Anajaribu ila wale wenzetu sio wajinga kama sisi bara letu. Uchaguzi mkuu wa Taiwan huwa China inakuwa concerned mno, tatizo wananchi wa Taiwan hawataki kuwekwa chini ya mwavuli wa chama kimoja, mkono wa chuma na kufungwafungwa kama Wachina. Sijawahi ona watu wenye freedom wakaikataa wakataka kubanwa. GDP per capita, economic freedom, civil rights vyote Taiwan inaizidi China
 
Basi ikitokea wakavamiwa Taiwanese wengi watapelekwa concentration camps
 
Kinachofanya China asiivamie mpaka saivi ni nn?

Mzee hii ishu sio rahisi kama unavyofikiria.

Ungejua yanayoendelea China main land usingeongea haya.

Migomo ya mara kwa mara, watu wanakatwa pesa Zao za mishahara na pensheni bila sababu hivyo vitu China saivi vimekuwa ni vya kawaida.

Maswala ya vita huwa hayana prediction, unaweza kuwaza Hivi halafu mambo yote yakaenda tofauti kabisa na unavyowaza.

Jeshini tu PLA la uchina Kuna tatizo rushwa lililo kithiri, unajua hadi vyeo vya kijeshi China watu wananunua? Sasa hiyo ni mbaya sana na inashusha morali.

Kwa kifupi China ina mapungufu mengi sana, nakushauri watafute wachambuzi wa maswala ya Geopolitics Mr. George G Chong na Mr Peter Zein wasikilize hao jamaa wameishi China na Hong Kong for more than 25 years wamezunguka China main land kwenye makampuni ya selikari ya China na private wanachambua vizuri sana madhaifu ya China.

Huu mgogoro kwa kifupi utaleta matokeo mabaya sana kwa China.
 
Ni kosa kudai uhuru wa Taiwan kutoka China iwe ndani ya Republic Of China au People's Republic Of China.

Visiwa vya Taiwan ni sehemu ya Uchina
Jitafakari kichwan mwako , kuna element za umilembeb, South Sudan kudai uhuru ni sawa ila Taiwan kudai uhuru sio sawa
 
Taifa lako lingepata kuwa nafasi ya China sioni kama ungeunga mkono harakati hizo.
Hii comment yako inaonesha uchiz wko , kwamba unaunga mkono sababu wew taifa lako ni sehem ya China? Kwan usiseme kuwa sehem ya Taiwan ? Swala la kujitenga huamuliwa na wakaz wa eneo husika , je kwann China mainland inang'ang'ania umoja wkt Taiwan hatak umoja na hawafanani kila kitu sio sera za kiuchumi wala sera za kisiasa , na ww kilaza unaunga mkono uwaweke Taiwan pamoja na nchi isiyo na uchaguz wenye haki kwa kila mchina yaan kati ya wachina 1B rais anachaguliwa na watu elf 3 tu na wewe ndo unataka Taiwan aingie kweny huo uzuzu?
 
Republic Of China haiwezi kuwa chini ya CPC. Hakuna mahali imetamkwa hivyo.
Kwamba huyo Xi Jinpin ana edit katiba ili abakie madarakan ndo ajirekebishe baada ya kuwa ndan ya Republic , kwamba wataiwan chini ya 90m anawaheshimu kuliko wachina 1B?
 
Una andika maneno mengi yasiyo na faida na mahusiano na suala la Taiwan

Tabiri zako kuhusu serikali ya China na CPC hazina maana.
Hizi stress za maisha zitawaua vijana wa dar , unaililia China kuzid bara lako la afrika
 
Hizi stress za maisha zitawaua vijana wa dar , unaililia China kuzid bara lako la afrika
Sio mtanzania, Huyu ni mchina kama ulikuwa hujui

CCP ina kitengo cha propaganda kipo maalumu kueneza habari za propaganda za CCP duniani.

Huyo jamaa kasomea kiswahili maalumu kabisa kwa kazi hii ya kugeuza fikra za waTanzablnia na jamii zingine zinazozungumza kiswahili
 
Marekani inachochea vita
 
Urusi kumetokea nini?
Unaongea km umekatwa kichwa.
Wayukren wapo kwenye shida sababu ya viburi vya hao wamarekani wewe unatuletea porojo za Hollywood?
Hao jamaa USA wanaipeleka Dunia kubaya
 
Urusi kumetokea nini?
Unaongea km umekatwa kichwa.
Wayukren wapo kwenye shida sababu ya viburi vya hao wamarekani wewe unatuletea porojo za Hollywood?
Hao jamaa USA wanaipeleka Dunia kubaya
Wa Ukraine wanayapigania maeneo yao,
they are fighting for their sovereignty...

Hakuna taifa litakubali taifa lingine liingilie maeneo yao
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…