best r mhapa
New Member
- Oct 26, 2013
- 1
- 1
wikiendi hii na mie nimepanga kupika nyama ya ngombe na kujaribu kuweka na wine nione test yake best eti wine gani nidondoshee au hata hata spirit konyagi itanoga?
napenda Chinese dumplings pia boiled crab ni tamu sana
Ahsante swahiba kwa uzi huu,mi napenda cuisines za mataifa tofauti kama hawa wachina,wathailand,waitaliano,wahindi na nigerians.....sasa je hii cabbage inapatikana kwenye supermarket zetu upande wa groceries?vingine vinapikika nyumbani...
watu8 my dear ' xie xie'
af nikwambie kitu kwa sisi tunaopenda kukunja goti jikoni walahi ukishantajia ingredients za mlo tu ndo ushantajia recipe !
hahahahhahahhahha umenipa idea ya milo kama mitano hiv.
.....sasa je hii cabbage inapatikana kwenye supermarket zetu upande wa groceries?vingine vinapikika nyumbani...
Mkuu mimi nataka nijaribu kula konokono ,vyura na nyoka. .unaweza kupata menu yake nione kabla sijafanya maamuzi magumu?
kwa aliye mtundu na jiko hivi vyakula vilivyowekwa hapa na mtani wangu vinapikika kabisa home,na mazaga zaga yake yanapatikana kabisa supermaket au soko la tx pale kinondoni nafkir halitakosa haya makitu yooote.
hakikisha uwe na zile simple machines za jikoni kama kinyundo,greater, thing like vya kustyle salad na matunda basi unajipikilisha!
Katika ulimwengu wa vyakula na mapishi kuna aina mbalimbali ya vyakula ambavyo upande mmoja wa dunia vinaweza kuwepo na upande mwingine kukosekana.
Ukiachana na hilo pia kuna jambo moja inabidi tutambue kuwa sehemu kubwa ya dunia aina ya raw materials za vyakula ni ile ile lakini namna ya upikaji ndio hutofautiana.
Katika thread hii ningependa kuweka bayana baadhi ya vyakula vilivyopikwa kwa recipes za kichina ambavyo Mtanzania na Muafrika yoyote anaweza kula pasipo kupata tabu ya ladha.
Kwa wale waliopo nyumbani Tanzania wanaweza kuingia kwenye Migahawa ya Kichina iliyopo huko na kuagiza hizi menu vivyo hivyo na kwa wale waliopo nje ya Tanzania.
NB:
Vyakula vingi vya kichina hupikwa kwa mtindo wa mboga ambapo ulaji wake huambatana na wali 'steamed rice' (huu hauwekwi mafuta wala chumvi), mikate ya kichina (mantou), tambi za kichina (miantiao) n.k..
Hivyo hakikisha uagizapo dishes hizi unaagiza na kimojawapo cha hivyo, lakini mimi nashauri muagize wali kwani ndio wengi wetu tumeuzoea.
Thread hii haitaelekeza namna ya upikaji wa chakula chochote cha Kichina bali itakupa mwangaza tu wa nini uchague utapoingia katika mgahawa wa Kichina.
Pia naomba sana mkuu Invisible na X-PASTER kwa heshima na taadhima thread hii uiweke kama Sticky thread ili iwe msaada kwa wananchi wengi.