China yazindua Cruise Ship ya kwanza, 'Adora Magic City.'

China yazindua Cruise Ship ya kwanza, 'Adora Magic City.'

Hatutakiwi kuwaza kwenye kutengeneza ndege kabisa kabisa, hizo ni ndoto za mchana. Boeing ambao ndio giant duniani wanatumia zaidi ya trilioni 6 za Kitanzania kufanya research na development, hapo wana products ambazo tiyari zinakubalika, wana plants tiyari, wana wataalamu na uzoefu, wana contracts na suppliers. Yani wanaweza kaa miaka minne bila kuleta modernization yoyote ya ndege na wakaendelea kuwa sokoni ila bado wanatumia zaidi ya trilioni 6 kwenye utafiti, sembuse sisi tukitaka kuanza na moja tuwekeze kiasi gani.

Sisi tuwaze kutengeneza zana za kilimo, viwepo viwanda vya matrekta, mabomba ya kumwagilia, combine harvesters, cold rooms za kuhifadhi matunda kama parachichi za kule Njombe, silos za kisasa na vitu kama hivyo.
Tukitoka stage hiyo twende kwenye kutengeneza nguo. Kisha viwanda vya kuchakata bidhaa nyingine za kilimo habari za kubeba magunia ya korosho kwenda nje tuache, tubebe maboksi ya korosho zilizokuwa roasted.

Hapo hapo tunaweza elekea kwenye kuunda magari kwenye assembly lines tukichukua licence kutoka kwa manufacturers. Unakuwa mwisho wa kununua daladala nje. Hapo sasa tunaongeza miundombinu ya reli na bandari inaongezwa nyingine hasa Mtwara, tunaelekeza nguvu kwenye nishati inakuwa cheap na uhakika. Hapo ndipo tunaita wawekezaji wakubwa wa kujenga kiwanda cha hata bilioni 500.

Hapo nimefanya kwa ufupi, kuna mlolongo mrefu sana unatakiwa mfano kwenye elimu, sheria, kupambana na rushwa, uhuru wa kibiashara na mengine. Ila kwa akili za kibongo hizi za kujadili mpira asubuhi saa moja inatakiwa roho ngumu ishushwe kutoka mbinguni kujaribu kufanya haya.
Kaka kichwani una vitu,
 
Shanghai, China
06/06/2023


Kampuni kubwa ya utengenezaji meli inayoitwa China State Shipbuilding Corporation (CSSC) yenye makao yake Shanghai walizindua meli ya kwanza ya kitalii (Cruise ship) kutengenezwa China, iliyopewa jina la Adora Magic City.

Itakuwa cruise ship ya kwanza duniani kuwa na internet ya 5G

Meli hiyo yenye uwezo wa kubeba abiria 5246 na vyumba vya kulala 2826 ina
•Restaurants
•Theaters
•Shopping centres
•Water parks & swimming pools
•Outdoor Cinema
•Casinos
•Gaming lounge
•Luxury-brand boutiques
•Photo Gallery & Shop
•Bar
•Modern gym
•Spa
•Beauty saloon
•Stage for live perfomance
•Multi-Sports Course (for playing volleyball/basketball/tennis
•Themed entertainment for kids in 3 age groups
(i)Age 2-5 yo, 6-8 yo, and 9-11 yo
(ii)Children Club Lounge is for older kids (12-14 yo/video games, movies, parties, planned activities),
(iii)Teen Club for teenagers (15-17 yo/movies, interactive video gaming, karaoke, themed parties, booking teen-only cruise shore excursion).


Mwonekano wa nje;

View attachment 2654911

View attachment 2654912



Baadhi ya picha za mwonekano wa ndani

Hotel
View attachment 2654913


Restaurant
View attachment 2654914

Theatre
View attachment 2654915

Mall
View attachment 2654917

Water park
View attachment 2654952

Sasa ni wakati wa China kuingia katika ushindani na makampuni ya Ulaya na America katika utengenezaji wa cruise ships.

UTENGENEZAJI WA MELI CHINA
Mbali ya meli za abiria pia meli zinazotengenezwa kwa wingi nchini China ni meli za mizigo kama liquefied natural gas (LNG) tankers, oil tankers na container ships.

Baadhi ya rekodi zilizowekwa na China katika utengenezaji wa meli;

●Kwa miaka 13 mfululizo China inashikilia rekodi ya kuongoza uuzaji wa meli duniani.

●China State Shipbuilding Corporation (CSSC) ilisaini mkataba na kampuni ya Ufaransa ya CMA CGM kuitengenezea meli za kubeba kontena kubwa 16 zenye thamani ya 4 billion U.S. dollars. Imekuwa kampuni ya kwanza duniani kupewa oda kubwa kwa wakati mmoja

●Meli kubwa duniani ya kubeba container yenye ukubwa wa viwanja 4 vya mpira wa miguu, iliuzwa kwa kampuni ya Mediterranean Shipping Company (MSC) SA. Ilitengenezwa na kampuni ya Hudong-Zhonghua Shipbuilding Co Ltd, yenye makao yake Shanghai. Imepewa jina la MSC TESSA

View attachment 2654947


●China pekee inachangia 47.3% ya meli za mizigo zinazotengenezwa duniani

●Kampuni za China zinaongoza kwa kuwa na zaidi ya nusu ya oda za meli zote ulimwenguni

According to Voice Of America (VoA):
China has 19 modern shipbuilding yards pumping out commercial and naval ships. One of China's shipyards is so large that its capacity surpasses that of all U.S. shipbuilders combined.
cosco shipping offshoreseamen
 
Tuna safari ndefu sana kama taifa, mimi binafsi kichwa kinaniuma kuona sisi hapa duniani tunakaa kusubiri watu wa mataifa mengine wafanye ugunduzi halafu sisi tunabaki kuwa consumers tuuuuu.
Nyie wa kwenu ata agukindua bunduki mnamkamata badala ya,kuendeleza ujuzi.nyie ugunduzi wenu ni uchawi tu na wakina dr msukuma kushangilia kuuza bandari
 
Nyie wa kwenu ata agukindua bunduki mnamkamata badala ya,kuendeleza ujuzi.nyie ugunduzi wenu ni uchawi tu na wakina dr msukuma kushangilia kuuza bandari
Bado tuna safari ndefu kwa sababu hatuna sera wezeshi kwa innovators
 
Nyie wa kwenu ata agukindua bunduki mnamkamata badala ya,kuendeleza ujuzi.nyie ugunduzi wenu ni uchawi tu na wakina dr msukuma kushangilia kuuza bandari
Unaelewa maana ya kugundua wewe ?

Kuiga na kujaribu kutengeneza kitu ambacho wengine walishakiunda na kukitengeneza miaka mingi nyuma sio jambo la kawaida
 
Sisi tuwaze kutengeneza zana za kilimo, viwepo viwanda vya matrekta, mabomba ya kumwagilia, combine harvesters, cold rooms za kuhifadhi matunda kama parachichi za kule Njombe, silos za kisasa na vitu kama hivyo.
Tukitoka stage hiyo twende kwenye kutengeneza nguo. Kisha viwanda vya kuchakata bidhaa nyingine za kilimo habari za kubeba magunia ya korosho kwenda nje tuache, tubebe maboksi ya korosho zilizokuwa roasted.
Sahihi kabisa kiongozi, kilimo ndio sekta nzuri sana ya kuanzia ili kuijenga hii nchi.

Isitoshe soko lipo la kutosha kuanzia kwa majirani mpaka Kusini mwa Africa, nadhani bado hatujawa makini na hii sekta.
 
Duniani panazidi tu kunoga,wakati tukifurahia mafanikio ya wenzetu tusiache Muomba Mungu aepushilie mbali majanga katika hivi vyombo vinavyobeba ma elfu ya watu.

Najaribu tu kuwaza Meli inayoweza beba watu wazima 5000 and above, hujaongelea wenye watoto assume watoto wakubebwa wawe 500 plus vitoto vingine bado hujaweka wafanyakazi/wahudumu,nk

yani AJALI ya haya madude ikichukua watu wote unakua MSIBA wa DUNIA sio hata wa china maana ni yale yale ya TITANIC ndio tunakoelekea

Watafiti naombeni mnisaidie,IPO meli kwasasa iliyokuta ukubwa wa titanic na kuzidi labda au tuendelee kusubiri ila kwasasa haipo???
 
Sahihi kabisa kiongozi, kilimo ndio sekta nzuri sana ya kuanzia ili kuijenga hii nchi.

Isitoshe soko lipo la kutosha kuanzia kwa majirani mpaka Kusini mwa Africa, nadhani bado hatujawa makini na hii sekta.
hela zilizopo ni za kutoa zawadi kila goli likifungwa na motisha kwa wote watakao fanya jambo lolote zuri. ila sio kuwekeza kuboresha katika vitu vya maana.
 
China's 1st domestically-built large #cruiseship "Adora Magic City" concluded its 2nd sea trial and arrived at a port in Shanghai Tue. It is expected to be the world's 1st #5G cruiser and can provide passengers with high-speed Wi-Fi experience as good as they can access on land.
 
20231123_150136.png


In 2023, the global shipbuilding industry will indeed see surprising changes: the collapse of South Korea's shipbuilding industry and the crazy expansion of China's shipbuilding industry.
 
Back
Top Bottom