Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
干煎黄鱼 (Gan Jian Huang Yu) - Pan Fried Yellow Fish
Ni samaki aliyekaangwa na wakati mwingine huwekwa viungo vyenye kumfanya awe na ladha nzuri mdomoni.
![]()
Jamani nyoka aliyeokwa sijamuona hapo sijui hii menu inaitwaje nataka nijaribu
...tatizo ni huo wali usio na ladha sijui utapita kooni!!
Kusema kweli wachina MashAllah.
Apa kwetu zenji kuna Restaurant yao inaitwa Pagoda. Ama nkiwa na uchenji wa maana sijinyimi. Bata wao watam ajabu, na prawns na kaa. Na soup zao.
Ila iyo iwe kwa hapa tz yetu. Ukienda kwao ni kheri uagize mboga mboga mana mara unalishwa chura au nyoka au mbwa. Lols
小白菜 (Xiao Bai Cai) - Chinese cabbage
Hii ni mboga ya majani ambayo hupatikana Mashariki ya Mbali na ni moja ya mboga za majani maarufu huko.
Mapishi yake kwa kawaida hutumia mvuke au huchemshwa pasipo kutokosa na huwekwa vitunguu saumu na chumvi tu.
![]()
Hapa naona gari la KORIE liliangukia kwa bahati mbaya,ukipiga mfululizo unakaribisha Cholesterol,BP,SHELL na Caltex lol回锅肉 (huíguōròu) - Twice Cooked Pork
Hii ni nyama ya kitimoto hivyo kwa wale ndugu zangu msiotumia hii bidhaa inabidi kutoagiza hii.
Ni chakula chenye asili ya Jimbo la Sichuan na kawaida huwa haina vikorombwezo vingi zaidi huwa na majani ya kabichi ambayo huwekwa sour vinegar ili kuleta ladha ya uchachu na wakati mwingine huambatana na pilipili hoho na pilipili za kawaida.
![]()
Hapa naona gari la KORIE liliangukia kwa bahati mbaya,ukipiga mfululizo unakaribisha Cholesterol,BP,SHELL na Caltex lol
Mkuu mimi nina visa na chakula chenye mafuta mengi...kwa orodha uliyotoa naona havinifai...
Je. kuna menu nyingine yenye vyakula visivyo na mafuta mengi ?
Endelea kutoa darasa best labda uoga wa kukaribia misosi yao utatutoka wengineMafuta ya hawa jamaa ni salama kwa afya otherwise kwa wingi wa Wachina duniani basi huenda lingekuwa ni taifa la watu wanene kuliko wote duniani.
Most of fried chinese cuisine huwa zinatiririsha mafuta kama hivyo when served.
Mkuu mimi nina visa na chakula chenye mafuta mengi...kwa orodha uliyotoa naona havinifai...Je. kuna menu nyingine yenye vyakula visivyo na mafuta mengi ?
Mafuta ya hawa jamaa ni salama kwa afya otherwise kwa wingi wa Wachina duniani basi huenda lingekuwa ni taifa la watu wanene kuliko wote duniani.
Most of fried chinese cuisine huwa zinatiririsha mafuta kama hivyo when served.
清蒸鱼 (Qing zheng yu)
Huyu ni samaki ambaye yuko steamed na viungo, mtamu balaa. Hakuna mimafuta wala nini na aina ya samaki inayotumika zaidi hapa ni samaki asiye na miba midogo midogo, yaani hapo ni wewe na chop stick yako ukimaliza upandemmoja unageuza upande wa pili unaendelea
![]()
Mimi nilidhani sangara...huyu samaki anaitwa chewa ... yes ni mtamu sana