China yawawekea vikwazo viongozi 28 wa Trump ndani yake yupo Mike Pompeo

China yawawekea vikwazo viongozi 28 wa Trump ndani yake yupo Mike Pompeo

Zuio la USA linabaki PALEPALE.
Huwezi kufurahi aliyekuua akifa. Its illogical. Tanzania mnaitegemea sana USA lakini USA haiitegemei sana China. Mpaka viongozi wakuu wa Nchi wanalalia vyandarua vilivyoandikwa USAIDS. Au kwa hisani ya watu wa Marekani.
Wewe huyajui masuala ya uchumi wa kimataifa. Nenda google uamgalie kati ya China na Marekani nani anadaiwa kiasi kikubwa cha deni?

Kisha uelewe kwamba marekani imefanya uwekezaji mkubwa ndani ya China kwa sababu ya cheap labour na human resource.
Bidhaa nyingi unazonunua marekani hasa electronics zinatokea china under licence production.
Wewe kaa ukitafuta habari duniani acha kujifungia KINONDONI.
Ufipa.
 
Zuio la USA linabaki PALEPALE.
Huwezi kufurahi aliyekuua akifa. Its illogical. Tanzania mnaitegemea sana USA lakini USA haiitegemei sana China. Mpaka viongozi wakuu wa Nchi wanalalia vyandarua vilivyoandikwa USAIDS. Au kwa hisani ya watu wa Marekani.
Kwani aliyezuiwa ni nani na nani? Na kama hawajaenda huko Marekani sisi tutaathirikaje?
 
Mashabiki wa chadema wanafikiri mwisho wa pua zao tu!

China kwa sasa ni hot cake kwa dunia!

Hivi mnafikiri zile bifu za Trump na china ilikuwa ni kwasababu ya kujifurahisha? Tishio la Marekani kwa sasa ni China, ndio hapo sasa umuhimu wa china kwa Marekani kibiashara unapoonekana.

Marekani ana soko kubwa sana china kwa bidhaa za nafaka, ndio maana ukiibuka mzozo huwa unakuwa ni mjadala wa kidunia.

Wajinga wanafikiri ni ubushani wa simba na yanga!

It is all about economic issues.
 
Hahaaaa
[emoji849][emoji849][emoji849][emoji849][emoji849][emoji849][emoji849][emoji849][emoji849][emoji849][emoji849][emoji849][emoji849][emoji849]... sawaaaa lakini sio mahusiano na "SHIT HOLES COUNTRIES" kama Tanzania na Uganda sijui Kenya kwa 2022

Na kama unabisha subiri uone Bieden atakavyo kazia kuhusu Tanzania na Uganda shubaaaamit this time tutasoma namba kwa kirumi !!!

Miongoni mwa mvua za rasharasha tumesitisha mafunzo ya JKT kwa tangazo linaloumiza roho eti "walionyumbani msije na mlio kambini ondokeni"
 
Mara nyingi huwa namshukuru Mungu kwa kuliinua taifa la China
Haijalishi wamefikia wapi ila kikubwa wameleta mapindunzi ya uchumi na siasa duniani
China wameleta mapinduzi ya siasa? Mhhh
 
Na sisi tukimpiga ban sijui ataenda kutalii wapi kudadeki.
 
US ilipoweka zuio la baadhi ya bidhaa toka China, ukuaji wa uchumi ianguka toka 7% mpaka 2%. China ililipiza kwa kuweka zuio la baadhi ya bidhaa toka US, lakini uchumi wa US haukuonesha kutetereka kwa aina yoyote.
Wao ndio watoa takwimu na propaganda so hawawezi kujiponda. International politics ni ajenda pana mkuu
 
Mara nyingi huwa namshukuru Mungu kwa kuliinua taifa la China
Haijalishi wamefikia wapi ila kikubwa wameleta mapindunzi ya uchumi na siasa duniani
China , ma dictator wanaoua mtu yeyote anaehoji utendaji kazi wa chama cha ki communist cha China . Hao ndiyo tuchukue mfano kutoka kwao ??!!

Odhis *
 
Wanabodi,
Siku moja tu baada ya kuachia nafasi yake serikalini, Waziri wa mambo ya nje (secretary of state) wa Marekani aliyemaliza muda wake, Mr Mike Pompeo, pamoja na jamaa wangine waliokuwa kwenye serikali ya Trump, wamewekewa zuio la kuingia nchini China.

Pompeo ambaye siku ya mwisho ya uongozi wake alitangaza kuwawekea vikwazo vya visa kuingia Marekani baadhi ya viongozi wa Tanzania akiwatuhumu kuvuruga uchaguzi, amezuiliwa kuingia China kwa kutuhumiwa kufanya kampeni ya kuichafua China, kuvuruga mahusiano kati ya China na USA, na kuingilia na kuhatarisha maslahi binafsi ya China.

Kila muosha huoshwa!

Kwa habari zaidi soma hapa: China imposes sanctions on 'lying and cheating' Mike Pompeo, other Trump officials
Sasa aende China kufanya nini😀
 
Mara nyingi huwa namshukuru Mungu kwa kuliinua taifa la China
Haijalishi wamefikia wapi ila kikubwa wameleta mapindunzi ya uchumi na siasa duniani
Ulipaswa kumshukuru Mungu wako kwa kuwepo na taifa kama Marekani!Tofauti na hapo waafrica mngeuawana kama kuku na hakuna aambaye angejali!Mngeweza kutesana na kufungana na huyo Mchina yeye akaangalia maslahi yake na kuondoka kama haoni chochote!Usisahau hilo kumshukuru Mungu kwa hilo!
 
Wachina mpaka leo, kila siku wanaenda Ulaya na America kutafuta wawekezaji. China kwa sasa ndiyo nchi inayoongoza kwa kuvutia mitaji mikubwa toka nje. Makampuni ya Ulaya na America huwekeza wastani wa dola bilioni 80 kwa mwaka.

Ili makampuni yaliyoko China yapate mitaji ya kutosha yanalazimika kujiandikisha kwenye share markets za Europe, America na Australia.

Watu wanaikuza China kuliko uhalisia. Kuna mambo kadhaa ndio ukweli kuhusu China:

1) kwa kiasi kikubwa, China haifanyi ugunduzi wa kiteknolojia. Wao huwa wanakopi kwa njia rasmi za kibiashara au kwa kuiba

2) China bado ni nchi inayoendelea, na kundi kubwa la Wachina ni maskini

3) Katika maendeleo ya watu, China ni nchi ya 89 Duniani. Inazidiwa hata na baadhi ya nchi za Afrika kama Botswana

4) China ni nchi ya pili kwa ukubwa wa pato la Taifa Duniani lakini kiuhalisia ipo chini sana ikilinganishwa na US. Ukubwa wa pato unatokana na ukubwa wa nchi na uwingi wa watu, na siyo kutokana na mifumo bora ya uchumi kama ilivyo kwa mataifa ya Ulaya na America.

5) Asilimia kubwa ya makampuni makubwa yaliyopo China, siyo ya wachina bali ni ya nchi za Magharibi. Kampuni pekee kubwa ya China ni HUAEI

6) Ni uwongo kuwa China imeikopesha US. Pesa ambayo serikali ya Beijing huwa inaidai Washington ni ya mauzo ya government treasury bills. Serikali ya China ili kutaka kujiimarisha na kutengeneza faida huwa wanapenda kununua treasury bills za US

7) Makampuni yote ya nchi za Magharibi yaliyowekeza China yana bima maalum ambayo inayafanya yasipate hasara yoyote kama endapo yatalazimika kufunga na kuondoka. Na yakifanya hivyo, uchumi wa China utayumba kwa kiasi kikubwa kuliko itakavyotokea kwa nchi za Magharibi. China inalijua hilo, ndiyo maana inajiegemeza sana Afrika.

8) Kilichoibadilisha China kwa kiasi kikubwa ni uwekezaji mkubwa wa nchi za Magharibi nchini China baada ya China kuachana na mifumo ya uchumi wa kijamaa. Wachina kwa miaka mingi wameishi katika uchumi duni.
 
We na we mbona unaleta ufananishi wa mbingu na ardhi?

Mimi nimesema China ilikua inaiba data wewe unasema USA akiamua na yeye anaweza kupata data.

Hivi hata umeelewa nilichoandika? Unaelewa maana ya dependency?
Unategemea hiyo dependency unaiwekaje or in what context.
Na why dependency kwa china iyonekane mbaya , wakati b4 that we have been dependent to western countries
 
China , ma dictator wanaoua mtu yeyote anaehoji utendaji kazi wa chama cha ki communist cha China . Hao ndiyo tuchukue mfano kutoka kwao ??!!

Odhis *

Mimi nimesema nani tuchukue mfano wa kuua China? Rudia kusoma nilichoandika kwa utulivu

mama D said:
Mara nyingi huwa namshukuru Mungu kwa kuliinua taifa la China
Haijalishi wamefikia wapi ila kikubwa wameleta mapindunzi ya uchumi na siasa duniani
 
Ulipaswa kumshukuru Mungu wako kwa kuwepo na taifa kama Marekani!Tofauti na hapo waafrica mngeuawana kama kuku na hakuna aambaye angejali!Mngeweza kutesana na kufungana na huyo Mchina yeye akaangalia maslahi yake na kuondoka kama haoni chochote!Usisahau hilo kumshukuru Mungu kwa hilo!
Nikuulize swali moja tuu,

HAO UNAOSEMA TUWASHUKURU LEO WAKATI WANAKUJA WALIWAKUTA WAAFRIKA WANAUANA KAMA WANAVYOANA SASA PALE DRC CHINI YA USIMAMIZI WAO?
 
Back
Top Bottom