China yazindua Cruise Ship ya kwanza, 'Adora Magic City.'


Usisahau na bei nafuuu [emoji41]
 
Hivi wale wabunifu wetu wa helcopter waliishia wapi? Kwanini wasiwe accelerated ili siku moja wafike huku? Hawa wachina si nao walianza kama wetu?
Wale sio wabunifu, wale ni kama kijana wa mtaani anayeweza piga danadana zaidi ya 200 alafu uje useme akasajiriwe timu ya ligi kuu.
Kama ungekuwa mtumiaji mzuri wa YouTube ungeona demonstrations za watoto wa vyuo na wahuni uko duniani wakitengeneza maroketi madogo kilo kama 50 linapaa makumi ya kilomita na wanapiga kila kitu kwa kompyuta na programu wanazo na calibrations wanafanya. Wakitoka hapo sio eti wanaamini wana uwezo wa kuunda roketi, wala media hazihangaiki nao.
Kuna bwana mmoja yeye anatengeneza mini -engines kwenye channel yake ya YouTube nimesahau jina.

Bongo mtu anachomelea mabati na kuweka mota used ya mashine ya kusaga alafu media na kamera zao wanakuja kusema eti "kaunda helikopta". Hata uweke trilioni moja kwenye mradi, hutoi helikopta pale.

Manufacturing ya vitu vikubwa sio jambo la mtu mmoja, inabidi iwe sera ya nchi na dira ijulikane tunafanya vitu vingapi ambavyo vikiungana ndio vinawezesha industry fulani ikue. Mfano Boeing ndege zao zina components zaidi ya milioni moja, yani ndege moja inahitaji ufanye utafiti, ukague ubora, utoe certificate, ufanye testing, ufanye upgrade, upime resistance sijui uwezo wa mwisho na mambo mengine mengi kwa kila component na hapo una vitu zaidi ya milioni moja vyote upitie process hiyo.

Kwa hali hiyo hakuna uwezekano ndege nzima ikaundwa na Boeing. Landing gear atakuwa labda General Electric, power supply labda awe BAE Systems, kompyuta na mifumo ya mawasiliano labda awe Raytheon na makampuni zaidi ya 100 yanahusika.

Sasa bongo mtu anakwambia anatengeneza gari la umeme ila akionyesha sehemu anakotengenezea ni kama sebule kubwa, sakafu ya nyumbani, vifaa vya kutengenezea gari hamna; sikuona moulding machines, sikuona lathes, sikuona vya kufanya cutting, kupaka rangi ile electropainting, hakuna sehemu ya drawings na design. Mafundi gereji wameshika spana alafu kuna raia kwa akili zao kabisa wanaamini pale kuna gari linatengenezwa. Nitaambiwa nina chuki na "mbona hata Toyota sio kila kitu wanatengeneza wao".
Kama kufanya assembling hapo sawa hata mafundi gereji wanaweza, si huwa wanafungua kila kitu kwenye gari na kukirudisha.

Sasa hivi vitu havifanyiki nchi haina steel industry, vyuo vinakaririsha vitini, shule zinafundisha uchavushaji wa maua na matobo ya panzi kupumulia, umeme ghali na hauaminiki, hakuna investing culture kila mtu anajenga nyumba za kupanga hapo anaona amewekeza, rushwa, hakuna juhudi binafsi za kulinda viwanda vya ndani.
Manufacturing ni ngumu sana usione matajiri wa bongo wanaenda kununua vitenge China waje kuuza wawe mabilionea wakati viwanda vya nguo kibao nchini vimekufa na pamba sio zao tena la kibiashara.
 
afu mtu jinga moja utaliskia wanaijeria wachawi!!!uchawi ndo huu sasa
 
China akishakuwa na soko la ndani inamtengenezea production capacity kubwa ambayo inatosheleza soko la nje ukizingatia orders zinavyokuwa. Mwaka juzi hivi Serbia walinunua air defense system kutoka kwao nadhani ni HQ-9 kama sisahau, zililetwa mwaka jana wakati ukinunua systems za Marekani au Ulaya inabidi ukae zaidi ya miaka miwili ndio upokee, ukitaka haraka zaidi unalipa hela nyingi zaidi.
Mwaka jana tena Pakistan ikapata delivery yake ya pili ya J-10C fighter jets, wakati wameziagiza ndani ya miaka miwili vilevile. Nigeria ilivyoagiza JF-17 hazikukawia.

Yani ukiwa vitani na una compatibility na silaha za Mchina ambazo zipo in service utapata silaha kwa nguvu kidogo kuliko manufacturers wa nchi nyingine. Kutimiza mahitaji ya wateja wa nchi ya watu bilioni 1.3 itakufanya uone kama ni kucheza ukitengeneza bidhaa za nchi ya watu sijui milioni 60.
 
Well said
 
🤣😄
 
Duuuu....hiii kichwaa hatari..ckupangaa kucoment.semaa inaonekana uko bright..Africa tuna safari ndefu aiseee
 
Hatutakiwi kuwaza kwenye kutengeneza ndege kabisa kabisa, hizo ni ndoto za mchana. Boeing ambao ndio giant duniani wanatumia zaidi ya trilioni 6 za Kitanzania kufanya research na development, hapo wana products ambazo tiyari zinakubalika, wana plants tiyari, wana wataalamu na uzoefu, wana contracts na suppliers. Yani wanaweza kaa miaka minne bila kuleta modernization yoyote ya ndege na wakaendelea kuwa sokoni ila bado wanatumia zaidi ya trilioni 6 kwenye utafiti, sembuse sisi tukitaka kuanza na moja tuwekeze kiasi gani.

Sisi tuwaze kutengeneza zana za kilimo, viwepo viwanda vya matrekta, mabomba ya kumwagilia, combine harvesters, cold rooms za kuhifadhi matunda kama parachichi za kule Njombe, silos za kisasa na vitu kama hivyo.
Tukitoka stage hiyo twende kwenye kutengeneza nguo. Kisha viwanda vya kuchakata bidhaa nyingine za kilimo habari za kubeba magunia ya korosho kwenda nje tuache, tubebe maboksi ya korosho zilizokuwa roasted.

Hapo hapo tunaweza elekea kwenye kuunda magari kwenye assembly lines tukichukua licence kutoka kwa manufacturers. Unakuwa mwisho wa kununua daladala nje. Hapo sasa tunaongeza miundombinu ya reli na bandari inaongezwa nyingine hasa Mtwara, tunaelekeza nguvu kwenye nishati inakuwa cheap na uhakika. Hapo ndipo tunaita wawekezaji wakubwa wa kujenga kiwanda cha hata bilioni 500.

Hapo nimefanya kwa ufupi, kuna mlolongo mrefu sana unatakiwa mfano kwenye elimu, sheria, kupambana na rushwa, uhuru wa kibiashara na mengine. Ila kwa akili za kibongo hizi za kujadili mpira asubuhi saa moja inatakiwa roho ngumu ishushwe kutoka mbinguni kujaribu kufanya haya.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…