Nchi za Afrika hatuna budi kupeleka shukrani kwa Chinese...
China imetufungulia dunia, Infinix, Tecno, Xiaomi hizi piki piki n.k, ujenzi wa miundo mbinu na majengo mengi huku Africa, zana za kijeshi kama ndege na silaha, Tanzania ndege zetu zote za kijeshi ni Chinese halafu kuna watu wanawabeza...
Wazungu walikuwa hawana muda wa kufanya biashara na sisi, iPhone tunanunua si kwa ajili ya Africa huo ndio ukweli... China wamewatajirisha wafanya biashara wangapi pale Kariakoo?
China kaleta tik tok ku compete na IG,Youtube, Facebook... US kawafanyia roho mbaya... Huawei kaleta 5G US kashinikiza wenzie waisusie na si salama...
Leo hii unasema eti China bado Sana, don't you see wanavyoogopeka?
Hivi nyie pasipo gharama nafuu za ujenzi, mngekua mnaendesha gari kwenye vumbi bado ukweli mchungu, boda mnazopanda kila siku ni China huyo, ukifika kwako unawasha TV unakutana na China, ukiwasha iphone yako utumie ni assembled in China, ukishika simu uingie jf ni China, kwenye nguo na viatu ndipo usiseme kabisa... Ukiona hizo dalili ujue kabisa huyo ndio superpower mwenyewe kwamba humkimbii 😂😂😂
Mzungu alikuwa hana muda wa kufanya biashara na sisi , sisi kwao ni kama kima tu, mzungu alikuwa ana deal na Arabs na wazungu wenzie, Afrika kwa huu umasikini ilikuwa ngumu Sana kuweza kuendana na kasi ya dunia...
Kwa pamoja tuseme asanteni wa China...
Mchina kaifungulia dunia Afrika...,