Makachu
JF-Expert Member
- Aug 2, 2022
- 447
- 461
Nchi za Magharibi na USA/Marekani kwa ujumla kuna Dini au Raia wake wana dini na mbona sio Masikini?Sisi bado tunapigiana makelele usiku mzima watu hawalali mtaani, wanaopanga kwenda kazini asubuhi hawapati muda wa kulala sababu ya kelele za makanisa alaf ukiingia kanisani unakuta watu watatu tu. Waumini washakuwa masikini wakutupwa kwa kutajirisha wajanja wachache wanaomiliki kanisa.
Ukija kwa upande wa kobaz saa 10 asubuhi washaamshwa watu na maspika yao wahusika na wale ambao sio wahusika.
China wangefuata huu upuuzi wa kizungu na kiarabu mpaka leo nchi yao ingekuwa masikini. Maana wangekuwa wanalala makanisani kutoana mapepo yasioonekana, badala ya kutumia muda huo kulala viwandani kutengeneza utajiri wa raia mmoja mmoja na kukuza uchumi wa nchi.
Mtu kama masanja alieishia darasa la saba anapiga hela ndefu kutoka kwa waumini masikini, huku maprofesa wenye vyeti vyao wakishindia mihogo na maji ya kunywa.
Na pia Nchi za Kiarabu kama Qatar, Saudi Arabia na Iran kuna Dini na uchumi wao uko vizuri ukilinganisha na nchi nyingi za Afrika?
Nchi nyingi za Afrika Serikali zao hazina Dini bali Raia ndio wenye Dini. Hivyo kuwa mkweli kinacholeta umasikinini sio Dini(Uisilamu na Ukristo) bali ni Ubinafsi wa viongozi wa Kiafrika wakiongozwa na UFISADI pamoja na RUSHWA.
Ukisingizia Dini utakuwa unakosea kwa Maana China wana Dini zao pia za Kipagani lakini hazijawaletea umasikini. Na Halikadhalika na India.
Otherwise labda utakuwa na upande fulani kama Mtoa mada.