CHINESE CUISINE: Nini ule ukienda kwenye mgahawa wa kichina...

CHINESE CUISINE: Nini ule ukienda kwenye mgahawa wa kichina...

Tatizo lao wanatia sukari kwenye mapishi yao hasa nyama

Kwa kawaida vyakula vya kichina vinatofautiana kulingana na wapi asili ya chakula hicho.

Mathalani upande mkubwa wa majimbo ya kaskazini ya China vyakula vyao hujumuisha sukari, si haba kukuta nyama ya ng;ombe imewekwa sukari.

Lakini kwa vile vyakula vya kusini ya China majimbo kama Sichuan, Kunming, Guangzhou au katikati ya China kwenye majimbo kama Hubei, Xi'an, Hunan au kaskazini magharibi kule Urumuq ni wao vyakula vyao havina sukari na ni vyakula maarufu na vitamu.
 
重庆辣子鸡 (Chóngqìng làzǐj&#299😉 Kama wewe ni mpenzi wa chakula chenye pilipili kali basi jaribu kula hii menu kwani pengine nusu huwa ni pilipili na nusu nyingine huwa ni vipande vya kuku na viungo vingine.
35-%E9%87%8D%E6%85%B6%E8%BE%A3%E5%AD%90%E9%B8%A1-Chongqing-Style-Spicy-Chicken-1024x768.jpg
chakula hichi lazima utafute feni kujipuliza ukiwa toilet maana ni nomaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaa
 
sa mdau kibongo bongo mgahawa gani wa kichina mzuri...maana nataka kula point 3 kwa mtoto mmoja nikimpeleka dinner...picha nakua mi ndio starling najifanya najua majina ya kichina ya misosi ka Jack Chen vile.
Ila niambie katika hiyo list uliyotoa kwa hela za madafu hipi expensive hipi kawaida..maana sio unaenda dinner inakucost gharama ya kununua vits

Hahahah!!!

Mkuu vyakula nilivyoweka vyote bei zake ni za kawaida ingawaje hiyo mboga ya mayai na ile ya majani huenda ikawa rahisi zaidi lakini sidhani kama itakuwa ni special meal kwa mtoko kama uutakao.

Sina uzoefu sana na bei za migahawa ya Kichina hapa Dar es Salaam, labda kwa Nairobi au Zanzibar ndio kidogo nina clue.

Kwa uzoefu huo maybe hakikisha uwe na pocket money kuanzia elfu sitini hivi kwa kuwa ni dinner ya watu wawili...(hii bei nimejaribu kufananisha na ile ya Zenji).

Ila huenda ikawa chini ya hapo just give it a try kwa kwenda kuulizia kwanza kabla ya mtoko, ili siku ya mtoko uwe na details za kutosha(kwenye migahawa kuuliza huwa yaruhusiwa).

Kuna "Istana Restaurant" wao huwa na cuisines mbali mbali kama Indian, Malaysian, Chinese. Unaweza kuangalia kupita pale siku ya Jumanne jioni ukacheck maana ndiyo siku wanakuwa na Buffet la Vyakula vya Kichina.
Istana ipo karibu na BMTL Victoria au opposite na Oilcom ya Victoria na bei zao ni very standard.

Pia kuna mgahawa mwingine unaitwa Tangren, upo Mtaa wa Ursino(Mikocheni) karibu kabisa na mgahawa wa "Addis in Dar".
Nimetafuta hii link walau uone walivyo navyo hawa jamaa, pia bei zao ni kawaida ...

Narudi Nyumbani !: Tangren chinese restaurant
 
Mmmh ukienda tena magahawa wa Chinese, itafute Konjee Crispy Lamb au Chicken Thread. Its all time my favourtie

cc watu8
 
Last edited by a moderator:
Kipenzi hilo jina la dish ya kwanza nadhani lina asili ya uhindini eenh...

Wachina hiyo menu huwa wanaiita 'Shao Yang Rou' ( 烧羊肉 ).

Hii ya pili sijawahi kuila nitajaribu next time nikipata kwenda kwa Wachina...

Mmmh ukienda tena magahawa wa Chinese, itafute Konjee Crispy Lamb au Chicken Thread. Its all time my favourtie

cc watu8
 
Last edited by a moderator:
干煎黄鱼 (Gan Jian Huang Yu) - Pan Fried Yellow Fish

Ni samaki aliyekaangwa na wakati mwingine huwekwa viungo vyenye kumfanya awe na ladha nzuri mdomoni.

3254577175_05b7ca0163_o.jpg
huyu samaki anaonekana ana "CRISPY SKIN" nam nam....
 
Originally ni Chinese cuisine....na sio hiyo Shao Yang Rou, maana haiwi gravy yenyewe ni dry and crispy. Chicken thread make good appetizer, there's option for prawn thread also.
 
Originally ni Chinese cuisine....na sio hiyo Shao Yang Rou, maana haiwi gravy yenyewe ni dry and crispy. Chicken thread make good appetizer, there's option for prawn thread also.

Okay...gotcha kipenzi
 
Kasheshe ni kukumbuka hayo majina mkuu.
Vp ulienda au unasomea?

Majina si tabu mkuu, natumai muda mwingi watu huwa wanakuwa na simu zao za mikononi.

Simu nyingi za kisasa zinaruhusu mtu kufungua mitandao, hivyo ukifika kwa restaurant ya kichina unaweza itumia hii thread kuwaonesha wahudumu chakula utachochagua.
 
炒饭 (chǎofàn)

Huu ni wali uliokaangwa (kwa muonekano ni kama pilau kama ukiwekwa soya source) ambao mara nyingi huja katika aina mbalimbali mathalani wali uliokaangwa na nyama ya ng'ombe/kitimoto/kuku, wali uliokaangwa na mayai/mbogamboga/mahindi mabichi. Mchanyato huo wakati mwingine hujumuisha viungo vyenye harufu nzuri, pilipili hoho, karoti, pilipili wakati mwingine huweka Soya source ili kubadili rangi nyeupe ya wali na kuupa ladha murua.

1. Wali uliokaangwa na nyama ya ng'ombe huitwa - 牛肉炒饭 (niu rou chaofan)

2. Wali uliokaangwa na nyama ya kuku huitwa - 鸡肉炒饭 (ji rou chaofan)

3. Wali uliokaangwa na nyama ya kitimoto huitwa - 猪肉炒饭 (zhu rou chaofan)

4. Wali uliokaangwa na mayai huitwa - 鸡蛋炒饭 (ji dan chaofan

chaofan.jpg

Aisee sijawahi kula wali mtamu kama huu,nilikuwa nakula hata bila mboga...hasa ule wanaoweka na prawns halafu natafutia ile mishikaki yao ya kuku au bilinganya inayochomwa mtaani mida ya usiku
 
Aisee sijawahi kula wali mtamu kama huu,nilikuwa nakula hata bila mboga...hasa ule wanaoweka na prawns halafu natafutia ile mishikaki yao ya kuku au bilinganya inayochomwa mtaani mida ya usiku

Okay, ulikuwa mji gani huo?

Maana najua hizo streets za hivyo zipo karibia miji yote ya China.
 
Guangzhou,kuna kasehemu kanaitwa gangbei lu

Oooh!!

Nimefika sana Guangzhou ila mara nyingi nikitaka kula nilikuwa nala kwa migahawa ya Wahindi au Waarabu (maeneo ya Tian Xiu Lou ground floor) au wale jamaa wa Xinjiang (hapo ni mwendo wa dapanzhi).

Ulikuwa waishi huko, biashara au ulikuwa wasoma?
 
Nimekaa hapo mwaka mzima,nilienda kusoma ila niliishia kati nikarudi Tz.pale tian xiu kuna waTZ wanapika chakula cha kinyumbani nyumbani
 
Nimekaa hapo mwaka mzima,nilienda kusoma ila niliishia kati nikarudi Tz.pale tian xiu kuna waTZ wanapika chakula cha kinyumbani nyumbani

Okay.

Naam Tian Xiu alikuwepo jamaa mmoja anaitwa Ally ni Mzenji alikuwa anapika misosi ya kibongo, sina uhakika kama bado yupo.
 
Okay.

Naam Tian Xiu alikuwepo jamaa mmoja anaitwa Ally ni Mzenji alikuwa anapika misosi ya kibongo, sina uhakika kama bado yupo.

Sijajua hlf kipindi nipo wanawake wengi ndo walikuwa wanapika.kuna kipindi visa ilikuwa ngumu kupata wengi wakakimbilia hongkong
 
Back
Top Bottom