Embu tusubiri tuone.Hata Russiana uwa anaingiza figher jet kwenye anga la UsA pia Us.A kwa Russia uwa wana zi nchi husika inatuna ndege kuzionya.
Ila kijiografia na military assets China ilizonazo mh ngojea tuone.
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Embu tusubiri tuone.Hata Russiana uwa anaingiza figher jet kwenye anga la UsA pia Us.A kwa Russia uwa wana zi nchi husika inatuna ndege kuzionya.
si mara 1 hata mwaka jana tai wa Us waliruka ndani ya anga la china na hakuna kilichotokea.. mnachokiandika hapa wachina wenyewe wanawashangaAnaweza akaingiza 1 wakiishtukia wanatuma ndege inawaelekeza kugeuza ila sio hii ya kuingiza madege yote hayo.....ukifanya hivyo kwa taifa lenye msuli hapo ushamaanisha unataka vita....na hiko ndo kitu china anakitaka anasubiri upande wa pili wa jibu ....na wao wapeleke za kwao kwake au watume tu hata ka roketi kuelekea china ili na wao wajibu
Kwani Taiwan ni mwanachama wa NATO?Ukraine sio mwanachama wa Nato........angalia vizuri historia ya Crimea ilikuwaje ikawa sehemu ya Ukraine na raia wa hapo wengi wana asili ya wapi utaona kwanini ilikuwa rahisi kwa Urusi kuichukua kibabe.
Nilimsahihisha aliyesema Ukraine yupo NATO.Kwani Taiwan ni mwanachama wa NATO?
Zilikua ndege ngapi na UCHINA aliingiza ndege ngapi TAIWAN kwakitendo cha UCHINA kuingiza ndege zake hizo aloingiza TAIWAN lilikua tangazo rasmi la VITAsi mara 1 hata mwaka jana tai wa Us waliruka ndani ya anga la china na hakuna kilichotokea.. mnachokiandika hapa wachina wenyewe wanawashanga
View attachment 1964262
insu ni ndege kuruka ndani ya anga la china na sio idadi.Zilikua ndege ngapi na UCHINA aliingiza ndege ngapi TAIWAN kwakitendo cha UCHINA kuingiza ndege zake hizo aloingiza TAIWAN lilikua tangazo rasmi la VITA
US hata kaa athubutu kupeleka idadi hio ya ndege UCHINA ama URUSI halaf vusitokee vita tena sio URUSI na UCHINA hata IRAN hawezi akawafanyia huo UPUUZI walofanziwa TAIWAN na UCHINA ila TAIWAN hawakua na lakuifanya UCHINA
Nilishasoma tena labda ulikuwa hujazaliwa.Kasome hiyo vita vizuri halafu urejee hapa useme kuwa hakuna kilichomkuta.
Kama hakuna kilichomkuta basi maeneo yaliyokaliwa na N.K kwa mabavu yangerudi.
Basi kaa utambue ukweli usiendekeze ushabiki.Nilishasoma tena labda ulikuwa hujazaliwa.
Hii kwa mujibu wako wewe sio china...maana hakuna sehemu yoyote serikali ya china imesema kama ulichokisema hapa...Anachoona China ni kwamba akichelewa Taiwan itazidi kujiimarisha na silaha za Marekani.
Pia akiwahi kuivamia kuna uwezekano likawa ni jambo la hatari linaloweza kuiyumbisha China kwa kiwango kikubwa, ila kuna option wanayo ya kuwahi kuibeba taiwan huku wakiwa tayari kuingia vitani na Amerika pale itakapobidi.
Option hii hata Amerika anaiogopa maana itamgarimu kwa kiwango kilekile itakavyoigarimu China.
Naweza kukwambia Taiwan haitomaliza miaka 10.
Baadhi yetu humu tutalishuhudia hili! China yupo tayari kwa 100% hata kuiingiza dunia vitani kwaajili ya Taiwan kuliko Marekani ilivyo tayari kusimama na Taiwan kwa 100%
Inawezekana upo usingizini[emoji3]Kwa sasa China imeimarika kijeshi, kitecnologia huku Marekani ambaye ndio anaipa kiburi Taiwan akiwa anazidi kukosa ushawishi duniani. Pia maadui wa Marekani wamepata nguvu na wanazidi kupata nguvu siku hadi siku... Kibaya zaidi maadui wa Marekani wanashirikiana na China.
Huhitaji akili kubwa kutambua hili... Wakati ni sasa
Walianza lini kuwa na roho ya hivi wakati Mjapani alishambomoa vibaya sana kwenye vita?Sawa mkuu... Kama tungefahamiana ningekukumbusha wakati ukifika.
Wachina ni nyoko! Wapo tayari hata wafe milioni 500 lakini wahakikishe wanalinda heshima yao na adui amesalimu
💨 Leo Taiwan imeripoti kuwa Ndege 9 za China zimeingia kwenye anga lakeTaiwan inasema imeshuhudia ndege 38 zikiingia kwenye eneo lake la ulinzi
2 Oktoba 2021
![]()
Uvamizi huo wa Ijumaa uluihusisha ndege za kivita aina ya jet J-16 jets (kama zinavyoonekana kwenye picha hii ya maktaba), Taiwan imesema
Taiwan imeripoti kuwa ndege za kijeshi za Uchina 38 zimepaa na kuingia eneo lake la ulinzi la anga siku ya Ijumaa- ukiwa ni uvamizi mkubwa zaidi kuwahi kufanywa na Beijing hadi leo.
Wizara ya ulinzi ilisema kuwa ndege hizo, ikiwa ni pamoja na zana zenye uwezo wa kulipua mabomu, ziliingia katika eneo hilo kwa awamu mbili.
Taiwan ilijibu kwa kuzuwia haraka uvamizi huo kwa jeti zake na kutuma mifumo yake ya makombora angani.
China inaiona Taiwan yenye demokrasia kama jimbo lililojitenga, lakini Taiwan inajiona kama taifa huru.
Taiwan imekuwa ikilalamika kwa zaidi ya mwaka mmoja juu ya harakati za kijeshi za mara kwa mara za vikosi vya anga vya China karibu na kisiwa hicho.
"China imekuwa ikifanya uchokozi wa kijeshi, na kuharibu amani ya eneo ," Waziri mkuu wa Taiwan Premier Su Tseng-chang aliwaambia waandishi Jumamosi.
Serikali ya Beijing - ambayo inaadhimisha miaka 72 tangu kuanzishwa kwa Jamuhuri ya watu wa China- hadi sasa haijatoa kauli yoyote kuhusu tukio hilo.
Lakini awali ilisema kwamba safari kama hizo za anga zilikuwa ni za kulinda nchi na pia yalilenga "njama "baina ya Taiwan na Marekani.
Katika taarifa yake, wizara ya ulinzi ya Taiwani ilisema kuwa ndege 25 za kikosi cha jeshi la People's Liberation Army (PLA) ziliingia katika eneo la kusini -magharibi kama sehemu ya vikosi vya ulinzi ya utambuzi wa eneo (ADIZ) wakati wa saa za mchana, na kupaa karibu na visiwa vya Pratas.
Eneo la utambuzi wa kijeshi ni eneo lililoko nje ya eneo la nchi na ni eneo la anga la kimataifa - lakini ni eneo ambalo ndege ya kigeni bado inatambuliwa, kufuatiliwa, na kudhibitiwa kwa maslahi ya usalama wa taifa.
Ni eneo linalojitangaza na kiufundi linasalia kuwa eno huru la anga la kimataifa.
hii ilifuatiwa na wimbi la pili la ndege 13 za China katika eneo hilo hilo Ijumaa jioni. Zilipaa juu ya maji kati ya Taiwan na Ufilipino
![]()
Wizara ilisema kuwa ndege ya Kichina zilikuwa pamoja na zana za mabomu nne aina ya H-6 , ambazo zina uwezo wa kufanya mashambulio ya silaha za nyuklia, pamoja na ndege ya kuzuwia mashambulio yanayotoka kwenye manuari za kijeshi.
Mara kwa mara Beijing hufanya uvamizi wa aina hiyo kuelezea kutofurahishwa kwake na kauli zilizotolewa na Taiwan.
Haijafahamika nini kilichopsababisha uvamizi wa hivi karibuni
Maelezo zaidi juu ya mzozo baina ya Taiwan na China
Yapi maoni yako?
- Kwanini China na Taiwan zna uhusiano mbaya? China na Taiwan ziligawanyika tangu vilipotokea vita vya wenyewe kwa wanyewe katika miaka ya 1940, lakini Beijing inasisitiza kuwa kisiwa hicho kitarejeshwa kwake wakati mmoja, kwa nguvu iwapo itakuwa lazima.
- Taiwan inatawaliwa vipi? Kisiwa hicho kina katiba yake, viongozi waliochaguliwa kidemokrasia, na takriban wanajeshi 300,000 na vikosi vya usalama.
- Nani anaitambua Taiwan? Ni nchi chache tu zinazoitambua Taiwan. Wengi wanaitambua serikali ya Beijing badala yake. Marekani haina uhusiano rasmi na Taiwan lakini ina sheria inayoipasa kuipatia uwezo wa kujilinda
Maoni ya serikali ya Taiwan
China huenda ikawa na uwezo wa kuishambulia Taiwan kufikia 2025’ Waziri wa Ulinzi
Uhusiano wa kijeshi na China ni mbaya zaidi katika miaka 40, waziri wa ulinzi wa Taiwan amesema.
Chiu Kuo-cheng pia alionya China itakuwa na uwezo wa kukivamia kisiwa hicho ifikapo 2025.
Maoni yake yalikuja baada ya China kutuma "idadi kubwa " ya ndege za kijeshi katika eneo la ulinzi wa anga la Taiwan kwa siku nne mfululizo.
Taiwan inajiona kuwa nchi huru. Beijing, hata hivyo, inaiona Taiwan kama jimbo lake lililojitenga.
Haijafutilia mbali uwezekano wa matumizi ya nguvu kufanikisha kuungana na kisiwa hicho.
"Kufikia mwaka 2025, China itasongesha karibu uwezekano wa mzozo kamili. Ina uwezo sasa, lakini haitaanzisha vita kwa urahisi, ikizingatia mambo mengine mengi," Chiu Kuo-cheng alisema wakati kamati ya bunge Taipei ikiingatia muswada wa matumizi ya ulinzi wa mabilioni ya dola kujenga makombora na meli za kivita.
Taiwan ilijitenga na China bara wakati wakomunisti walipochukua madaraka mnamo 1949.
Wachambuzi wameonya kuwa Beijing inazidi kuwa na wasiwasi kuwa serikali ya Taiwan inaelekea kuafikia azimio rasmi la kujitangazia uhuru na inataka kumzuia Rais wake Tsai Ing-wen kuchukua hatua zozote katika mwelekeo huo.
Washirika kadhaa wa Magharibi wa Taiwan wameelezea wasiwasi wao juu ya onyesho wazi la China la nguvu zake za kijeshi katika siku za hivi karibuni.
Hata hivyo, Rais wa Marekani Joe Biden alisema mwenzake wa China Xi Jinping amekubali kutii "makubaliano ya Taiwan".
Bwana Biden alionekana kuashiria sera ya muda mrefu ya Washington ya "China moja" ambayo inaitambua China badala ya Taiwan.
View attachment 1965431
Marekani atashika namba 3 kwa usupapawa muda si mrefu 😊💨 Leo Taiwan imeripoti kuwa Ndege 9 za China zimeingia kwenye anga lake
Taiwan ni kisiwa kinachojitambua kama taifa huru ila China inasema ni jimbo lake na anairudisha kwenye himaya yake.
Marekani ndiyo huwa inaipa jeuri Taiwan ila China ishawahi muambia anacheza na moto.
Mnaanza wakivamia tukishangilia msije sema tunapenda vitaTaiwan haiwezi kuwa sawa na Crimea au Kashmir, ni ngumu kumezwa kwa nguvu bila kutokea madhara au uharibifu.