CHINESE CUISINE: Nini ule ukienda kwenye mgahawa wa kichina...

CHINESE CUISINE: Nini ule ukienda kwenye mgahawa wa kichina...

kwa kweli napenda sana mapishi ya kila aina na hii imenivutia the most naenda kuzijaribu hizi zote na spices najua ntapata super market,

thanks kwako utupaye hizi just give us more and more will be gratefully
 
nilpofka tu hapo kwenye "mbuzi katoliki" dah! Ushaniharibia ratiba ya leo watu8
 
Last edited by a moderator:
醋溜土豆丝 (cù liū tǔ dòu s&#299😉 - Chopped Potatoes with sour flavor


Hii chakula huwa ni viazi mviringo vilivyocharangwa na huchangwanywa kidogo na vinegar na pilipili. Kuna baadhi ya sehemu huwa wanaweka na karoti au hoho ambazo nazo huwa zimecharangwa mithili ya viazi.



2d9c7e4b90abdfa63b0d0639c05048e3.jpg
 
wikiendi hii na mie nimepanga kupika nyama ya ngombe na kujaribu kuweka na wine nione test yake best eti wine gani nidondoshee au hata hata spirit konyagi itanoga?

Dear i wish i could help, ila mimi si unajua mambo ya mapishi sijui kivile...hapa nawapa maujanja ya nini cha kula ukiingia mgahawa au hoteli za Wachina au ukipewa dinner ofa na Mchina.

napenda Chinese dumplings pia boiled crab ni tamu sana

Binafsi huwa sipendi kabisa hizo dumplings 'jiaozi' sijui kwa nini
 
黄瓜炒鸡蛋 (Huángguā chǎo jīdàn) - Cucumber with scrambled eggs

Hii ni mboga au saladi rahisi sana ambapo huwa na matango na mayai yaliyokaangwa. Wakati mwingine huwekwa pilipili na karoti.


5914522543_0a89fb8ce2_b.jpg
 
yani watu8 ur not serious yani mambo ya vyakula vya kichina iwekwe sticky.
My foot
 
Last edited by a moderator:
番茄菜花 (Fānqié càihu&#257😉 - Cauliflower mixed with Tomato

Kwa wale wapenzi wa mbogamboga mnaweza kuagiza mboga hii ya mchanyato wa nyanya na kolimaua. Huwa ni tamu sana haswa ukute imeongezewa viungo vya 'chicken bouillon'.


105QGW2-0.jpg
 
yani watu8 ur not serious yani mambo ya vyakula vya kichina iwekwe sticky.
My foot

This's a very special edition....not every Chinese meal is included.

Btw bandiko gani huwekwa sticky especially kwenye Jukwaa kama hili la JF Chef?
 
watu8 my dear ' xie xie'
af nikwambie kitu kwa sisi tunaopenda kukunja goti jikoni walahi ukishantajia ingredients za mlo tu ndo ushantajia recipe !
hahahahhahahhahha umenipa idea ya milo kama mitano hiv.
 
Last edited by a moderator:
Ahsante swahiba kwa uzi huu,mi napenda cuisines za mataifa tofauti kama hawa wachina,wathailand,waitaliano,wahindi na nigerians.....sasa je hii cabbage inapatikana kwenye supermarket zetu upande wa groceries?vingine vinapikika nyumbani...

kwa aliye mtundu na jiko hivi vyakula vilivyowekwa hapa na mtani wangu vinapikika kabisa home,na mazaga zaga yake yanapatikana kabisa supermaket au soko la tx pale kinondoni nafkir halitakosa haya makitu yooote.
hakikisha uwe na zile simple machines za jikoni kama kinyundo,greater, thing like vya kustyle salad na matunda basi unajipikilisha!
 
hii dressing yao ya msosi mie hoiii
eti amu ?
dah mi chakula kiniite kwa macho kwanza bana!
 
Last edited by a moderator:
watu8 my dear ' xie xie'
af nikwambie kitu kwa sisi tunaopenda kukunja goti jikoni walahi ukishantajia ingredients za mlo tu ndo ushantajia recipe !
hahahahhahahhahha umenipa idea ya milo kama mitano hiv.

'buyong xie' mtani...

Karibia 60% ya vyakula nilivyoweka hata mimi napika kwa kuwa niliwahi kupika nikiwa kwao mtani...

Kwa huku nyumbani sijafanya hilo zoezi kabisa ingawa kuna supermarkets najua zinauza viungo vya kuandaa baadhi ya hii minuso...

Pale K'koo karibu na kituo cha Bakhresa kuna mini supermarket moja kwa jina nimeisahau ila ipo kati ya Exim Bank na kituo cha Bakhresa huwa wanauza hii mambo ya viungo.

Halafu jaribu kutafuta kiungo kimoja kinaitwa "chicken bouillion", vegs nyingi za kichina huweka hii kitu na wakati mwingine huwekwa hata kwenye vitoweo.


1020-245745.jpg
 
.....sasa je hii cabbage inapatikana kwenye supermarket zetu upande wa groceries?vingine vinapikika nyumbani...

Hiyo chinese cabbage haipatikani huku kwetu umatumbini...

Kula kwangu na kuishi kote China sijawahi kuona cabbage inayofanana 100% na hii ya kwetu isipokuwa kuna aina fulani ya cabbage huitwa White Cabbage ndiyo walau yafanana na ya kwetu...nitaiweka hapa baadaye.

Ukiwa na viungo vyote, asilimia kubwa ya hivi vyakula niwekavyo vinapikika nyumbani...bahati nzuri uwepo wa Wachina Tanzania umeleta na mini-supermarkets kwa ajili ya mahitaji ya wachina.

Mkuu mimi nataka nijaribu kula konokono ,vyura na nyoka. .unaweza kupata menu yake nione kabla sijafanya maamuzi magumu?

Hahahah...mkuu nikiweka picha ya hizo menu hapa nitakuwa nimeharibu dhima nzima ya uzi huu...kama unatumia PC, copy hayo majina ya kichina hapo chini halafu google search images zake.

Nyama ya chura huitwa 青蛙肉 - Qīngwā ròu, mara nyingi huwa anatengenezwa kama supu(mchemsho) au anakaangwa kwa mafuta.
Nyama ya konokono huitwa 蜗牛肉 - Wōniú ròu, mara nyingi hutengenezwa kama supu au hupikwa kama roast
Nyama ya nyoka huitwa 蛇肉 - Shé ròu, hii hubanikwa, hukaangwa n.k
 
kwa aliye mtundu na jiko hivi vyakula vilivyowekwa hapa na mtani wangu vinapikika kabisa home,na mazaga zaga yake yanapatikana kabisa supermaket au soko la tx pale kinondoni nafkir halitakosa haya makitu yooote.
hakikisha uwe na zile simple machines za jikoni kama kinyundo,greater, thing like vya kustyle salad na matunda basi unajipikilisha!

nimecheka sana eti nyundo nyundo tumia mtwangio wa kinu bana watu watachukua linyundo la misumari wagongee nyama
 
hii dressing yao ya msosi mie hoiii
eti amu ?
dah mi chakula kiniite kwa macho kwanza bana!

kweli kabisa na mie kikiwa machoni hakieleweki wallah hakipiti napataga tabu sana nkienda nyumba za watu ambao kupika kwao ni adhabu!!full kushinda na njaa daaa
 
Last edited by a moderator:
Mkuu, sangara hafai kuchemsha, kwa samaki wa ziwa anaefaakuchemsha ni Mboju
 
sa mdau kibongo bongo mgahawa gani wa kichina mzuri...maana nataka kula point 3 kwa mtoto mmoja nikimpeleka dinner...picha nakua mi ndio starling najifanya najua majina ya kichina ya misosi ka Jack Chen vile.
Ila niambie katika hiyo list uliyotoa kwa hela za madafu hipi expensive hipi kawaida..maana sio unaenda dinner inakucost gharama ya kununua vits
top_intro_pic_chinese.jpg

Katika ulimwengu wa vyakula na mapishi kuna aina mbalimbali ya vyakula ambavyo upande mmoja wa dunia vinaweza kuwepo na upande mwingine kukosekana.

Ukiachana na hilo pia kuna jambo moja inabidi tutambue kuwa sehemu kubwa ya dunia aina ya raw materials za vyakula ni ile ile lakini namna ya upikaji ndio hutofautiana.

Katika thread hii ningependa kuweka bayana baadhi ya vyakula vilivyopikwa kwa recipes za kichina ambavyo Mtanzania na Muafrika yoyote anaweza kula pasipo kupata tabu ya ladha.

Kwa wale waliopo nyumbani Tanzania wanaweza kuingia kwenye Migahawa ya Kichina iliyopo huko na kuagiza hizi menu vivyo hivyo na kwa wale waliopo nje ya Tanzania.

NB:
Vyakula vingi vya kichina hupikwa kwa mtindo wa mboga ambapo ulaji wake huambatana na wali 'steamed rice' (huu hauwekwi mafuta wala chumvi), mikate ya kichina (mantou), tambi za kichina (miantiao) n.k..
Hivyo hakikisha uagizapo dishes hizi unaagiza na kimojawapo cha hivyo, lakini mimi nashauri muagize wali kwani ndio wengi wetu tumeuzoea.

Thread hii haitaelekeza namna ya upikaji wa chakula chochote cha Kichina bali itakupa mwangaza tu wa nini uchague utapoingia katika mgahawa wa Kichina.

Pia naomba sana mkuu Invisible na X-PASTER kwa heshima na taadhima thread hii uiweke kama Sticky thread ili iwe msaada kwa wananchi wengi.
 
Last edited by a moderator:
watu8 naumbuka ndugu angu dinner day inakaribia afu ticha umenikimbia ntapata div 5 sasa..
 
Last edited by a moderator:
Back
Top Bottom