mfianchi
Platinum Member
- Jul 1, 2009
- 11,904
- 8,371
Kasheshe ni kukumbuka hayo majina mkuu.
Vp ulienda au unasomea?
Itabidi uprint hicho kipande cha maelezo halafu weka kwa pochi ,ukifika kwa mgahawa onyesha na basi ujienjoy kwishney
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Kasheshe ni kukumbuka hayo majina mkuu.
Vp ulienda au unasomea?
mkuu watu8 hii chakula nimeichunuku sana lazima niitafute this weekends da pan ji...ila jina lazima nikariri大盘鸡 (Da Pan Ji)
Hiki ni chakula chenye asili ya Jimbo la XinJiang lipatikanalo Kaskazini Magharibi mwa China na wengi wa wapishi wa pishi hili ni Wz XinJiang ambao wana migahawa karibia kila kona ya China na baadhi ya nchi nje ya China.
Chakula hiki huwa ni mchanganyiko wa supu ya vipande vya kuku, viazi mviringo na viungo (seasoning spices) vingine vingi kwa ajili ya kutia ladha na harufu murua.
![]()
![]()
Katika ulimwengu wa vyakula na mapishi kuna aina mbalimbali ya vyakula ambavyo upande mmoja wa dunia vinaweza kuwepo na upande mwingine kukosekana.
Ukiachana na hilo pia kuna jambo moja inabidi tutambue kuwa sehemu kubwa ya dunia aina ya raw materials za vyakula ni ile ile lakini namna ya upikaji ndio hutofautiana.
Katika thread hii ningependa kuweka bayana baadhi ya vyakula vilivyopikwa kwa recipes za kichina ambavyo Mtanzania na Muafrika yoyote anaweza kula pasipo kupata tabu ya ladha.
Kwa wale waliopo nyumbani Tanzania wanaweza kuingia kwenye Migahawa ya Kichina iliyopo huko na kuagiza hizi menu vivyo hivyo na kwa wale waliopo nje ya Tanzania.
NB:
Vyakula vingi vya kichina hupikwa kwa mtindo wa mboga ambapo ulaji wake huambatana na wali 'steamed rice' (huu hauwekwi mafuta wala chumvi), mikate ya kichina (mantou), tambi za kichina (miantiao) n.k..
Hivyo hakikisha uagizapo dishes hizi unaagiza na kimojawapo cha hivyo, lakini mimi nashauri muagize wali kwani ndio wengi wetu tumeuzoea.
Thread hii haitaelekeza namna ya upikaji wa chakula chochote cha Kichina bali itakupa mwangaza tu wa nini uchague utapoingia katika mgahawa wa Kichina.
Pia naomba sana mkuu Invisible na X-PASTER kwa heshima na taadhima thread hii uiweke kama Sticky thread ili iwe msaada kwa wananchi wengi.
Kwa wale wasopenda vyakula bahari watakula hii
重庆辣子鸡 (Chóngqìng làzǐjī😉
Kama wewe ni mpenzi wa chakula chenye pilipili kali basi jaribu kula hii menu kwani pengine nusu huwa ni pilipili na nusu nyingine huwa ni vipande vya kuku na viungo vingine.
![]()
Mmh hili sasa mbona balaa, pilipili nyingi hivyo! Au ndo inakuwa kama mboga na yenyewe?
Sent from my BlackBerry 9300 using JamiiForums