China yazindua Cruise Ship ya kwanza, 'Adora Magic City.'

Kuna watu hata kama uwakubali inabidi uwape credit zao China mnajua sana.

Sent from my Infinix X624 using JamiiForums mobile app
 
Safi sana

Viva China ✌️
 
Haya ni matokeo chanya ya serikali ya China kuwekeza kwenye R&D na sera nzuri za serikali kwenye masuala ya teknolojia na uchumi.
Maraisi wote waliopita kuanzia Chairman Mao Zedong, comrades Deng Xiaoping, Jiang Zemin, Hu Jintao wamefanya kazi nzuri.

Ila kwa njia ya kipekee Xi Jinping ameiinua sana China kwenye teknolojia sera yake ya China kutotegemea teknolojia ya nje na kuwekeza kwenye R&D imeleta innovations nyingi za ndani ya China
 
China akishaingia kwenye production ya kitu au bidhaa fulani tegemea lazima aje kuongoza.

Mwezi Desemba mwaka jana 2023, BYD imeipiku Tesla kwa kuuza magari mengi zaidi ya umeme duniani

Hizi sio habari njema sana kwa bwana Elon Musk
Nasubiri kwa hamu C919 na C929 zitakapokuja kuzipiku Airbus na Boeing kimauzo duniani
 
Titanic kwa sasa hayumo hata kwenye top 100 kwa ukubwa duniani!
 
Ila sijajua kwanini naamini haya maendeleo ya China kwasasa yamechagizwa na bwana jintao

Au sijui sababu jamaa nilikua namkubali tuuu Jintao nilikua namuelewa sanaaaaaaaa
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…