ChinaTech: Sehemu kubwa ya China haijaathirika na mvurugiko wa TEHEMA (IT) uliotokea leo duniani kote kwenye Microsoft Windows

ChinaTech: Sehemu kubwa ya China haijaathirika na mvurugiko wa TEHEMA (IT) uliotokea leo duniani kote kwenye Microsoft Windows

Crowdstrike wanafanya kazi na deep state ya Marekani

Leo walikuwa wanakusanya taarifa za watumiaji mbalimbali duniani

This is a cyber attack iliyobarikiwa na serikali ya Marekani sio ya kuichukulia poa
Watu mnapenda sana conspiracy, yani kukuibia data unadhani mpaka mfumo uwe down? Haya mambo hutokea au umesahau kuwa kati vitu vilivyoiua blackberry mojawapo ni technical glitch iliyosababisha huduma yao ya bbm messenger kuwa down, facebook nayo mara kadhaa imekumbana na kutopatikana kwa muda, same to Google.
Errors kwa mifumo huwa haikosekani kama binadamu anaumwa ije kuwa mifumo kubuma.
 
Crowdstrike wanafanya kazi na deep state ya Marekani

Leo walikuwa wanakusanya taarifa za watumiaji mbalimbali duniani

This is a cyber attack iliyobarikiwa na serikali ya Marekani sio ya kuichukulia poa

Source: trust me bro.
 
Na Russia ilikua salama kabisa kwa zile safari za ndani
Kuna haja ya kujitegemea hapa yunakumbushwa pia umuhimu wa kuiombea SMO ya RUSSIA pale Ukraine izidi kufanikiwa
 
Source: trust me Bro 🤣🤣
Trust me bro 😄

Screenshot_20240720-182009_Chrome.jpg
 
Kwahiyo hiyo article ndo proof ya hii statement yako

"Leo walikuwa wanakusanya taarifa za watumiaji mbalimbali duniani

This is a cyber attack iliyobarikiwa na serikali ya Marekani sio ya kuichukulia poa"

Kwamba hii disruption ni kukusanya taarifa? Kama zamani walikua wanakusanya kimya kimya nini kimewashinda Leo?

Sio nyie mnaosema China na Russia hawatumii MS?

Umeona Hapo inasema forefront of conspiracy theories, wewe ndo upo Hapo.

Kawaida maskini haamini kama tajiri nae anakufa, anadhani tajiri kufariki ni njama sio kifo Cha kawaida tu. Ndo wewe sasa huamini kama hata big companies suffer same fate as smaller ones. Hata hizo OS za nchi zingine zinapata disruption ila market share yao ndogo hata uwe na yako itapata hitilafu it's not a matter of IF but WHEN. Keep that in mind.
 
Leo huduma zote za TEHAMA zinazotumia Microsoft Windows zilikumbana na hii changamoto kwenye screen za computer ilikuwa ni 'bluescreen'

View attachment 3046558
View attachment 3046559
View attachment 3046783
View attachment 3046784
Huduma nyingi zinazotumia Microsoft Windows kama usafiri wa ndege, biashara, mashirika ya utangazaji zimeathirika sana leo zote zilisimama kwa muda.

Microsoft wanafanya kazi na kampuni ya kutengeneza antivirus ya CrowdStrike moja ya kazi ya hiyo antivirus ni kuzuia hackers.

Kwa mujibu wa CrowdStrike imekiri kwamba tatizo hilo lilisababishwa na updating ya programu ya anti-virus inayoitwa Falcon Sensor ambayo imeundwa kulinda vifaa vinavyotumia Operating System ya Microsoft Windows dhidi ya mashambulizi mabaya kama ya hackers.

Kwa hiyo wakati wa kuupdate kukotokea mvurugiko au outage kwa wanaotumia Microsoft Windows.

Upande wa China haikuwa hivyo kwa sababu huduma nyingi hasa katika mashirika ya serikali ziliachana na Microsoft Windows na kutumia China-made Operating System (OS) iitwayo NeoKylin.

Hivyo huduma za usafiri wa anga, benki n.k hazikuathirika.

Hii ni kwa sababu tangu mwaka 2015 China walikuja na mpango wa miaka kumi (2015–2025) unaoitwa Made in China 2025 (MIC25) wa kutotegemea teknolojia za kutoka nje bali kuendeleza na kutumia teknolojia za ndani.

Mojawapo ya eneo lililoguswa ni kujitegemea katika mifumo ya I.T (TEHAMA) hii ilitia ndani kuachana na utegemezi wa Microsoft Windows.

www.jamiiforums.com/threads/made-in-china-2025-mpango-wa-china-wa-kujitegemea-kiteknolojia-wafikia-asilimia-88.2220546/

CREDIT:www.scmp.com/tech/big-tech/article/3271171/microsoft-outage-leaves-china-largely-untouched-tech-self-sufficiency-campaign-pays
Hata Marekani watu wasiotumia Codwdstrike hawajaathirika.
 
Kwahiyo hiyo article ndo proof ya hii statement yako

"Leo walikuwa wanakusanya taarifa za watumiaji mbalimbali duniani

This is a cyber attack iliyobarikiwa na serikali ya Marekani sio ya kuichukulia poa"

Kwamba hii disruption ni kukusanya taarifa? Kama zamani walikua wanakusanya kimya kimya nini kimewashinda Leo?

Sio nyie mnaosema China na Russia hawatumii MS?

Umeona Hapo inasema forefront of conspiracy theories, wewe ndo upo Hapo.

Kawaida maskini haamini kama tajiri nae anakufa, anadhani tajiri kufariki ni njama sio kifo Cha kawaida tu. Ndo wewe sasa huamini kama hata big companies suffer same fate as smaller ones. Hata hizo OS za nchi zingine zinapata disruption ila market share yao ndogo hata uwe na yako itapata hitilafu it's not a matter of IF but WHEN. Keep that in mind.
Mimi nilisemaje kwani?
 
Back
Top Bottom